ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 26 Aprili 2016

Vyama vyakacha kuwasilisha hesabu NI CUF tu waliowasilisha

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 iliyotolewa jana mjini hapa inaonesha kuwa kati ya vyama 22 vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja pekee ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa ajili ya ukaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Profesa Mussa Asaad alitaja Chama cha Wananchi (CUF) , ndicho kimewasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari mwaka 2015 hadi Juni mwaka huo.
Alisema vyama vingine 21 vimeshindwa kufanya hivyo hali ambayo amemshauri Msajili wa vyama hivyo kufuatilia jambo hilo. “Ripoti hii inabainisha kwamba vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni 22, lakini hadi Juni mwaka 2015, vyama vilivyowasilisha hesabu zao kwa ukaguzi ni chama kimoja tu cha CUF, sasa hivi vingine vimekiuka sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992”, alisema Profesa Asaad.
Akizungumzia udhaifu mwingine ambao umebainika katika ripoti hiyo Profesa Asaad aliweka hadharani Balozi mbalimbali za Tanzania nje, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Ripoti ya CAG yaanika majipu

Imeandikwa na Ikunda Erick, Dodoma. MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametoa ripoti ya ukaguzi wa hesabu ya mwaka 2014/15 iliyoibua kasoro nyingi kwenye taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali huku halmashauri zikibainika kuwa na ‘madudu’ mengi.
Ripoti hiyo inaonesha kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia zina hati zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu. Kwa upande wa mashirika ambayo ripoti hiyo imeyagusa, Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limebainika mauzo ya hisa zake yalikuwa batili, hivyo CAG ameshauri lirudi chini ya usimamizi wa serikali hadi hapo mgogoro wa mgawanyo wa hisa utakapotatuliwa.
Kuhusu Wakala wa Usafiri wa Mwendo wa Haraka Dar es Salaam (DART), ripoti ya CAG imebaini kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 wakala huyo aliingia mkataba na UDA-RT wa kutoa huduma ya usafiri wa mpito wa kuendesha mabasi 76 kulingana na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Lakini, Sheria ya Manunuzi ya Umma, mkataba huo ulitoa ongezeko la ununuzi wa mabasi na kufikia 84 ili kulingana na matakwa ya DART. Hata hivyo kwenye ukaguzi wa hesabu zao, CAG alibaini kuwepo na ununuzi wa mabasi 140 ambayo ni sawa na ongezeko la mabasi 56 yasiyo ndani ya mkataba.
Na kwamba pamoja na makosa hayo, pia ilibainika kuwa mabasi hayo yalikuwa na nembo ya UDART badala ya DART, kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba na kuiagiza DART kuendesha UDA-RT kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa kwenye mkataba.
Aidha, ripoti hiyo imepigilia msumari kwenye suala la watumishi hewa na kusema tatizo hilo limekuwa sugu na serikali za mitaa zinaongoza kwa kulipa mishahara watumishi waliofariki na waliotoroka huku Sh bilioni 2.7 zikiwa zimetumika mwaka wa fedha 2014/15 kwa malipo hayo.
Jambo lingine ambalo limejitokeza kwenye ripoti ya CAG, ni utoaji wa misamaha ya kodi kwa kiwango cha juu huku ikionesha Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa, zilisamehewa katika kipindi kilichoishia Juni 30, 2015.
Madudu halmashauri
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa baada ya ripoti kuwasilishwa bungeni, CAG Mussa Assad alisema wamebaini kasoro nyingi katika taasisi mbalimbali za serikali, huku udhaifu mkubwa ukiwa kwenye serikali za mitaa.
Alisema kwa mwaka unaoishia Juni 30 ,2015, jumla ya hati za ukaguzi 465 zilitolewa kwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na mashirika ya umma. Ripoti imeonesha kuwa mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri kwa kupata hati nyingi safi, huku zile za mashaka zikiwa chache.
Aidha hakuna hati mbaya wala isiyoridhisha. Akifafanua alisema katika ukaguzi huo, halmashauri ndizo zinaongoza kwa kufanya vibaya . Kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia ni zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu.
“Mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri hakuna wenye hati isiyoridhisha au hati chafu, ila halmashauri bado kuna udhaifu mkubwa kutokana na kutokuwepo na mifumo madhubuti ya kutekeleza mapendekezo ya ukaguzi tunayoyatoa,” alisema Profesa Asaad.
Ripoti hiyo imeweka hadharani udhaifu wa Serikali za Mitaa katika kutekeleza mapendekezo ya CAG kutokana na kubainika kuwa asilimia 63 ya maagizo ya mkaguzi huyo kwa halmashauri nchini hayajatekelezwa.
Misamaha ya kodi
Wakati huo huo, akizungumzia misamaha ya kodi kwa kipindi kilichoishia Juni 30, 2015, Profesa Assad alisema ripoti yao inaonesha kuwa kiasi cha misamaha kilichotolewa ni Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa.
Kiwango hicho kwa mujibu wa Profesa Asaad, ni cha juu ikilinganishwa na lengo la serikali la kupunguza misamaha hiyo isizidi asilimia moja ya pato la taifa. Ripoti hiyo pia inabainisha uwepo wa bidhaa zilizohifadhiwa katika maghala kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi ambazo zilipewa misamaha ya kodi ya Sh bilioni 9.1 lakini hakuna ushahidi ulioonesha mauzo hayo kama kweli yalifanywa nje.
Katika misamaha hiyo, pia kuna utata kwenye mafuta yenye dhamana ya kodi ya Sh bilioni tano ambayo yalionekana kwenye mfumo wa forodha wa (TANCIS) kuwa yamesafirishwa nje kupitia nchini lakini hakuna ushahidi wa hilo.
“Sasa ukiangalia hayo na mengine utaona udhaifu mkubwa , tumeshauri serikali iweke mkazo usimamizi wa misamaha ya kodi na itolewe tu kwa mambo yanayostahili na uwepo ufuatiliaji kujua mrejesho wake, ili serikali ikusanye kodi na kujiimarisha kiuchumi”, alisema Profesa Asaad.
Deni la Taifa
Akizungumzia deni la taifa, Profesa Asaad alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka 2015, deni la taifa lilikuwa Sh trilioni 33.54. Deni la ndani lilikuwa Sh trilioni 7.99 na deni la nje likiwa Sh trilioni 25.5 hivyo jumla ya deni lote likiongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na deni lililoishia Juni 30, mwaka 2014.
CAG ameshauri serikali kuongeza jitihada za ndani za kuhamasisha ukusanyaji wa mapato kujenga wigo mpana wa kulipa madeni na kuwa na mpango wa kupunguza gharama za kuongeza mikopo yenye masharti nafuu.

Zito kabwe anena tena


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John Magufuli kukabiliana na vikundi vya mafisadi vinavyoiba mabilioni ya fedha za umma kupitia mikataba mibovu waliyoingia badala ya kuishia kutumbua majipu. 
 
Akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama chake jana, Zitto alisema ACT Wazalendo inaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, lakini bado hajagusa kiini chenyewe. 
 
Zitto alitolea mfano wa kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow kuwa bado kuna kampuni inayolipwa Sh8 bilioni kila mwezi kwa ajili ya mitambo yake ya umeme. 
 
Pia, alisema kashfa ya hati fungani imeongeza deni la Taifa kwa Sh1.2 trilioni. 
 
“Bado huo mtambo upo chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa Sh8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. Hivi ndivyo vikundi masilahi katika sekta ya nishati. Bila kuvibomoa, Rais ataonekana anachagua watu katika vita hii,” alisema Zitto. 
 
Alisema: “Ni kweli kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya Dola 6 milioni za Marekani zinazohusu hati fungani. 
 
"Serikali imewafikisha mahakamani madalali wa rushwa lakini waliotoa rushwa hiyo hawapo mahakamani. Waliopokea rushwa ambao ni maofisa wa Wizara ya Fedha hawajashtakiwa.” 

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema vita ya ufisadi siyo ya kutumbua majipu tu, bali kujenga mfumo madhubuti wa kuzuia mianya ya rushwa. 
 
Alisema Rais Magufuli anapaswa kuwaongoza Watanzania katika vita ya kukataa mikopo kama hiyo ambayo inawasababishia umaskini. 
 
Aungana na hoja za upinzani 
Zitto alisema chama chake kinaungana na vyama vingine vya upinzani kwa hoja walizozitoa baada ya kutoka bungeni za kutokuonyeshwa moja kwa moja kwa matangazo ya televisheni kutoka bungeni, matumizi ya Serikali nje ya mpango wa bajeti na Serikali kutokuwa na mwongozo kwa mawaziri wake. 
 
Akizungumzia kusitishwa kwa urushaji wa matangazo ya Bunge, Zitto alisema hatua hiyo inatakiwa kupigwa vita kwa sababu inajenga udikteta katika nchi na kuwanyima wananchi haki ya kupata habari za Bunge. 
 
“Ina maana TV zinapaswa kumuonyesha mtu mmoja tu akihutubia bungeni ambaye ni Rais tu... hapana hii siyo sawa,” alisema Zitto.

Akizungumzia suala la bajeti, Zitto alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka Rais kuhamisha fedha kwenda kufanya shughuli nyingine. Lakini alisema tangu Rais Magufuli achaguliwe, amekuwa akihamisha fedha wakati Bunge lilishapitisha bajeti. 
 
“Rais Magufuli kwani amekuwa waziri wa fedha, waziri wa ujenzi na Rais kwa wakati mmoja? Tunamtaka asiingilie majukumu ya mihimili mingine, wananchi tumnyooshee kidole na kumwambia afuate utaratibu,” alisema Zitto. 
 
Mbunge huyo pekee wa chama hicho, alisema tangu walipoapishwa, mawaziri hawajapewa mwongozo wa kazi na kutoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa miongozo kwa mawaziri. 
 
“Mpaka sasa nchi haina mawaziri kwa sababu hawajapewa miongozo. Kwa hiyo, Baraza la Mawaziri lina mawaziri wawili tu ambao ni Rais na makamu wake,” alisema Zitto na kulitaka Bunge kutengeneza mfumo wa kuisukuma Serikali kutekeleza mambo muhimu kwa Taifa. 
 
Kuhusu hali ya uchumi, Zitto alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka mpaka kufikia Sh29 trilioni lakini ana wasiwasi itakwama kwa sababu theluthi moja ya mapato ya ndani yanatoka bandarini ambako ripoti zinaonyesha kuwa yamepungua. 
 
Alisema Serikali imepanga kukopa Sh7 trilioni kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti na kwamba hatua hiyo inazidi kuongeza deni la Taifa ambalo limelalamikiwa pia na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake. 
 
Mwenyekiti wa ACT, Anna Mghwira aliwataka wajumbe wa chama hicho kusimama pamoja ili kukijenga chama hicho na kukifanya kiwe mbadala kwa Watanzania akisema kimewavutia watu wengi ambao wanachukizwa na ufisadi

Rais Magufuli Amteua Thobias Andengenye Kuwa Kamishna Mkuu Wa Jeshi La Zimamoto Nchini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDxBp6II6x5wdTuzCTfdVyDVwa8-B2t0SwccmyYQeNg8ukUDAQQahZ87XVIDHxDE4Xq5bzO9S2Gj8xf8bjhXa3D4Sfwqe43tnvTsaqIQmrRkPxlt9-IZfnjtJ02l1rtUF-kv5YVN6R8Oc/s1600/mag2.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.

Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Uteuzi wa Dkt. Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-25 Aprili, 2016

Siwema wa Nay wa Mitego Afungwa Miaka Miwili Gerezani kwa Kutishia Kusambaza Picha za Uchi za Mpenzi Wake



Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili  jijini  Mwanza.
 
Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kueleza ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili  ila taarifa za awali  zilidai kwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.

Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv  na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.

Amesema kilichompeleka Siwema jela ni kumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.

Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.

Magazeti ya Leo jumanne ya tarehe 26/04/2016



Headline za magazeti haya ya Leo zinaletwa kwenu Kwa hisani kubwa ya NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE wanaotoa huduma ya tuition kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita ENEO ni majengo ya kanisa catholic  Madizini ilula iringa Tanzania 
Kwa mawasiliano zaidi ni +255784428256


























Jumatatu, 25 Aprili 2016

Breaking News :Rais Magufuli Ateua Makatibu Tawala wa Mikoa 26


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.

Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

    1.Arusha -    Richard Kwitega
    2.Geita -      Selestine Muhochi Gesimba
    3.Kagera -     Armatus C. Msole
    4.Kilimanjaro -     Eng. Aisha Amour
    5.Pwani -      Zuberi Mhina Samataba
    6.Shinyanga -   Albert Gabriel Msovela
    7.Singida -     Dr. Angelina Mageni Lutambi
    8.Simiyu -    Jumanne Abdallah Sagini
    9.Tabora -   Dkt. Thea Medard Ntara
   10.Tanga -    Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;

1.Kigoma -   Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
2.Morogoro -  Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)

Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;

    1.Dar es salaam -  Theresia Louis Mbando
    2.Dodoma -     Rehema Hussein Madenge
    3. Iringa -   Wamoja Ayubu Dickolagwa
    4.Katavi -    CP Paul Chagonja
    5.Lindi -   Ramadhan Habibu Kaswa
    6.Mara -   Benedict Richard Ole Kuyan
    7.Manyara -     Eliakimu Chacha Maswi
    8.Mbeya-    Mariam Amri Mjunguja
    9.Mtwara -    Alfred Cosmas Luanda
   10.Mwanza -  CP. Clodwing Mathew Mtweve
   11.Njombe -   Jackson Lesika Saitabau
   12.Rukwa -   Symthies Emmanuel Pangisa
   13.Ruvuma -   Hassan Mpali Bendeyeko

Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Aprili, 2016