Ijumaa, 13 Mei 2016
Alhamisi, 12 Mei 2016
Kitaa kunanini:Tapeli aibuka chuo kikuu cha Dar Es salaam(DUCE)
Na stanley kilangi
Picha Grace tapeli)
Katika hali isiyokuwa ya kawaida ilitokea katika chuo kikuu kishiriki cha DUCE baada ya Dada mmoja aliejulikana Kwa jina la kitapeli la Grace ambapo alijikuta akiwa katika ulinzi mkali wa polisi na walinzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam baada ya kukutwa akiwa ndani ya chuo akijihusisha na kuomba na kurubuni wanafunzi waliopo chuoni hapo
Akiongea na waziri wa ulinzi wa DARUSO- DUCE askari wa chuo hicho alidai Dada huyo amekuwa akipita getini hapo kila siku akidai anapita kuelekea nje ya geti la chuo hicho
Dada huyo alikuwa akiomba Pesa hizo Kwa wanafunzi akidai anakaa mbagala na hana uwezo wa kupata mahiji ko angehitaji msaada huo lakini Mara baada ya kufanyiwa mahojiano ya kina ilibainika kuwa dada huyo hakuwa na maisha magumu na alikuwa anaishi na mama yake katika maisha ya kawaida lakini aliamua kuwa ombaomba kutokana na faida kubwa ya kuombaomba katika vyuo vya Dar Es Salaam kikiwepo TIA na DUCE
Dada huyo aliomba msamaha na kukiri kutoridia tena. Tukio hili limetokea tarehe 02/05/2016 Ama kweli mjini shule kijijini tusheni

Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais
Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika
video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana
''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa
mahakama ya juu''.
Video hiyo ilisambazwa kwa kasi
kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia
mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu
nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika
uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza
Besigye na Amama Mbabazi.
Kadhalika,
Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya
kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na
Amama Mbabazi.
Tanzia: Msanii wa Vichekesho Mohammed Abdallah (Kinyambe) Amefariki Dunia
Mchekeshaji
maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed
Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia Jumatano hii baada ya kusumbuliwa
kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.
Taarifa
za kifo chake zilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii baada
ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku wakiandika RIP
Kinyambe.
Mmoja
kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania,
Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.
“Kinyambe
alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu Pia watu wake wa karibu akiwemo Mke wake wanadai imetokana na kujaa Kwa maji kwenye mapafu, ila jana ndo
amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.
Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.
“Kusema
kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana
na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikikamilika tutaweka
wazi,” alisema Mkono.
Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho..
Mungu amlaze mahali mahali pema peponi -Amina
Msanii Maalufu wa tasinia ya uigizaji wa comedy amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo .Sababu ya kifo chake ikiwa bado haijajulikana ila kifo hicho kimetokea katika hospital ya mkoa wa mbeya .mungu amlaze mahali pema peponi kinyambe.
Mwili umechukuliwa na mazishi yake yanatarajia kufanyika Uyole mbeya
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)