ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 26 Juni 2015

Mwanafunzi chuo kikuu mkwawa kugundua dawa ya ukimwi, je kunani?



 Image result for wasomi

 Wanafunzi wa chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa wamegundua dawa ya Maradhi ya Ukimwi, wamedai hadi sasa mtu mmoja Kapona. Ni wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo, nini maoni yako katika ugunduzi huu?
 je unadhani kiunahaja ya kuendelezwa kama mataifa ya ulaya?
 tanzania ni nchi nyenye watafiti wengi lakini changamoto ni ukasumba wa tasisi husika kushindwa kuwatumia
TUPE MAONI YAKO HAPA NINI KIFANYIKE, KUPITIA misaelkikoti11@yahoo.com

Wanafunzi waunda kondomu inayotambua magonjwa ya zinaa


Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.

Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .

Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''

''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''

Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.

Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa

"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu'

Joseph Mbilinyi ‘ Anena Bungeni

 Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alivyosimama na maneno yake Bungeni baada ya ishu ya mtoto wake kuzungumzwa.

Sugu 11 
Kwenye kilichosikika jana June 25 2015 toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma ilikuwepo pia ishu ya Mbunge Martha Mlata kuanzisha mjadala kuhusu amri ya Mahakama kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi Sugu akabidhiwe mtoto wake ambae amezaa na Faiza Ally kutokana na Mbunge huyo kuonekana kutoridhwishwa na malezi ya mtoto akiwa kwenye mikono ya mama yake.
Ombi likapokelewa kwenye meza ya Naibu Spika leo June 26 2015 >>>”Nimepokea ombi maalum la kuwasilisha maombi binafsi kutoka kwa Mbunge Joseph Mbilinyi kwa hiyo namruhusu” >>> Naibu Spika Job Ndugai.
“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo”
Mama Sasha
“Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia“
“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“
Sugu 6
Sugu na mwanae Sasha
“Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito“
Sugu 10 
Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge
Sugu 7 
Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niliwasilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge
“Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa”
Sugu 9

Ijumaa, 19 Juni 2015

Mamlaka ya Mji Mdogo Ilula

  

Na waandishi wetu, Longo na Kikoti


kata ya Ilula inamitaa ya Ilula-Itund, Masukanz, Igunga, Ikokoto, Madizini.


kata Nyalumbu ina mitaa ya Ilula-Mwaya,Ikuvala, Mtua, Ding'inayo, Ngelango, Ilula Sokoni,

Itabali,Matalawe


kata ya Mlafu ina mitaa ya Mlafu,Isagwa,Itungi

MATATIZO YANAYOUKUMBA MJI MDOGO WA ILULA


Tatizo la maji



Maji ni uhai na maji yana matumizi mengi katika maisha ya kila siku ya binadamu,

wanyama na hata viumbe vingine hai,ikiwemo mimea.Lakini kwa wakazi wa

Mji Mdogo wa Ilula uliopo Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, upatikanaji

wa maji kwao ni kitendawili cha miaka mingi sasa kwani ni tatizo sugu.

Ilula ni mji unaosifika kwa biashara mbalimbali hususan zao la nyanya na

vitunguu, hali inayoufanya uwe na mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka

maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wanaokwenda kwa shughuli

za kilimo na biashara.

Sababu za uhaba wa maji ilula

- kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu ukiringanisha na miundo

mbinu ya maji iliyopo katika-mji huo, pia suala la ubovu wa miundo

mbinu ya maji imeonekana ni tatizo kwani mingi imeharibika na-

hakuna jitihada zozote za kuirekebisha .

- pia sababu inayochangia uhaba wa maji katika mji huu ni-

pamoja na uharibu wa vyanzo vya maji; hasa katika chanzo

cha idemule.

je jitihada gani zimechukuliwa na serikali?

Serikali imejitahidi kuboresha miundombinu ya chanzo cha Idembe,

na imeanza kufanya upembuzi wa-awali ili kutumia vyanzo mbadala

vya mto Mgombezi na milima ya Selebu na kuchimba visima vingi

vya maji katika mji huo. akizungumza na wananchi waziri wa maji

alisema Profesa Maghembe wizara yake imekwishatoa Sh Milioni -

150 na itaongeza nyingine Sh Milioni- 150 ili kuboresha miundombinu-

ya chanzo cha Idembe.

Tatizo jingine ni miundombinu ya barabara za mitaani.

barabara za mitaani katika mji huu wa ilula bado ni tatizo kubw

hasa katika maeneo ya mtua, sokoni na isele na hii inatokana na

kutokuwepo mipango yakinifu iliyoweka na serikali ili kuzuia

wanajamii kujenga katika maeneo hayo ambayo barabara za


mitaani zinapaswa kujengwa, hivyo kusababisha hatari kumbwa

hasa kwa wananchi ikiwa hatari ikitokea kama ajari ya moto,

uwepo wa wagonjwa wanaohitaji msaada wa gari inakuwa ni

tatizo kwani hakuna barabara zinazoruhusu- magari kupita

kwa urahisi.


Je serikali imefanya jitihada gani?


suala la barabara za mitaani linaonekana kuendelea kufumbiwa-

macho, licha ya baadhi ya mitaa hasa Majengo mpya serikali

kutengeneza barabara ili kuzuia wanaojenga wasijenge lakini

wanashinda kutatua changamoto ya sehemu ambazo tayari

watu wameziba barabara hizo za mitaani.


Je ungekuwa we ungeshauri nini?


Sheria za barabara za mitaani zinatambulika vizuri, kwa hiyo;

ni vizuri serikali ikachukua hatua mapema kwa kuangalia

watu waliojenga maeneo hayo ya hifadhi za barabara za

mitaani na kuwachukulia hatua, na kama serikali ilifanya

makosa katika ugawaji wa maeneo bila kuacha maeneo

ya hifadhi ya barabara itafute njia ya kupata ramani

ambapo barabara zinatakiwa kupita na kulipa fidia

kwa jamii itakayoathirika na zoezi la upitishaji wa

barabara za mitaani ilula.













Jumanne, 16 Juni 2015

Hii ndo elimu bora

Elimu Bora ni ile inayozingatia masuala yafuatayo;

Image result for elimu boraImage result for elimu bora 
Hali ya Wanafunzi
Je, wako tayari na wanaweza kushiriki katika elimu yao? Je, wanapata ushirikiano kutoka kwenye familia na jamii zao?
Mazingira ya Kujifunzia
Je, ni salama kwa watoto wote bila kujali jinsia, imani na ulemavu? Je, vifaa kama vile madawati, vyoo na vitabu vinatosheleza mahitaji yote?
Mambo yanayofundishwa Darasani
Ni aina ipi ya ujuzi ambao Mitaala inatilia mkazo? Je, maudhui yake yanaendana na mahitaji ya jamii? Je, yanakuza uelewano, umoja, amani na haki za binadamu?
Walimu na Ufundishaji
Je, kuna walimu wa kutosha na wako tayari kufundisha? Je, ufundishaji unamjali mwanafunzi, na mahuasiano kati ya wanafunzi na mwalimu darasani yakoje?
Matokeo ya Elimu
Wahitimu wana aina gani ya maarifa, ujuzi na mtazamo? Na wanayatumiaje katika maisha yao ndani ya jamii?

Jumatatu, 8 Juni 2015

Waliochukua fomu urais kupitia CCM wafikia 18


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akionyesha begi lenye fomu za kuomba kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Makada watatu wa CCM jana walijitokeza katika makao makuu yake mjini hapa kuchukua fomu kuomba kupewa ridhaa na chama hicho ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
Waliochukua fomu jana ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kada wa chama hicho, Leonce Mulenda na Ofisa Mwandamizi mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Peter Nyalali na kufanya idadi ya wanaCCM waliokwisha fanya hivyo kufikia 18.
Nyalandu: Ninafahamu changamoto
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyalandu ambaye alisindikizwa na wabunge wa viti maalumu, Mary Chatanda na Martha Mlata alisema amechukua fomu akifahamu umuhimu wa kuyaendeleza yote yaliyofanywa na serikali ya awamu ya nne... “Ninafahamu changamoto zinazotukabili. Nazitazama, naziona hatua ambazo zipo tangu wakati wa Baba wa Taifa alipomkabidhi kijiti Rais Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete.”
Alisema anafahamu changamoto zinazolikabili Taifa na anaitazama nchi iendelee kulinda misingi iliyoachwa na waasisi wa Taifa kwa kuendeleza amani.
Alisema umoja, undugu na mshikamano atakaoulinda, utaifanya Tanzania iwe na nguvu ya kutatua changamoto za sasa na za kesho.
Huku akipigiwa makofi na wapambe wake, Nyalandu alisema waliambiwa zamani kuwa wazee wanaotawala vyema wanastahili heshima maradufu.
“Tutaendelea kuwaenzi wazee waliotutawala, wamekuwa wakitulea katika miji na vijijini, tutaendelea kuwaangalia vijana na wanawake kwa kuangalia nini ambacho tumefanikiwa katika awamu hii ya Rais Kikwete. Tutaangalia mageuzi tutakayoyafanya ili kijana wa Kitanzania aonekane si mzigo,” alisema.
Alisema endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo, serikali yake itajikita katika kuinua uchumi wa nchi.
“Tutajikita katika kuwekeza katika rasilimali watu, kuwawezesha wananchi kiuchumi… na sisi wenyewe kama Taifa tutasimama kwa miguu yetu. Tutatembea vichwa vikiwa vimesimama imara tuishangaze dunia kwa pamoja,” alisema.
Jambo jingine ni kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na uwezo wa kujilinda na raia wake.
“Tutaendelea kuhakikisha mifumo ya matatizo ikiwa ni pamoja na magonjwa, tatizo la Ukimwi, mshtuko wa ebola tulioupata ambao ulitetemesha utalii duniani, changamoto za kigaidi, tutajipanga kama Taifa na kama umoja kuhakikisha tunakabiliana nazo,” alisema.

Nyalandu alisema njia bora ya kuwawezesha watu ni kuboresha mfumo wa elimu ambao umefanikiwa chini ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Alisema  endapo atafanikiwa katika safari yake hiyo ya kuutafuta urais, atahakikisha kila shule ya msingi na sekondari inakuwa na kitengo cha mafunzo stadi.
Alipoulizwa iwapo chama kingine cha siasa kitashinda upande wa pili wa Muungano, alisema: “Ni muungano wa mapenzi ya ndani, ni muungano ambao unazidi tofauti zetu za dini, kabila na uwepo wa Bara na Visiwani na hali kadhalika, unazidi tofauti zetu za itikadi za vyama.”
Alisema atashirikiana na viongozi wa Zanzibar katika kuuenzi Muungano wa Tanzania ili uwe ishara ya amani na mshikamano.
Mulenda: Kipaumbele ni elimu bora
Mulenda (41) amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake kugombea urais huku akisema kipaumbele chake cha kwanza ni elimu bora.
Kada huyo ambaye alisindikizwa na watu wasiozidi sita, alisema kaulimbiu yake ni Serikali sikivu, makini na inayojali shida za watu.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Makao Makuu ya CCM, Mulenda alisema amejitathmini na kujipima kuwa anaweza kuwa kiongozi wa Tanzania. Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni kuhakikisha CCM inakuwa imara zaidi.
“Kwa upande wa chama nitahakikisha  nasimamia kwa vitendo katiba ya chama, kanuni na taratibu bila kuacha sheria na miongozo inayoongoza nchi yetu,” alisema.
Alisema atasimamia uamuzi wa vikao na kuhakikisha unatekelezwa na kupima matokeo kwa kufanya tathmini juu ya malengo waliyojiwekea.
Mulenda alisema endapo atashinda na CCM ikawa ndicho chama tawala, atakuwa na kazi ya kuisimamia Serikali.
“Ukiona Serikali inafanya vibaya na chama kinachotawala kinaona sawasawa, basi siku za kukaa madarakani za chama hicho zinahesabika,” alisema.
Alisema endapo atafanikiwa katika safari yake hiyo, atahakikisha Serikali yake kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM inakuwa sikivu, makini na inayojali shida za watu.
“Nawahakikishia wananchi kuwa kwa kutambua shida zao ni dhahiri nitajua wanataka nini na hawataki nini na kwa msingi huo, Serikali itakayokuwa chini yangu wakati wote tunahakikisha Watanzania tunawapeleka kule wanakotarajia kwa kutumia uwezo wetu ambao ulijengwa na waasisi wa Taifa hili,” alisema.
Alisema wazee waliwaambia kuwa nchi ina raslimali za kutosha na kinachotakiwa ni kujiongoza ili kutumia amani na utulivu kujenga nchi.