ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 11 Juni 2016

Habari zilizopo katika magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 11/06/2016





NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.  



















Ijumaa, 10 Juni 2016

Kilio Kwa watumia M-pesa, Tigo Pesa , Airtel Money na Wale wa Kwenye ATM.......Kila ukituma 1000/- utakatwa kodi 280/-

 Image result for MPANGO
Wachambuzi na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wakikumbwa na maumivu wa kodi.

Hiyo ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17.

Pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara.

Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa   kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma.

Jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.

Alisema katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika kila Sh  1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA.

Zitto alisema hali hiyo pia itawakumba watumiaji wa miamala ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania wanaotumia huduma hiyo nchini.

Aawali kodi ya bidhaa ilikuwa asilimia 10 lakini kwa hatua ya kuongezwa kwa kodi ya ongezeko la thamani kodi itapaa na kufikia asilimia 28.

Kwa mantiki hiyo, katika kila Sh 100 kodi ni Sh 28 na  katika Sh 1000 kodi ni Sh 280.

Kutokana na hali hiyo kodi ya VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambaye anatuma au kupokea fedha, hali ambayo itawaumiza watumiaji wa mwisho.

“Hivyo hivyo katika miamala ya M-pesa, Tigo pesa na kadhalika, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai 1, 2016, Sh  280 zitachukuliwa na TRA,” alisema Zitto.

Alisema   ameshangazwa na hatua ya Serikali kuongeza kodi ya VAT kwenye utalii hali ambayo inaweza kusababisha Tanzania kupoteza watalii wengi kwa washindani wake kwa sababu itaongeza gharama kwa watalii.

“Kama tunataka kutumia utalii kama kichocheo cha ajira ni vema kufikiria upya suala hili,” alisema.

Akizungumzia mapendekezo ya Serikali katika Sheria ya Kodi ya VAT ili kutoza kodi bidhaa zinazotoka Zanzibar, alisema hatua hiyo inavunja misingi iliyowekwa na sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile za Zanzibar.

“Ikumbukwe kuwa Sheria ya Kodi ya VAT ya 2014 ilivunja misingi iliyowekwa ya sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile ya Zanzibar. Mapendekezo ya sasa yana madhara makubwa kwa Zanzibar kwa sababu  hakuna atayewekeza Zanzibar ili kufaidika na soko la Bara.

“Biashara nyingi zinazozalisha Zanzibar zitahamia Tanzania Bara. Mapendekezo haya yanaweza kusababisha  mgogoro kati ya pande mbili za Muungano,” alisema.

Hotuba Ya Msemaji Mkuu Wa Kambi Rasmi Ya Upinzani Bungeni Katika Wizara Ya Fedha Na Mipango 2016/2017

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016

1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Mwanafalsafa Baron Montesquieu aliwahi kuandika ifuatavyo kuhusu mgawanyo wa madaraka “Pale ambapo madaraka ya Bunge na ya Serikali kuu yanakuwa yamehodhiwa na mtu mmoja, au katika chombo hicho hicho cha hukumu, hakutakuwa na uhuru, kwa sababu hofu itazuka, utawala huo huo au bunge litatunga sheria kandamizi na kuzitekeleza kwa mfumo kandamizi. Pia hakutakuwa na uhuru endapo madaraka ya Mahakama, Bunge na Serikali hayatatenganishwa.

Pale ambapo madaraka ya Serikali kuu yanapokuwa yamefungamanishwa na Bunge, uhai wa Bunge na Uhuru wake unakuwa katika hatari kubwa ya kudhibitiwa kiholela: kwa kuwa Jaji hawezi kuwa mtunga sheria. Pale ambapo Serikali kuu imefungamanishwa na mahakama, basi Jaji anaweza kuwa na tabia ya mabavu na ukandamizaji. Inakuwa mbaya zaidi, pale ambapo mtu huyo huyo au chombo hicho hicho, iwe ni wateule wa Serikali au watu wengine wanapotumia hayo madaraka ya kutunga sheria, kutekeleza maazimio ya umma na kutoa hukumu za jinai au tofauti za watu”

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa mada iliyowasilishwa na Profesa P.J. Kabudi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juu ya “Mafundisho ya Mgawanyo wa Madaraka na jinsi yanavyotumiwa Tanzania” (Doctrine of Separation of Powers and its Application in Tanzania: Success, Challenges and Prospects) ni kwamba; hakuna mgawanyo dhahiri wa madaraka baina ya mihilimili mikuu ya dola na kwamba bado Tanzania ina ‘hang-over’ ya ulevi wa siasa za chama kimoja . Sehemu ya Mada hiyo inasomeka hivi: nanukuu; “Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 bado inatumika mpaka leo pamoja na kuwa marekebisho yalikuwa mfano wa Ustawishaji wa mfumo wa chama kimoja nchini Tanzania. Katiba pia iliendelea kustawisha dhana ya Ukuu wa Chama kushika hatamu. Ibara ya 3 na 10 zilibainisha kuwa CCM ndio chama pekee cha Siasa Tanzania na kuwa shughuli zote za Serikali ilibidi zifuate sera na miongozo ya chama. Hii ilimaanisha kuwa Bunge na Mahakama vilitakiwa kufuata maelekezo ya chama katika kutenda majukumu yao. Zaidi ya yote, kama ilivyokuwa kwa Katiba ya Mpito, ibara ya 63(4) ya Katiba ililifanya Bunge kuwa kamati maalumu ya Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa. 
Ilikuwa ni jambo la kawaida pale ambapo bajeti ya wizara imekwama basi wabunge waliahirisha mkutano na Bunge lilikaa kama kamati ya Chama ili kujadili hilo suala. Mara tu uamuzi unapofikiwa basi Bunge linarejea na bajeti inapitishwa bila kuwa na upinzani mkubwa”

Rais Magufuli Amuapisha Jaji Wa Mahakama Ya Rufani Pamoja Na Jaji Kiongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Juni, 2016 amemuapisha Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila alikuwa Jaji Kiongozi.

Wakati huohuo, Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi, Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.

Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Leons Katipwa Wambali amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila ambaye amekua Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

Akizungumza na Balozi huyo, Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameishukuru Oman kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania, na ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano ipo tayari kuongeza ushirikiano huo.

Mhe. Rais Magufuli pia amemuomba Balozi Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi kufikisha salamu zake kwa Sultani wa Oman Mtukufu Qaboos bin Said al Said na kumueleza kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Oman na inatarajia kuona miradi ya ushirikiano katika uwekezaji ukiwemo mradi wa Bagamoyo inaanza kutekelezwa haraka.

"Naomba umfikishie salamu zangu za dhati Mtukufu Qaboos bin Said al Said, Sultan wa Oman na umwambie tunamkaribisha Tanzania na nitafurahi kuona mradi wa uwekezaji wa Bagamoyo unakuwa kielezo cha undugu na urafiki wetu uliodumu kwa miaka mingi" Amesema Rais Magufuli.

Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Oman na China zimekubaliana kutekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
10 Juni, 2016
.

Nida Yaanza kutoa Vitambulisho vyenye Saini

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwenye kitambulisho kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akifafanua Mdami alisema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa ambapo katika hatua ya kwanza mamlaka hiyo inachakata taarifa za wananchi walizotoa wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Utoaji wa vitambulisho hivi vyenye saini ya mwombaji utasaidia kuwatambua wahusika pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii.

“Upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la Watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma” alisisitiza Mdami.

Utoaji huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za utambulisho kwa wananchi ili zisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati mchakato wa kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.

Mdami alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili ya uhakiki wa taarifa hizo.

Wasichana 500 kurejeshwa nchini

Imeandikwa na Hellen Mlacky
SERIKALI itawarudisha nchini Watanzania 500, waliokwama India baada ya kampuni zilizowachukua kwenda kuwatafutia kazi, kukiuka mikataba yao na kuwalazimisha kufanya kazi tofauti ikiwemo ukahaba.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga aliyasema hayo jana Dar es Saalam wakati akizungumzia matatizo wanayoyapata Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi.
“Kati ya Machi hadi Mei 2016, balozi zetu nchini India na Malaysia zimepokea maombi ya kusaidia kuwarejesha nyumbani Watanzania ambao walipelekwa nchini India na Thailand kwa ahadi za kupatiwa ajira ambazo hutolewa na watu wasio waaminifu ambao wanashukiwa kujihusisha na mtandao wa biashara ya kusafirisha binadamu,” alisema Kasiga.
Alisema mtandao huo unawatafuta wasichana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 na hata chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika hoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani nchi za nje na kuwawezesha kupata hati za kusafiria na tiketi ya ndege kwa ajili ya kusafiri kwenda kwenye nchi husika.
“Wengi huvutika kirahisi kwa kuona hiyo ni fursa ya kujipatia kipato ila kwa taarifa tulizopata ni kwamba wengi hujua mapema kuhusu kazi wanayoenda kuifanya huko ila ugumu wa maisha unapelekea kurubuniwa na kuingia kwenye matatizo makubwa,” alifafanua msemaji huyo.
Alisema nchini India peke yake, kuna Watanzania takribani 500 wengi wao wakiwa New Delhi (350), Bangalore (45), Mumbai (20) na wengine wanaelekea Goa. Alisema kwa upande wa Mashariki ya Kati, kumekuwa na wimbi kubwa la wasichana kurubuniwa kwa kutafutiwa fursa za kwenda katika nchi za Oman, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu hasa Dubai kufanya kazi za ndani.
“Baadhi ya wahanga wamekuwa wakikimbilia kwenye ofisi zetu za ubalozi kuomba msaada na balozi zimekuwa zikiwahifadhi ubalozini na kisha kuwasiliana na jamaa zao ili wawatumie nauli na kurejea nyumbani,” alisema.
Alisema wizara imekuwa ikipokea maombi kutoka ofisi za ubalozi nchi za Asia na Mashariki ya Kati ili kuwasaidia wasichana hao kurejea nchini, na hivi karibuni kutoka Ubalozi wa Oman kulikuwa na wasichana 18 kati yao 10 wamesaidiwa kurudi na kuunganishwa na familia zao na Ubalozi wa India wasichana 15 wamepeleka maombi yao.
Aliyataja matatizo yanayowakabili Watanzania nchi za Mashariki ya Kati na Asia kuwa ni pamoja na kulazimishwa ukahaba na kunyang’anywa hati za kusafiria ili kuwadhibiti wasitoroke na wengine kujikuta kukubali kufanya ukahaba ili kurejesha gharama za kuwasafirisha pamoja na kupata nauli.
Matatizo mengine ni kufanya kazi bila mikataba, kufanya kazi nyingi ambazo zingetakia kufanywa na zaidi ya watu wawili au watatu, kufanya kazi kwenye familia zaidi ya moja tofauti na makubaliano, kufanya kazi bila muda maalumu wa kupumzika, kunyanyaswa na kubaguliwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kupigwa, kutopewa fursa ya kuwasiliana na mtu yeyote pamoja na kunyanyaswa kijinsia.
Alisema serikali imechukua hatua mbalimbali, ikiwemo kutafuta majina ya wahusika wote wa mtandao huo na kufanya mawasiliano na serikali za nchi hizo ili kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika mkono wa sheria.

Mzee Mwinyi akunwa mabasi ya haraka

Imeandikwa na Anastazia Anyimike
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi jana alitembelea Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka na kusema licha ya kuchelewa kwa mradi huo ana imani utasaidia kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kumaliza safari yake katika kituo cha Kivukoni jana akitokea kituo cha Morocco na kwenda kituo cha Gerezani, Kariakoo na baadaye Kivukoni, Mwinyi aliyekuwa amefuatana na mkewe, Mama Sitti, alisema mradi huo utasaidia kupunguza foleni katika jiji na kwamba umeanza kuwaondolea wananchi adha ya kugombea usafiri wakati waendapo na warudipo katika shughuli zao.
Alisema licha ya mabasi hayo kugawana abiria na daladala na bodaboda, ana imani siku zijazo na utaratibu ukiwekwa vyombo vingine vya usafiri visiingie mjini ili mabasi hayo yawe huru kufanya kazi, tija zaidi itaonekana.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Ronald Lwakatare alisema muda wowote ndani ya mwezi huu wananchi wataanza kutumia tiketi za kadi baada ya taratibu zote kukamilika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT, David Mgwasa alisema wananchi wameanza kuelewa juu ya matumizi ya mabasi na miundombinu yake, huku akisema tatizo linalowakabili kwa sasa ni mlundikano wa abiria wakati mmoja jambo ambalo linafanya usafiri huo kuelemewa nyakati fulani.