ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 15 Januari 2017

Matokeo ya Kidato cha Pili Yatangazwa yatazame hapa

Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.

Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa

Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.

Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55

Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History, Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.

Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya wanafunzi wote, wamefaulu na soko lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic Mathematics ambapo asilimia 21.55 wamefaulu.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa Canosa ya Dar es Salaam.

Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.

Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu
.

Magazeti ya Leo jumapili ya tarehe 15/01/2017







































Jumamosi, 14 Januari 2017

TANGAZO KWA UMMA: KUHUSU WAHITIMU WA SHAHADA NA STASHAHADA ZA UALIMU (SAYANSI) WALIOTAKIWA KUWASILISHA VYETI

Image result for moevt
TAREHE 12/12/2016 WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO KWA
AJILI YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.

WAHITIMU WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-
     (1) WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA AU SHAHADA
     (2) WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION – PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;
WAHITIMU AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.
WAHITIMU AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI .
WAHITIMU WALIOPO KWENYE ORODHA HAPO JUU WASIWASILISHE NYARAKA HIZO TENA.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. WAOMBAJI LAZIMA ‘WA-SCAN’ VYETI HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES - KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA, STASHAHADA YA UZAMILI AU SHAHADA) NA SIYO KIVULI CHA CHETI (PHOTOCOPY) ;
  2. WAOMBAJI WA STASHAHADA YA UZAMILI (PGDE) NA SHAHADA LAZIMA ‘WA-SCAN’ NA KUTUMA NAKALA ZA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZA SHAHADA YA KWANZA.
  3. WAOMBAJI LAZIMA WAWEKE NAKALA ZA VYETI VYAO VYOTE KWENYE ‘FILE’ MOJA LIKIWA KATIKA ‘PDF’ NA LIPEWE JINA LA MWOMBAJI HUSIKA KABLA YA KUTUMA. NYARAKA ZITUMWE KUPITIA ‘BARUA PEPE’ ZAO WENYEWE NA SIYO ZA WATU WENGINE.
TANBIHI:
  1. WAOMBAJI WATUME TAARIFA ZAO KUPITIA BARUA PEPE YA WIZARA info@moe.go.tz
  2. TAREHE YA MWISHO KUPOKEA NYARAKA NI 17 JANUARI,2017.
  3. BARUA PEPE ZA KUWASILISHA NYARAKA ZA WAOMBAJI ZITUMWE MARA MOJA TU NA SI KWA KURUDIA RUDIA ILI KUEPUKA USUMBUFU WA KUTAFUTA ZILIZO SAHIHI.

IMETOLEWA NA
PROF. SIMON S. MSANJILA
KAIMU KATIBU MKUU
12/01/2017