ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 3 Februari 2017

MCH MSIGWA MBUNGE WA IRINGA ATOA MIL 1.5 KAMA MOTISHA TU KWA LIPULI FC.... we unasubiri nini?

Wakati kesho jumamosi timu ya wanaIringa Lipuli Fc inaingia katika mchezo wake muhimu wa kuingia kucheza ligi kuu ya VPL baada ya kuwa na uhakika wa kutwaa pointi 3 zilizosalia,  wadau  wa mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema) wameahidi kutoa motisha ya Tsh milioni 1.5 kwa timu ya Lipuli Fc .

Katika taarifa iliyotolewa na Mbunge Msigwa ambae yupo mjini Dodoma kuendelea na vikao vya bunge amesema yupo tayari kesho kuungana na wabunge wengine wa mkoa wa Iringa kuja kuishangilia timu ya Lipuli fc pamoja na mashabiki wengine.

Uzalendo huu ambao mbunge wetu aendelea kuonyesha ni wazi ligi kuu Iringa ipo mbioni kufanyika mkoani hapa  msimu ujao.

Tayari wabunge mbali mbali kama Ritta Kabati , Venance Mwamoto ,Costa Chumi, Mahamudu Mgimwa, Godfrey Mgimwa na wengine wameendelea kuisaidia timu ya Lipuli Fc .

Iwapo upo tayari kuchangia Lipuli Fc Tuma mchango wako kuanzia tshs 10,000/= kwenda namba 0713446699  na 0754695874  *zote Abousufian Silia..

Wasanii watii Amri ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda

 

TID akiingia lango la central polisi 

Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwataka baadhi ya mastaa wanaoshukiwa kujihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuwasili kituo cha polisi cha kati siku ya leo baadhi ya mastaa wametii agizo hilo na kuwasili.


Wema Sepetu ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Da es salaam Paul Makonda kwamba anatumia Madawa ya kulevya, amewasili kituoni hapo  huku akiwa amevalia vazi la  hijab.

Wasanii wengine waliofika kituoni hapo ni pamoja na TID, Nyandu Tozzy pamoja na mtangazaji wa Clouds TV Babu wa Kitaa. 



#MAGAZETINI LEO# Rais Magufuli aitaka Mahakama kufuatilia madeni ya kesi serikali ilizoshinda

Na Beatrice Lyimo - MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo jana  jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Alisema  kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo  Serikali imeshinda kesi hizo japo  fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
 
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
 
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.
 
Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.
 
Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
 
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.

Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kes

#MAGAZETINI LEO# Mbowe na Naibu Spika Dr Tulia Ndani ya BIFU Jipya

 
Mvutano  umeibuka bungeni kati ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya Mbunge huyo wa Hai kumwuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa swali lililopingwa na Naibu Spika kwa maelezo kuwa ni la kisheria si la kisera.

Sakata hilo liliibuka asubuhi katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, baada ya Mbowe kuhoji sababu za Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kusota rumande kwa kukosa dhamana, Peter Lijualikali wa Kilombero anayetumikia kifungo cha miezi sita gerezani na wanachama wengine wa Chadema wanaokabiliwa na mashitaka mbalimbali.

Mbowe alimtaka kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni, aeleze kama ni sera ya Serikali kuua vyama vya upinzani, huku akisema Rais John Magufuli alipata kutamka kuwa atavimaliza vyama vya upinzani kabla ya mwaka 2020.

Kwa maswali hayo, Dk Tulia alimtaka Waziri Mkuu kujibu swali linalohusu sera na kuachana na yanayogusa masuala ya kisheria.

Jambo hilo liliwafanya wabunge wa Upinzani huku wakipiga meza kwa takribani dakika tano kupinga, wakimtaka Naibu Spika aache Waziri Mkuu ajibu swali hilo.

Katika swali lake la msingi, Mbowe alisema wakati jana ikiwa ni Siku ya Haki Duniani, imepita miezi mitatu tangu Lema aanze kusota rumande huku akinyimwa dhamana licha ya kuwa iko wazi.

Pia alisema Lijualikali anatumikia kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kisiasa sambamba na mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew aliyefungwa miezi minane na madiwani zaidi ya sita na viongozi wengine 215 nao wakifungwa au kuendelea na mashitaka huku zikifanyika hila za kuidhoofisha CUF.

“Haya yanayoendelea katika Serikali ambayo ni kinyume na utamaduni na mazoea yetu kama Taifa, je ni utekelezaji wa sera ya kuua upinzani chini ya Rais Magufuli?” Alihoji Mbowe.

Kabla ya Waziri Mkuu kujibu swali hilo, Dk Tulia aliingilia kati na hali kuwa hivi:

Dk Tulia: Katika swali lako kuna masuala ya kisera na kisheria. Maswali yanayomhusu Lema na Lijualikali na madiwani sita ni ya kisheria, hayo kuhusu leo (jana) kuwa siku ya haki duniani, Waziri Mkuu anaweza kuyajibu.

Majaliwa: Nakanusha, Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani, nchi inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu na kuna Bunge, Serikali na Mahakama. Hakuna mhimili unaoingilia mhimili mwingine. Jambo lililopo mahakamani halizungumzwi kokote, siwezi kuzungumzia hilo.

Mbowe: Kwa kuwa Rais anaonekana kuvunja Katiba ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, je tukileta ushahidi kuwa Rais amekusudia kuumaliza upinzani kabla ya 2020, Waziri Mkuu utakuwa tayari kuwajibika kwa kujiuzulu?

Dk Tulia: Mbowe swali lako la maelezo ya jumla, yako sawasawa ila la kumtaka Waziri Mkuu kuwajibika si la kisera, kuwajibika si sera uliza swali la kisera.

Mbowe: Labda swali langu nilielekeze kwa Naibu Spika (Dk Tulia). Swali langu lilikuwa la mwendelezo ambalo hutokana na majibu ya msingi yaliyotokea. Kama kulikuwa na msingi wa kisera kwenye swali la msingi, swali la mwendelezo linakwenda kutokana na majibu yaliyotolewa. Waziri Mkuu aseme tu kama yupo tayari kujiuzulu tukileta ushahidi.

Katika maelezo yake, Dk Tulia alitaka Mbowe ajikite katika swali la kisera jambo ambalo Mwenyekiti huyo wa Chadema alipinga na kusisitiza kuwa huenda mambo yanayofanyiwa wapinzani, wabunge, mawaziri Serikali inayafurahia.

Magazeti ya Leo ijumaa ya tarehe 03/02/2017