Jumapili, 1 Mei 2016
Jumamosi, 30 Aprili 2016
Ijumaa, 29 Aprili 2016
Rufaa kupinga kuachiwa Zombe na wenzake kusikilizwa leo
Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Bernard Luanda, wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage. Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), alikata rufaa mwaka 2013, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake, baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa inawakabili.
Katika rufaa hiyo, DPP anadai kuwa Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia huru washitakiwa hao kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wote. Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Gwabisabi.
Katika kesi ya msingi inadaiwa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam Zombe na wenzake waliwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Morogoro, Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, pamoja na dereva teksi Juma Ndugu.
Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Agosti 17, 2009, Jaji Massati aliwaachia huru washitakiwa kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao bila kuacha shaka na Mahakama ikiwaona hawana hatia kwa makosa yaliyokuwa yanawakabili.
Kilombero watafakari ongezeko la maji
Mkakati huo unatokana na kuendelea kunyesha kwa mvua za masika hali itakayosababisha mto Kilombero kujaa maji na kukifanya kivuko hicho kusitishwa kuendelea kufanya kazi zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya kikao cha Afya ya Msingi Mkoa kilichofanyika mjini Morogoro.
“Hadi leo (jana) maji katika mto Kilombero yamefikia ujazo wa mita 60 kutoka usawa wa bahari na ili Kivuko cha Mv Kilombero kisimame kufanya kazi ni pale ujazo wa maji utakapofikia mita 90 kutoka usawa wa bahari,” alisema Gembe na kuongeza: “Kwa sasa bado kiwango cha ujazo wa maji mto Kilombero ni mita 60 kutoka usawa wa bahari na kufanya Kivuko cha Mv Kilombero II kiendelee utoaji wa huduma na tunaomba mvua hizi zisizidi kupita kiwango hicho.”
Alisema Kivuko cha Mv Kilombero II bado kinaendelea kufanya kazi za uvushaji wa abiria, mizigo na magari kulingana na taratibu zilizowekwa.
Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi Mkuu TIC
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Dk Magufuli ametengua uteuzi huo rasmi kuanzia Aprili 24, mwaka huu. Profesa Mkenda alisema pamoja na mambo mengine, hatua hiyo imechukuliwa na Dk Magufuli baada ya kupata taarifa kuwa mkurugenzi huyo alikuwa hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa, jambo lililozua maswali.
Aidha, kwa mujibu wa Profesa Mkenda, endapo Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Tano, atapangiwa kazi nyingine. Alisema kutokana na hatua hiyo, tayari mchakato wa kumpata Mkurugenzi mpya umeanza mara moja.
Spika apangua tena Kamati za Bunge
Spika Ndugai alisema Ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imelipa uhalali Bunge kuunda Kamati za Bunge za namna mbalimbali kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
Alisema pia kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni ya 116 (3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili 2016, amelazimika kufanya mabadiliko ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge.
Spika alisema sababu kubwa iliyomfanya kufanya mabadiliko hayo ni kuhakikisha kuwa kila mbunge ikiwa ni pamoja na wabunge wanne wapya walioapishwa Aprili 19, anakuwa mjumbe kwenye kamati mojawapo ya Bunge.
CAG: Walimu ‘vihiyo’ waongezeka nchini
Katika ripoti hiyo iliyofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutolewa mapema wiki hii mjini Dodoma, inaonesha kuwa idadi ya walimu hao imeongezeka kutoka walimu 963 mwaka 2014 hadi kufika waalimu 2,108 mwaka jana. Ilieleza kuwa sababu kubwa ya kuwa na walimu wasio na sifa zaidi ya moja imetokana na Ofisi ya Waziri Mkuu (wakati huo), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kushindwa kuwa na mpango wa kuwaendeleza walimu waliowaajiri.
Ripoti maalumu hiyo ya ubora wa elimu nchini imebaini kuwa matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona idadi ya walimu wasio na sifa ikipungua kutokana na wengi wao kustaafu na wengine wapya kuajiriwa ambao wana sifa, lakini cha ajabu idadi hiyo imeongezeka.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)