ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 11 Juni 2016

Mwigulu Nchemba ndio waziri mpya wa mambo ya ndani


Nafasi yake imechukuliwa na Dr Tizeba, Mwigulu amechukua nafasi hiyo baada ya aliekuwa waziri wa wizara hiyo kuondolewa na rais Kwa madai ya kuingia na kujibu maswali bungeni  akiwa amelewa, wateuliwa wote  wataapichwa na rais ikulu siku ya jumatatu.

Kuhusu ajira za walimu: TAMISEMI wanena

 
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.  

Mameya wampinga Dk Mpango Kuhusu ushuru wa majengo


Uamuzi wa Serikali kuziondolea halmashauri mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo, umeibua sintofahamu huku baadhi ya mameya wakidai ni agenda dhidi ya upinzani.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka 2016/17, Waziri za Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ili kodi hiyo iwe inakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema lengo ni kuifanya TRA kukadiria kodi ya majengo na kuyafanyia tathmini na kupewa uwezo wa kukusanya kodi hiyo kwa kutumia utaratibu wake wa kawaida.

Waziri aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa muswada huo utaweka utaratibu wa namna ya kuhifadhi na kuwasilisha kodi ya majengo, inayokusanywa na TRA kwa halmashauri husika.

Hata hivyo, utaratibu huo umepingwa na mameya wa halmashauri za manispaa na majiji nchini na kwa siku mbili kuanzia juzi walikutana jijini Arusha na walitarajia kutoka na azimio la pamoja kupinga suala hilo.

Habari kutoka katika mkutano huo zinadai kuwa huenda jana hiyo saa 7:00 mchana mameya hao bila kujali tofauti za itikadi za kisiasa, wangetoka na tamko la pamoja kupinga uamuzi huo mahakamani.

Hata hivyo, mameya wanaotoka katika halmashauri zinazoongozwa na madiwani kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameenda mbali na kudai kuwapo agenda mahsusi ya kuua upinzani.

Meya wa Halmashauri ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Shaban Jacob alisema Serikali haina historia ya kurejesha kodi inazokusanya kwa niaba ya halmashauri. 

“Serikali inaposema itarejesha si kweli. Kodi ya Ardhi imekusanywa na Serikali na sisi kama Halmashauri ya Kinondoni hatukuwahi kupewa kwa miaka 10,” alisema Jacob.

Meya huyo alitoa mfano wa kodi ya majengo iliyokusanywa na TRA hadi mwaka 2013 iliporejeshwa halmashauri, kwamba kipindi chote hicho halmashauri haikuwahi kupewa zaidi ya Sh1 bilioni.

Jacob alisema mwaka wa fedha wa 2016/17, halmashauri yake ilipanga kukusanya kodi ya majengo inayofikia Sh10 bilioni ambayo ndiyo kwa sehemu kubwa ingetekeleza miradi ya maendeleo.

 “TRA haina mfumo wala watendaji kufanikisha hili. Ili TRA iweze kukusanya Sh1 bilioni hapa Kinondoni itahitaji kuajiri vijana 5,000 kusambaza bili, jambo ambalo hawataliweza,”alisema.

Meya huyo alisema zipo hisia kuwa mpango huo unalenga kuzidhoofisha halmashauri za manispaa na majiji, ambazo ziko chini ya Ukawa ili zisiweze kutekeleza kikamilifu mipango ya maendeleo.

Vyama vilivyo chini ya Ukawa vimetwaa halmashauri za majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na manispaa ya Iringa.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat), ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Gulam Mkadam amesema Alat inapinga kuipa TRA mamlaka ya kukusanya kodi za majengo.

Alisema kitendo hicho kitadhoofisha uwezo wa mamlaka hizo kuwahudumia wananchi. Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya, alisema uamuzi huo unaathari mbaya, kwa vile halmashauri zilishapitisha bajeti zikitegemea fedha hizo.

“Property Tax (kodi ya majengo) ni chanzo kikuu cha mapato katika halmashauri nyingi za mijini. Leo unapokiondoa chanzo hicho, hiyo miradi itatekelezwaje? Kuna kitu kimejificha hapa,” alisema.  
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.   

Juma Abdul, Telela kuwakosa Waalgeria

Imeandikwa na Vicky Kimaro.
WACHEZAJI mahiri wa Yanga, Juma Abdul na Salum Telela, hawatakuwepo katika kikosi cha Yanga kitakachoondoka nchini kesho kwenda Uturuki kwa kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) dhidi ya MO Bejaia ya Algeria mwishoni mwa wiki ijayo.
Hata hivyo wachezaji wapya wa timu hiyo, mabeki Hassan Kessy kutoka Simba, Vicent Andrew ‘Dante’ kutoka Mtibwa na Juma Mahadhi kutoka Coastal Union ni miongoni mwa nyota watakaokuwemo katika msafara huo.
Meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh alisema jana kuwa wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali. “Juma Abdul ni majeruhi, hivyo hatoweza kwenda, Telela yeye mkataba wake umeisha na mpaka sasa uongozi bado haujamuongezea,” alisema Meneja huyo.
Hata hivyo,Telela inadaiwa tayari amefanya mazungumzo na timu za Simba na Azam kwa nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Kwa mujibu wa Saleh, wachezaji Mahadhi, Dante na Kessy watakuwepo kwenye msafara huo na kwamba wanaamini timu yao itaenda kufanya vizuri ugenini.
Alisema mara baada ya mchezo na MO Bejaia watarejea Uturuki kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na watarejea nchini siku mbili kabla ya mchezo huo.
Yanga imepangwa Kundi A katika michuano hiyo na TP Mazembe ya DRC, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana na itaanza ugenini nchini Algeria wiki ijayo. Kwa upande wa Kundi B zipo timu za Kawkab Athletic, Fath Union Sports zote za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli ya Libya.

Amuua mkewe, achoma moto nyumba mbili

Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime
MKAZI wa kitongoji cha Nyabirama kijiji cha Matongo Nyamongo, Tarafa ya Ingwe, wilayani Tarime mkoani Mara Wambura Mrimi (50) amepata kipigo kutoka kwa wananchi na kulazwa akiwa na hali mbaya kwa tuhuma za kumchinja kwa kumkata shingo mke wake Maria Maningo (38) na kuchoma nyumba zake mbili baada ya kumhusisha mke wake na imani za kishirikina.
Mrimi amelazwa katika Hospitali ya wilaya Tarime akiwa chini ya ulinzi mkali. Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, ACP Andrew Satta alisema kuwa tukio hilo la mauaji lilifanyika June 8, mwaka huu katika kitongoji cha Nyabirama, kijiji cha Matongo Nyamongo baada ya kutokea ugomvi kati ya mke na mume.
Alisema Mrimi alikuwa akimtuhumu mke wake Maria kuwa anamloga na kushiriki katika mambo ya kishirikina lakini mke alikuwa akikana tuhuma hizo. Kamanda Satta alisema wakati wakigombana mtuhumiwa Mrimi alikuwa na panga mkononi ndipo alipomkata shingo mkewe na kuacha panga limeninginia na kisha kuchoma nyumba zao mbili zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.
Thamani ya nyumba hizo na mali zilizoteketea hazikuweza kufahamika mara moja. Alisema wananchi ambao ni wakazi wa kitongoji hicho cha Nyabirama walisikitishwa na kitendo hicho na kuamua kupiga yowe na kumkamata mtuhumiwa na kuanza kumshambulia kwa mawe hadi alipookolewa na polisi waliofika mapema eneo hilo na kumchukua kwa gari akiwa hajitambui.
Kamanda Sitta alisema mtuhumiwa huyo alikimbizwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi na yupo chini ya ulinzi wa Polisi hadi sasa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nyamongo kwa uchunguzi zaidi wakati ukisubiri kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko.