HOMA ya pambano la raundi ya kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika kati
ya Yanga na APR ya Rwanda, imezidi kupanda, kiasi cha kila moja kutamba
kumshikisha adabu mpinzani wake.
Tayari makocha wa klabu hizo, Hans van der Pluijm wa Yanga na Nizar
Khanfir wa APR aliyeweka rekodi ya kuwa mwarabu wa kwanza kufundisha
soka Rwanda baada ya kuanza kazi rasmi jana, ameelezea utayari wake
kushinda mechi ya Jumamosi wiki hii huko Kigali, Rwanda.
Khanfir amekaririwa jana kuwa, ameshawaona Yanga kupitia video
mbalimbali na kwamba anataka kuwafunga Jumamosi. “Lengo letu ni kushinda
huo mchezo,”amesema na kuongeza; “Nimeona baadhi ya video zao na
tutaendelea kuwachambua katika siku chache zijazo kuelekea kwenye
mechi”.
Kwa ujumla, Khanfir amesema malengo yake makuu katika miezi sita ya
mwanzo ni kuiwezesha timu kutetea ubingwa wa Rwanda na pia kuifikisha
mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Mtaalamu huyo wa Tunisia aliongoza
mazoezi yake ya kwanza APR jana Uwanja wa Kicukiro akisaidiwa na kocha
aliyemkuta kazini, Emmanuel Rubona.
“APR ni timu kubwa Rwanda na ina heshima kubwa Afrika na pia ina
wachezaji wengi katika timu ya taifa, ambacho ndicho kilichonivutia mimi
kukubali kazi hii,” amesema Khanfir. “Wachezaji ni vijana wadogo na
timu ina uwiano mzuri ambao unafaa vizuri katika falsafa yangu.
Tunaitaka kuipeleka timu katika kiwango kingine.
Ni wajuzi na tunataka kuongeza ufundi zaidi, lakini zaidi ya hapo
nimevutiwa na timu kwa ujumla,” amesema. Wakati Khanfir akisema hayo,
Pluijm kwa upande wake amesema anatambua wanakwenda Kigali kwenye mchezo
mgumu wa ugenini dhidi ya APR, lakini watapambana wasipoteze.
“APR ni timu nzuri na watakuwa wamejiandaa vizuri, lakini sisi tuko
vizuri, tutakwenda kupambana tusipoteze mchezo, ili tumalizie vizuri
mchezo wa nyumbani,”amesema. Yanga SC inatarajiwa kuondoka leo nchini
kwenda Kigali kwa ajili ya mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa
kusisimua.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezeshwa na marefa wa Malawi Jumamosi
Uwanja wa Amahoro, Kigali Rwanda. Duncan Lengani anatarajiwa kupuliza
filimbi, wakati washika vibendera watakuwa Clemence Kanduku na Jonizio
Luwizi.
Mchezo wa marudiano wiki moja baadaye Dar es Salaam, utachezeshwa na
marefa wa Shelisheli; katikati Bernard Camille na pemebeni watakuwapo
Eldrick Adelaide na Gerard Pool.
Mchezo wa kwanza utafanyika mjini Kigali, Rwanda Machi 12 kabla ya
timu hizo kurudiana Dar es Salaam Machi 19 na mshindi wa jumla atakutana
na mshindi wa mchezo mwingine wa raundi ya kwanza, kati ya Al Ahly ya
Misri na Recreativo de Libolo ya Angola mwezi ujao.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako ameingilia kati mgogoro wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.
Joseph Dar es Salaam, waliogomea kufanya mitihani na kuwataka warejee
madarasani wakati matatizo yao yakishughulikiwa.
Wanafunzi hao walikuwa katika siku ya tatu ya mgomo wao jana ambapo
pamoja na mambo mengine walikuwa wakilalamikia mapungufu yaliyopo chuoni
hapo, ikiwa ni pamoja na maabara za kufanyia mafunzo kwa vitendo,
matatizo ya kiutawala, mitaala ya kufundishia pamoja na ada.
Profesa Ndalichako aliwasili chuoni hapo jana asubuhi na kukagua
mazingira ya kufundishia ya chuo hicho kwa kutembelea maabara zote
chuoni hapo na kisha kwenda kuzungumza na utawala, Serikali ya wanafunzi
na mwisho alihutubia wanafunzi wote.
Ndalichako baada ya kuzungumza na pande zote mbili aliagiza wanafunzi
hao warejee madarasani kuendelea na mitihani yao na kuutaka uongozi wa
chuo uyafanyie marekebisho mapungufu ya kiutawala yaliyojitokeza.
Aidha ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), chini ya Katibu
Mtendaji wake, Profesa Yunus Mgaya kufuatilia na kuchunguza kwa makini
madai ya wanafunzi hao juu ya kuwepo kwa wahadhiri wasio na sifa
zinazotakiwa.
RAIS John Magufuli amesema anatamani mafanikio ya nchi ya Vietnam
kiuchumi na kubainisha kuwa ziara ya Rais wa nchi hiyo, Truong Tang Sang
nchini, ni fursa na changamoto kwa watanzania kujifunza mambo mengi,
yatakayosaidia kukuza pia uchumi wa Tanzania.
Aidha amehamasisha Watanzania kuchangamkia fursa na rasilimali
zilizopo nchini katika kujiinua na kuimarisha nchi yao kiuchumi. Alisema
Tanzania ni miongoni mwa nchi tajiri kwa rasilimali na fursa nyingi,
ingawa bado iko nyuma kimaendeleo. Kwa upande wake, Rais Sang amesema
nchi yake na Tanzania zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya
biashara, kilimo, viwanda na uvuvi lengo likiwa ni kuhakikisha nchi zote
zinanufaika kwenye ushirikiano huo.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na marais hao Ikulu
Dar es Salaam jana, Dk John Magufuli alisema ni wakati sasa wa Tanzania
kujifunza kutoka kwa nchi hiyo ya Vietnam ambayo pamoja na kukabiliwa
na vita ya muda mrefu, imefanikiwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi
wa kati. “Ukweli ni kwamba ziara ya Rais Sang nchini kwetu ni muhimu
sana na imekuja kwa wakati muafaka.
Mwaka 1976 Rais wa Vietnam alikuja nchini na alichukua mbegu ya
korosho na kuipeleka nchini kwake, na leo hii Vietnam ni moja ya nchi
zinazoongoza kwa kuzalisha korosho duniani,” alisema. Alitaja mafanikio
mengine ya nchi hiyo ni pamoja na kuwa na uchumi wa kati, licha ya
kukabiliwa na mapigano ya muda mrefu. Ilipata uhuru wake mwaka 1945 na
ilidumu kwenye mapigano hadi Julai 2, mwaka 1976.
Alisema mwaka 1977 mapato ya kila raia wake yalikuwa ni dola 100,
lakini sasa imefanikiwa kupandisha mapato hayo na sasa kila raia wa nchi
hiyo mapato yake ni dola 2000 kwa mwaka na imepunguza kiwango cha
umasikini kwa asilimia 50. “Sisi tangu mwaka 1960 bado tuko kwenye nchi
masikini, kwa hiyo hii ni changamoto kwa nchi yetu. Tunatakiwa kujifunza
kuondokana na hali hii.
Wao uzalishaji kwa mchele wanalima mara tatu kwa mwaka, sisi tunalima
mara moja tu na inawezekana uzalishaji wetu ni mdogo sana,” alisema.
Alisema nchi hiyo pamoja na kuchukua mbegu ya korosho nchini, ndio nchi
inayoongoza kwa kuzalisha korosho duniani, wakati Tanzania ndio iliyotoa
mbegu hiyo, zao hilo badala ya kuzalishwa kwa wingi ndio uzalishaji
wake unafifia.
“Samaki sina uhakika kama walichukua huku, lakini leo hii Vietnam ni
wazalishaji wa samaki wakubwa sana. Lakini kwa nchi yetu ambayo ina
maziwa 21 na mito kila mahali na bahari lakini uzalishaji wa samaki uko
chini…” “Tuna ng’ombe zaidi ya bilioni 22 hadi bilioni 23 nafikiri
tunaweza kuwa wa pili barani Afrika baada ya Ethiopia, lakini ngozi zetu
za viatu hapa tunaagiza nje.
Kwa hiyo kwa hili watanzania tunatakiwa tusiogope kujifunza kwa wale
waliotutangulia ili na sisi nchi yetu iweze kufika mahali pazuri,”
alisisitiza Dk Magufuli. Alisema ujio wa Rais Sang pamoja na ujumbe wake
wa zaidi ya mawaziri takribani 20 na wafanyabiashara ni wakati pekee wa
Watanzania na wa Vietnam, kuimarisha ushirikiano uliokuwepo kwa zaidi
ya miaka 50 sasa kuhakikisha uhusiano unaleta maendeleo kwa pande zote.
“Ziara hii ni muafaka kwetu sisi watanzania kujenga uhusiano mzuri na
nchi ya Vietnam ili kuweza kujifunza na sisi tuweze kufikia lengo letu
la kuwa nchi ya kipato cha kati,” alisema. Pamoja na hayo, Rais Magufuli
alisema katika mazungumzo yake na Rais wa Vietnam alipata mwaliko wa
kutembelea nchi hiyo mwakani. “Kwa kweli mwaliko huu nimeupokea na
ninajisikia kuthaminiwa na kuheshimiwa sana,” alisema.
Kwa upande wake, Rais Sang alisema anajisikia fahari kuona uhusiano
kati ya Tanzania na nchi yake unaimarika. Alisisitiza kuwa uhusiano na
ushirikiano huo utaleta maendeleo ya dhati baina ya nchi hizo mbili.
Alipongeza serikali kupambana dhidi ya umasikini kwa kusisitiza kuwa
inafanya vizuri kiuchumi kwani ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo
uchumi wake unakua kwa kasi.
“Kama rafiki wa karibu tunavutiwa na maendeleo yenu hasa katika
kupambana na umasikini lakini pia ukuaji wa kasi wa uchumi wenu. Katika
mazungumzo yetu na Rais Magufuli tumezungumzia masuala mbalimbali ya
maendeleo, ikiwemo kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kilimo,
biashara na viwanda,” alisema rais huyo. Aidha, alisema uhusiano wa nchi
hizo mbili ni wa muda mrefu, kwani pamoja na umbali wa kijiografia
Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na
Vietnam.
Alisema ziara hiyo ni moja ya njia za kudumisha na kuboresha zaidi
uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. Rais huyo alisema
kwenye mazungumzo yake na Magufuli, wamekubaliana kushirikiana katika
maeneo yatakayonufaisha nchi zote. Maeneo hayo ni kilimo, biashara,
viwanda na mawasiliano. Pia walisaini mikataba ya kutowatoza kodi mara
mbili wawekezaji na wafanyabiashara wanaowekeza katika nchi hizo.
Aidha Rais huyo alisema katika kikao chake na Rais Magufuli pamoja na
mawaziri wa nchi zote mbili wamekubaliana kuanzisha tume ya pamoja
itakayosimamia masuala ya uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo
mbili. Aidha marais hao walizungumzia masuala ya kimataifa ambapo wote
kwa pamoja walikubaliana suala la kuhakikisha amani na utulivu linapewa
kipaumbele na mataifa yote duniani.
“Tulikubaliana kuwa nchi zote zina wajibu wa kuhakikisha suala la
amani linapewa kipaumbele, ikiwemo na mataifa ya kimataifa kuwa mstari
wa mbele katika kuhamasisha na kutuliza vurugu zinazoibuka katika nchi
mbalimbali,” alisema. Alisisitiza kuwa amemwalika Rais Magufuli
kutembelea Vietnam wakati wowote. Tayari Marais wastaafu Benjamin Mkapa
na Jakaya Kikwete, walishafanya ziara katika nchi hiyo wakati wa utawala
wao.
Rais Sang aliyeongozana na ujumbe wa watu 51 ataendelea kuwepo nchini
kwa ajili ya kumalizia ziara yake katika maeneo mbalimbali, ikiwemo
kutembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA).
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaalika wawekezaji kutoka
Vietnam na kuwahakikishia kuwa Tanzania ni nchi inayoheshimu uwekezaji
na kwamba Serikali imesaini mikataba mbalimbali ya kupinga kutaifisha
mali za wawekezaji.
Majaliwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana kwenye kongomano baina ya
ujumbe wa Tanzania na Rais wa Vietnam, Truong Tan San aliyeongozana na
ujumbe wake katika ziara ya siku nne nchini na wafanyabiashara wa
Tanzania.
Waziri Majaliwa alisema Tanzania ni nchi yenye mazingira mazuri ya
uwekezaji katika nyanja mbalimbali na kusisitiza kwamba wanaotaka
kuwekeza nchini wanafurahia mazingira hayo na uwepo wa dhamana ya mitaji
waliyowekeza.
“Ukiwekeza Tanzania una uhakika wa usalama wa mtaji na uwekezaji wako
kwa sababu nchi imesaini mikataba mbalimbali ya kupinga utaifishaji
mali za wawekezaji na kuhimiza uwekezaji wa kigeni katika mazingira
salama na yenye amani,” alisema Majaliwa.
Alisema kila mara nchi imekuwa ikiboresha sheria na kuimarisha
ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kuchochea mazingira ya uwekezaji kwa
lengo la kuimarisha uchumi na kuinua maisha ya wananchi wake.
Akizungumzia soko mara baada ya kuwekeza nchini, Waziri Majaliwa
alisema, wawekezaji wanaowekeza nchini wana uhakika wa masoko ya zaidi
ya watu milioni 300 waishio Mashariki na Kusini mwa Afrika, ambao
hufurahia kuwepo kwa nchi katika Jumuiya kama ya SADC na EAC.
Aidha, nchi zaidi ya sita ambazo hazina bahari hutegemea bandari ya
Tanzania kufanya biashara na masoko katika eneo hilo. Akizungumzia
uwekezaji kutoka nje ya nchi, Waziri Majaliwa alisema serikali imekua
ikiboresha mazingira ya uwekezaji na hiyo imeongeza uwekezaji kutoka
nje.
Alisema mfano mzuri ni uwekezaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania Ltd, ambao ni wawekezaji kutoka Vietnam
Ndalichako: Vyeti Vya Form Six Vilivyo Katika Mfumo wa GPA Havitabadilishwa Kwenda Division
Serikali
imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato
cha sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda
Divisheni.
Msimamo huo wa serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.
Amesema
serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali
wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo.
“Hatuwezi
kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho
madogo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili
kwenda mfumo wa divisheni,” alisema.
Februari
mwaka huu, Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), lilitangaza kusitishwa
kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka
2015, huku likiagiza kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao
vinatakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho.
Hata
hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk, Charles Msonde, hakubainisha
marekebisho ambayo wanatakiwa kuyafanya kwenye vyeti hivyo na badala
yake kudai baraza linataka kujiridhisha na baadhi ya vitu.
Hatua
hiyo ya kubadili vyeti hivyo iliibua utata mkubwa, huku baadhi ya wadau
wakiwamo maofisa elimu, wakihisi Necta huenda inalenga kuvibadili vyeti
hivyo kutoka kwenye mfumo wa wastani wa alama (GPA), kwenda kwenye ule
wa jumla (division).
Atupwa Jela Miaka 7 kwa Kumkata Mkewe Sehemu za Siri Ili Apate Mali
Kikoti blog
Mkazi
wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa
kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe
kwa imani za kishirikina ili apate mali.
Hakimu
Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.
Hakimu
Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho
kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za
kishirikina.
Awali
wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa
jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika
eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Wakati
wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni
mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu
za siri za mkewe atapata Sh5milioni.
Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili huo.
Alidai
baada ya kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri
mkewe na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.
Alidai
kwa mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele
kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.