ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 24 Julai 2016

Maamuzi ya Wizara ya Elimu kuhusu wanafunzi wanaotakiwa kwenda Field na mikopo yao

WhatsApp-Image-20160723

Kapombe afuata nyayo za Messi, Aguero

Azam FC
UNAWEZA ukashangazwa lakini huu ndio utambulisho mpya wa beki wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, ambaye ameamua kuja na staili mpya ya kufuga ndevu zake kuelekea msimu ujao.
Kapombe amewashangaza watu wengi kufuatia staili yake hiyo, aliyoanza kuonekana nayo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, tokea alipoanza mazoezi mepesi ya gym Jumanne iliyopita.
Beki huyo ameanza mazoezi baada ya kupona ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu), uliokuwa ukimsumbua na kumfanya akae nje ya dimba kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu staili yake hiyo mpya, Kapombe amesema staili hiyo ndio itakayomtambulisha msimu ujao na kudai kuwa hawezi kuzinyoa ndevu hizo mpaka pale atakapofunga ndoa na mchumba’ke aliyekuwa naye sasa.
“Mchumba’ngu ndio kaniambia nifanye hivi, ameniambia napendeza sana nikiwa na ndevu hizi, nasikiliza ushauri wake na nitazinyoa tutakapofunga ndoa hivi karibuni,” alisema.
Kapombe, 23, aliyecheza jumla ya dakika 3188 msimu uliopita, amefuata nyayo za wachezaji mahiri duniani kutoka Argentina, Mchezaji Bora wa Dunia, Lionel Messi na staa wa Manchester City, Sergio Aguero waliowahi kufuga ndevu zao lakini wao wakikamia ubingwa wa Copa America mwaka huu.
Wawili hao waliweka kiapo cha kutonyoa ndevu hizo wakati wakiiongoza Argentina kwenye michuano ya Kombe la Copa America wiki chache zilizopita wakiamini kuwa ni uchawi utakaowapa taji la michuano hiyo na kuondoa mkosi wa kukosa mataji, lakini walishindwa kwa kufungwa na Chile kwa mikwaju ya penalti 4-2 kwenye mchezo wa fainali.

Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM

Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.
CLkG9v5UYAEMLK6Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman  Mbowe alipokuwa akimkabidhi kadi Mgana Msindai mara baada ya kutangaza kuhamia chama hicho.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.
Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama, alisema mjumbe huyo.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) Machi 2010.
 
Mwigizaji Jackline Wolper akiongea katika mkutano wa Edward Lowassa aliofanya na Wanawake wa CHADEMA jiji Dar es Salaam Agosti 2015.

Alichokiandika Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kupewa uenyekiti wa CCM

Leo July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM  Leo July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM   baada ya kupigiwa kura za ndio 2398  kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika
Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…
>>>’Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda‘
Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.’ –Zitto Kabwe

‘Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.‘ –Zitto Kabwe
ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu

wasanii wamuaga kikwete kwa huzuni kubwa

Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kimpya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipiti cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho.

Wasanii wameyasema hayo usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma walipofanya tamasha la Usiku wa Wasanii kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi uwenyekiti wa chama hicho na kumuachia uongozi Rais John Magufuli
ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu

Magazeti ya Leo jumapili ya tarehe 24/07/2016














ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu