ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 17 Mei 2016

MAGAZETINI:#Mabasi Dart ‘yawatema’ askari

Imeandikwa na Anastazia Anyimike HUDUMA ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka imeanza rasmi jana jijini Dar es Salaam huku yakilalamikiwa na watumiaji wakiwemo baadhi ya watu waliokuwa na msamaha wa kusafiri bila kutoa nauli, ambao sasa hawatambuliwi na mfumo mpya.
Utaratibu uliokuwa umezoeleka awali wa askari wa polisi, jeshi, magereza na walimu kutolipa nauli kwenye usafiri wa daladala, umeonekana kugonga mwamba chini ya mabasi hayo. HabariLeo ilishuhudia mwalimu ambaye alikataa kutaja jina lake akitaka mwongozo wa kutolipa nauli kwa kuwa yeye ni mwalimu.
“ Mama mfumo huu haumtambui mwalimu, askari,” alimjibu mmoja wa wahudumu wa UDA-RT aliyekuwa akihakiki tiketi za abiria kabla ya kupanda basi.
Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa alisema mwongozo uliotolewa na Sumatra, unamtambua mwanafunzi pekee ambaye anatakiwa kulipa Sh 200, wengine wote wanatakiwa kulipa nauli.
Mbali na walimu, askari, pia watu wenye ulemavu ambao walikuwa hawalipi nauli kwenye daladala, kwenye mfumo wa mabasi yaendayo haraka wanatakiwa kulipa.
Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni mfumo wa ukataji tiketi, ambao unadaiwa kusababisha foleni ndefu huku wahudumu wakiwa hawana chenji, jambo lililosababisha baadhi ya watu kulipa kiasi kikubwa cha fedha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria walisema walilazimika kukaa zaidi ya daika 20 vituoni kutokana kusubiri chenji na wengine kuamua kuacha fedha zao.
“Nimetoa Sh 1,000, nimepewa tiketi na kurudishiwa Sh 200 na kuwa hana Sh 150. Hapa inaonesha nimesafiri kwa Sh 800. Nauli hii ningeitumia kupanda daladala na kuzunguka nalo ili nipate kiti, ningepandia upande wa pili ningetumia Sh 500,” alisema Kasum Swakala, mkazi wa Ubungo Bonyokwa. “Nina haraka na siwezi kuipata hiyo 150 ambayo hawajanipa katika chenji yangu, inabidi tu kuondoka ili kuwapisha wengine lakini hali hii inatuumiza sana na siyo sawa kwa sababu kesho siwezi kurudi kuwadai chenji yangu,” alisema.
“Nimetoka Mbezi na kulipa 400, nimefika hapa wanasema hawana cheji kama nataka nilipe 800, siwezi kulipa kiasi hicho naenda kupanda daladala.”
Dada mmoja ambaye awali alimuuliza mwandishi eneo la kukatia tiketi baada kushuka na basi la Mbezi. Meneja Uhusiano wa UDA-RT, Deus Bugaywa alikiri kuwapo changamoto ya chenji na kusema asubuhi walikuwa na chenji nyingi ambazo ziliisha haraka hivyo kuleta usumbufu kwa baadhi ya abiria.
Mkazi wa Mbezi, Laurence Msuya alilalamikia hatua ya kukata tiketi mara mbili na kusema imesababisha usumbufu kwao kwa kupoteza muda. Wakala wa kukatisha tiketi katika kituo cha Mbezi alilalamikiwa kuchelewa kufika kwa jambo lililozidisha msongamano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UDA-RT, David Mgwasa alisema hali hiyo itaondoka pale mfumo wa kadi utakapoanza kufanya kazi.
“ Wananchi tuliwafundisha namna ya kutumia kadi, na siku moja kabla Serikali ikazuia matumizi yake, sasa tunasubiri maamuzi ili tuanze kuuza. Tulijua wananchi wangekuwa na kadi na wale wachache ambao ni wanafunzi na wale wanatumia mara moja moja ndio wangetumia tiketi za karatasi,” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), John Shauri alisema mfumo wa tiketi za kadi uko katika hatua za mwisho na mazungumzo. “ Ilikuwa ni lazima tuanze tiketi za karatasi, kwani tutakuwa na mifumo miwili inayofanya kazi hii ya tiketi za karatasi na kadi, mambo yakiwekwa sawa kadi zitaanza kutumika,” alisema.
Changamoto nyingine katika huduma hiyo iliyofanywa na baadhi ya wakala wa kukatisha tiketi kuzongwa au kutakiwa kutoa ufafanuzi ni pamoja na abiria kupewa tiketi za wanafunzi wakati wamelipa nauli ya watu wazima. Baadhi ya abiria walijikuta wakikata tiketi nyingine kutokana na za awali kuisha muda wake.
Hali hiyo ilitokana na wakazi hao kukata tiketi na kwenda kwenye shughuli zao nyingine na walipofika kituoni na kukuta muda wake umeisha walilazimika kukata nyingine.
“Awali walisema hizi tiketi unaweza kupandia basi wakati wowote lakini nashangaa leo nimekata tiketi nikaamua kwenda kwenye shughuli nyingine. Nimerudi hapa wakati tiketi inakaguliwa ikagoma kusoma kwa madai kuwa muda wake wa matumizi umeisha,” alisema mmoja wa wakazi wa Kimara Mwisho.
Akijibu hoja hiyo, Mgwasa alisema tiketi za karatasi zinatakiwa kutumika kwa safari moja na kuwa zinadumu kwa saa mbili kabla ya kuisha muda wa matumizi na ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kukata tiketi pale tu wanapotaka kusafiri.
Tiketi zilizokuwa zikitolewa na mawakala wanaohusika zilikuwa hazina maelezo ya nauli waliyolipa abiria zaidi ya kuonesha tarehe, muda uliokata, kituo ulichokatia jambo ambalo liliwafanya abiria kuhoji na kuona ni ujanja wa kupoteza mapato ya serikali.

MAGAZETINI:#Upinzani wakataa kusoma maoni yao bungeni

 KAMBI Rasmi ya Upinzani bungeni imekataa kusoma maoni yake kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya kutakiwa kuondoa maneno yanayokiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.
Ilikataa kufanya hivyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu kuagiza Kamati ya Kanuni za Bunge pamoja na kiongozi wa kambi hiyo ya upinzani ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema, kukutana na kurekebisha maoni yao kabla ya kuyawasilisha bungeni.
Aliagiza hivyo jana kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara na Waziri Charles Kitwanga, baada ya kueleza kuwa alipopitia maoni ya kambi ya upinzani aligundua kuwa yalikiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.

MAGAZETINI:#11 mbaroni kwa kurekodi video ya kujamiiana, kuisambaza mtandaoni

WATU 11 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 21, kisha kumpiga picha za utupu za video na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuonesha tendo hilo la ubakaji.
Kati ya hao, wawili wanashikiliwa kwa kubaka na kumpiga picha msichana huyo, wakati tisa wanatuhumiwa kusambaza picha hizo za utupu kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema jana mjini hapa, kuwa watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho Aprili 28, mwaka huu, saa 1 usiku katika nyumba ya kulala wageni yenye jina la Titii iliyopo Kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero.
Wakati kamanda akitoa taarifa hiyo, vile vile Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pia alitoa kauli ya serikali bungeni mjini Dodoma, kulaani kitendo hicho na akawataka watu wote wenye video hiyo kuacha kuisambaza kwa kuwa ni udhalilishaji kwa wanawake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Matei alisema msichana huyo (jina limehifadhiwa), aliitwa kwenye nyumba hiyo ya wageni na mwanamume aliyefahamika kwa jina la Zuberi Thabiti (30) mkazi wa Mbarali, mkoani Mbeya; ambaye alikuwa na mahusiano naye kimapenzi.
Alisema baada ya kuingia chumbani, alimkuta mwanamume mwingine aliyefahamika kwa jina la Iddy Adamu (32), mkazi wa Makambako.
Kamanda alisema mwanamume huyo, alimlazimisha msichana kufanya mapenzi huku akimrekodi picha za video na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Kwa mujibu wa kamanda, watuhumiwa hao pia walimtishia kisu msichana huyo asipige kelele wakati akifanyiwa kitendo hicho na kumtaka asitoe siri hiyo vinginevyo watamuua.
Kamanda Matei alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea wakati polisi ikiendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine waliosambaza picha hizo za video wafikishwe mahakamani.
Aliendelea kuonya wananchi kwa kuwataka kuepuka kusambaza picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii, vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Serikali yalaani Awali, Waziri Ummy alilaani kitendo hicho kwa kutaka hatua stahili zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.
Alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Kemilembe Lwota (CCM) kuomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu kuhusu video hiyo inayosambazwa.
Mbunge huyo wa viti maalumu alisema ipo video inasambazwa katika mitandao ya kijamii, inayomdhalilisha msichana wa kitanzania akifanyiwa vitendo hivyo, ambavyo vinakiuka mila na desturi za Mtanzania.
Ummy alisema, akiwa waziri anayesimamia masuala ya wanawake na watoto pamoja na serikali, wanalaani kitendo hicho kilichofanywa cha kumdhalilisha mwanamke.
Alisema baada ya kuiona na kuwasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, watuhumiwa hao wamekamatwa.
Alisema ana imani watafikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo. Aliwataka wanaume kuheshimu wanawake wote huku akisisitiza kuwa suala hilo halivumiliwi.

MAGAZETINI:#Serikali yamwaga ajira nchini


Imeandikwa na Mgaya Kingoba, Dodoma
SERIKALI inatarajia kumwaga ajira kwa askari na walimu katika mwaka ujao wa fedha huku ikisisitiza walimu kwamba watakaokaidi kwenda kuripoti kwenye mikoa ya pembezoni na baadaye kuamua kuomba tena, hawatapewa nafasi kama ambavyo imekuwa ikifanya.
Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni kwa nyakati tofauti na mawaziri tofauti wenye dhamana na taaluma husika.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17.
Kwa upande wa ajira kwa walimu 35,411 wa shule za msingi na sekondari, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha maswali na majibu.
Ajira polisi Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991.
Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira.
“Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga.
Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini katika kusimamia nidhamu kwa askari wake kwa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) kwa kuchukua vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanaoomba kujiunga na Jeshi la Polisi ili kuwa na askari wenye nidhamu na moyo wa dhati wa kulitumikia Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema linatarajia kutoa mafunzo kwa maofisa na askari 4,975 katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Taaluma ya Urekebishaji.
Alisema ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa miundombinu ya makazi kwa askari Polisi, serikali kupitia mkopo kutoka Serikali ya China inakusudia kujenga nyumba 4,136 chini ya usimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi.
Akizungumzia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema jeshi hilo linahitaji vituo 152 Tanzania Bara, lakini kwa sasa lina vituo 57 na kati ya hivyo, 38 vipo katika miji na 19 katika viwanja vya ndege. Alisema huo ni upungufu wa vituo 95 hali inayosababisha maeneo mengi kukosa huduma za zimamoto na uokoaji.
Inategemea kujenga kituo kimoja cha zimamoto na uokoaji katika eneo la Kigamboni katika Jiji la Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Tazara - Mchicha, Dar es Salaam.
Aidha, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na makosa yanayovuka mipaka hususani ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, wizi wa vyombo vya moto hususani magari, wizi wa kutumia mitandao ya Tehama, bidhaa bandia, na biashara haramu ya silaha na uchafuzi wa mazingira.
Walimu kuajiriwa Kuhusu walimu 35,411 watakaoajiriwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jaffo alisema uamuzi wa kuwaajiri umetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa mji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.
Jaffo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni na Lindi na kwingineko, lakini wakakataa kuripoti.
Alikiri kuwa walimu wengi hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni na si Lindi pekee, bali mingine ikiwemo Katavi, Kigoma. Hata hivyo alisema, pamoja na kwamba mwaka huu wanaajiri walimu 35,411 , ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini pekee, hawataajiriwa tena serikalini kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa kuomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.
Awali, Katika swali ya msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, LucyMlowe (Chadema) alitaka kufahamu mpango wa serikali uliopo wa kukabiliana na changamoto za uchache wa walimu kwenye shule za msingi na sekondari.
Naibu waziri alisema, ili kuboresha elimu nchini kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani serikali imeendelea kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Magazeti ya Leo jumanne ya tarehe 17may 2016



























Jumatatu, 16 Mei 2016

MAGAZETINI:# Leo jumatatu ya tarehe 16 may 2016

Pamoja katika magazeti ya Leo chini ya usimamizi mzuri wa kikoti blog







 Tangaza nasi Kwa being poaa 0769694963





 Furahi nasi na kutangaza bidhaa au biashara Kwa being rahisi kabisa




Jumapili, 15 Mei 2016

MATUKIO KATIKA PICHA


KUKABIDHIWA MSAADA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akikabidhiwa msaada wa moja ya cherehani 73 Dar es Salaam jana na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Alinajem (wa pili kulia). Kushoto ni Mbunge wa Ukonga, Bonnah Kaluwa, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mivinjeni Kata ya Buguruni, Barua Mwakilanga ambao wamepewa cherehani hizo zilizoombwa na mwenyekiti huyo. Kulia ni Meneja wa African Relief Organization Tanzania, Sammy Mohamed. (Picha na Yusuf Badi).

MJADALA - KUFUATILIA.

Wabunge wa CCM wakifuatilia mjadala bungeni mjini Dodoma jana. (Picha na Fadhili Akida).

KUZUNGUMZA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki (kulia) akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Mgonukulima kweye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. (Picha na Fadhili Akida).