Jumatano, 7 Septemba 2016
Jumanne, 6 Septemba 2016
Jumatatu, 5 Septemba 2016
Jumapili, 4 Septemba 2016
TAARIFA KWA UMMA - ILULA
KIKOTI EDUCATION CENTRE ILULA – MADIZINI
TAARIFA KWA UMMA
Mkuu wa kituo cha tuition cha KIKOTI
EDUCATION CENTRE kwa niaba ya uongozi wa TUITION CENTRE
na watumishi wote, anapenda kukanusha taarifa iliyoenezwa na mwalimu wa kituo
cha MWALIMU EDUCATION CENTRE-Diginayo Kwamba walimu wake wote wameondoka
kuelekea masomoni Pamoja na maneno ambatishi na tunaomba endeleeni kuleta na
kuandikisha wanafunzi kama kawaida na hatua zaidi za kisheria zinaendelea
kuchukuliwa na wanasheria wetu kujua lengo la mwalimu huyo: lakini pia tunaomba
umma wa wanailula utambue mambo yafuatayo kutoka mmliki wa kituo hicho
kinachojiita MWALIMU EDUCATION CENTRE:
- Hana madarasa ya kufundisha hivo
analazimika kufundishia wanafunzi kwenye ukumbi ambao ulikua unatumika kama bar
au sehemu ya kuuzia vinywaji ambayo ni kinyume na sheria na taratibu za wizara
ya elimu
- Pia mmliki huyu ni mtumishi wa umma anayepaswa kuwepo
kazini mda wote ambapo wanafunzi wenu watakuwa wakipata elimu kwenye ukumbi
huo.
- Ameshindwa kufuata sheria na taratibu kwa kusambaza
taarifa za uongo kwa wanafunzi alipokuwa akifanya promosheni kwenye shule
mbalimbali tena mdaaliopaswa kuwepo kazini yaani kati ya saa nne asubuhi mpaka
saa tisa na nusu
Kama kituo tumefanya mambo yafuatayo,
- Tumemwandikia barua Afisa wa elimu wilaya yenye kumbukumbu
no K.E.S/0012/2016 kumjulisha anachokifanya mtumishi wao na kumtaka kupitia
Mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi kufanya yafuatayo:
- kueleza sababu za kusambaza taarifa za uongo kwa maandhishi.
- mkurugenzi kutathimini kuona kama ni haki kwa mwajiri wake kufanya tuition mda wa kazi tena katika mazingira hatarishi.
- mwisho tumemtaka mwalimu huyo kufuta kauli hizi kupitia vyombo hivi vya habari kama tulivofanya sisi.
MWISHO:Tunapenda kuomba radhi kwa
wazazi wote mliokuwa mmekwisha kuandisha wanafunzi toka mwezi wa nane kwa hofu
mlioipata mda wote na tunaendelea kuwakaribisha wazazi wote kuleta wanafunzi KIKOTI
EDUCATION CENTRE -ILULA MADIZINI MAJENGO YA KANISA KATORIKI aweze kupata elimu
bora kutoka kwa walimu bora
Our moto: education for life
MWANASHERIA MKUU K.E.C
MWANASHERIA MKUU K.E.C
..........
Alfonce jackson kisoma
Misael Benitho
kikoti
NAKALA, Tarehe
29/08/2016
mkuu wa Mwalimu Education,
Mtendaji wa kijiji cha Dinginayo,
Afisa elimu wilaya ya kilolo,
Katibu tawala wilaya na mkoa(DAS&RAS)
Vyombo vya habari Iringa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)