ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 15 Agosti 2016

Magazeti ya Leo jumatatu ya tarehe 15/08/2016

Kikoti education centre 
Inapenda kuwataarifu wanafunzi wake wote wanaotarajia kuhitimu darasa la saba tarehe 08/09/2016 kuwa itaanza usajiri na kufundisha pre form one kuanzia tarehe 09/09/2016 katika kituo chao cha ilula Madizini katika majengo ya kanisa katoriki 
GHARAMA: 20000 KWA MUDA WA MIEZI MITATU
MWANAFUNZI ATAPEWA : TISHETI, PENI PENSEL NA DAFTALI PIA VITABU VITAUZWA NA KUGAWIWA KWA MAKUNDI
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NO 0769694963 AU FIKA KIKOTI EDUCATION CENTRE ILULA MADIZINI MAJENGO YA KANISA KATORIKI MADIZINI 
EDUCATION FOR LIFE




















Jumamosi, 13 Agosti 2016

Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 13/08/2016


















KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI
Mzazi/Mlezi wa ………………………………………………,kikoti education centre inapenda kukutarifu kuwa inatarajia  kuaanza kutoa elimu ya pre-form one kwaajili ya maandalizi ya kidato cha kwanza. Kuanzia tarehe 09/09/2016.Kwa gharama ya shilingi elfu ishirini(20,000) tu kwa muda wa miezi mitatu(3), ambapo mwanafunzi atapewa vitu vifuatavyo:-
1)      Tisheti  yenye jina la kituo
2)      Daftali, peni na pensel
3)      Vitabu vya masomo husikaVitakuwepo
4)      Mitihani kila wiki kupima maendeleo ya mwanafunzi
5)      Masomo yatakayopewa kipaumbele ni masomo yote ya sayansi(biology, chemistry,physics, mathematics na English ,GEOGRAPHY)
-          Mlete mwanao apate elimu bora kutoka kwa walimu bora na wenye taaluma na maadili ya ualimu kutoka vyuo vikuu bora Tanzania
Pia kikoti education centre wanaendelea na kutoa tuition kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita kama kawaida
OUR MOTTO: EDUCATION FOR LIFE
Kwa mawasiliano zaidi tupigio kwa namba 0769694963, 0625682117 au 0757927380 au fika kikoti education centre kwa maelezo zaidi:
MAHALI : ilula madizini- majengo ya kanisa katoriki,  mita 50 kutoka soko la TASAF.

Ijumaa, 12 Agosti 2016

TAHADHARI DHIDI YA MATAPELI KWA WAOMBAJI WA MIKOPO NA WADHAMINI WAO

Image result for heslbBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwatahadharisha  waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na umma kwa ujumla kuwa imepokea taarifa kuwa kuna watu wasio waaminifu ambao si watumishi wa Bodi ambao huwapigia simu baadhi ya waombaji kwa lengo la kuwatapeli.

Taarifa hizo za kitapeli zimekuwa zikisambazwa katika siku za hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwataka baadhi ya waombaji wa mikopo au wadhamini wao kutuma fedha (Tshs 39,000/-) kwa namba ya simu 0716463190 ili fomu zao za maombi ya mikopo zilizowasilishwa Bodi zirekebishwe kwa kuwa zimeonekana zina makosa na hivyo hawatapata mikopo.
Namba inayotumika kusambaza taarifa hiyo au kupiga simu kutoa taarifa hizo ni 0764640325 na mtu anayepiga anajitambulisha kwa jina la Charles Amos.
Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kuwa taarifa hizo si za kweli. Mtu huyo ni tapeli na si mtumishi wa Bodi ya Mikopo.
Iwapo waombaji watapigiwa simu na matapeli hao, watoe taarifa kwa vyombo vya dola kwa hatua zaidi.
Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kuwa utaratibu wa Bodi kuwasiliana na waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi hubainika kuwa na upungufu haujabadilika. Mara baada ya kazi ya ukaguzi wa fomu kukamilika, Bodi ya Mikopo itatoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo tovuti hii ya Bodi na kuwaalika waombaji kufanya marekebisho.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
IJUMAA, AGOSTI 12, 2016

Serikali: Hatuna ushahidi wa kuzihukumu shule za Feza, Hivyo Hatuwezi Kuzifunga

SERIKALI imesema haina ushahidi wa kutosha kuzitia hatiani shule za Feza nchini zinazodaiwa kumilikiwa na mmoja wa wananchi wa Uturuki anayetuhumiwa kujihusisha na ugaidi na kuitaka Serikali ya Uturuki kuwasilisha taarifa zenye ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.


Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga.

Alisema walipokea madai kutoka Ubalozi wa Uturuki nchini kuwa shule hizo zinamilikiwa na mmoja wa wananchi wa nchi hiyo anayejihusisha na ugaidi.

Balozi Mahiga alisema katika madai ya ubalozi huo, shule hizo ni miongoni mwa miradi inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo na kwamba, baadhi ya walimu wake hutumia mbinu za kigaidi kufundisha wanafunzi.

Akijibu tuhuma hizo, Balozi Mahiga alisema serikali kabla ya kutoa kibali kwa mwekezaji au mfanyabiashara yeyote kuendesha shughuli zake nchini, vyombo vya usalama nchini, hufanya upelelezi wa kina na wamejiridhisha kwamba wafanyabiashara wa Uturuki waliopo nchini wanafanya biashara halali.

“Ni kweli tumepokea tuhuma kutoka kwa Ubalozi wa Uturuki nchini kuhusu shule za Feza kwamba ni sehemu ya makundi ya kigaidi, lakini hatuwezi kuzitia hatiani shule hizo hadi tuletewe ushahidi wa kutosha,” alisema Balozi Mahiga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule za Feza, Habib Miradji alisema shule hizo ni za asasi iliyosajiliwa kisheria na Serikali ya Tanzania hivyo ni mali ya Tanzania na endapo kuna kitu au tatizo ni lazima wawasiliane na serikali na watafika kukagua ili kama kuna lolote baya hatua zichukuliwe.

Aidha alisema kwamba shule hazijafungwa.