Jumanne, 21 Machi 2017
Jumatatu, 20 Machi 2017
Ruge athibitisha Makonda kuivamia Clouds media akiwa na silaha
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uendeshaji wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba amehojiwa leo katika kipindi cha 360 cha televisheni ya Clouds
na kuthibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
alivamia kituo hicho..
Akizungumza
na watangazaji wa kipindi hicho, Ruge aliongea kwa hisia na
kuthibitisha kuwa tukio hilo lilitokea siku ya ijumaa ya tarehe 17
majira ya usiku kituoni hapo.
Alieleza
kuwa, siku ya Alhamisi RC makonda alifika katika kituo hicho na kuongea
na watangazaji wa SHILAWADU, Sudy Brown na Qwisser ambapo alisema kuwa
wanapiga tu stori.
“Mtangazaji
mmoja alinifuata akaniambia wamefanya mahojiano na mwanamke anayedaiwa
kuwa amezaa na Askofu Gwajima lakini Gwajima mwenyewe hawajampata.
Niliwaambia watangazaji kama hawajampata Gwajima, basi kipindi hicho
kisirushwe kwa kuwa hakina ‘balance’ na wamwambie Makonda.”
“Gwajima
alinipigia simu akisema amesikia kuwa kuna kipindi chake, nikamwambia
kuwa hakitarushwa kwa sababu hatujasikia pande zote. Na nikampigia simu
mkuu wa vipindi kumwambia ahakikishe kuwa kipindi hicho hakirushwi kwa
vile hakijabalance.”
“Ijumaa
saa 5 usiku nikapigiwa simu na Afisa Rasilimali Watu wa Clouds kuwa
Makonda amekuja ofisini akiwa na Askari na wana bunduki. Mlinzi
hakusita kumruhusu aingie kwa vile amemzoea Makonda, ila alishtushwa na
Askari wale waliokuwa na Bunduki.”
“Nilimwambia
mlizi aende juu studio aone kuna nini na alipokwenda alimkuta Makonda
anachukua kipindi kwenye ‘flash’ kisha akaondoka nayo. Hakuna kijana
yeyote aliyepigwa usiku ule lakini tatizo kubwa ni namna tukio zima
lilivyotokea.”
“Makonda
alikuja pale na Askari baada ya kuona kipindi chake hakirushwi, hivyo
ni kama alikuja kuhoji sababu za kutorushwa kwa kipindi hicho.” Alisema Ruge Mutahaba wakati wa mahojiano leo asubuhi.
Akizungumza
kuhusu video za kamera za ulinzi (CCTV) zilizosambazwa kwenye mitandao
ya kijamii, Ruge alikiri kuwa video hizo ni za Clouds lakini hajui ni
nani alizitoa kwa sababu wafanyakazi wengi wanafahamu mitambo ya CCTV
ilipo hivyo yeyote anaweza kutoa.
Vilevile
Ruge ameeleza kuwa amesikitishwa sana na kitendo alichokifanya rafiki
yake Paul Makonda kwani kilikuwa ni kitendo cha kuivunjia heshima Clouds
Media Group pamoja na wadau wengine.
“Makonda tumesaidiana sana tangu akiwa mkuu wa Wilaya. Kwa nini leo anafika kuja ofisini kwangu na bunduki?” alisema.
“Makonda tumesaidiana sana tangu akiwa mkuu wa Wilaya. Kwa nini leo anafika kuja ofisini kwangu na bunduki?” alisema.
“Makonda
ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam lakini ni mdogo sana kwangu kiumri,
lazima tuheshimiane. Sijayasema haya kwa sababu nataka mtu atumbuliwe,
bali nataka heshima kwenye kile tunachokifanya.”
“Sasa tunakuwa tunampa Rais Magufuli mambo mengine ya kufanya ambayo hakutakiwa kuwa anayawaza.”
Pamoja
na hayo aliongeza kuwa, wao kama Clouds Media Group hawana ugomvi na
serikali na ameahidi kutoa nafasi kwa kiongozi yeyote mwenye ajenda ya
maendeleo kuja Clouds na atapewa muda wa kuzungumza.
“Sisi tunatafuta viongozi wabunifu. Viongozi wanaokuja na mipango inayoweza kumwezesha mnyonge kuuona mwanga. Viongozi wanapaswa kufanya mijadala ya namna ya kuongeza maendeleo. Inapaswa tushirikiane kutengeneza timu moja na kushirikiana.”
“Sisi tunatafuta viongozi wabunifu. Viongozi wanaokuja na mipango inayoweza kumwezesha mnyonge kuuona mwanga. Viongozi wanapaswa kufanya mijadala ya namna ya kuongeza maendeleo. Inapaswa tushirikiane kutengeneza timu moja na kushirikiana.”
Mkurugenzi
Ruge Mutahaba, alimaliza kwa kusema kuwa amelizungumzia jambo hilo leo
ili limalizike na watu waendelee kufanya mambo mengine ya kuisaidia nchi
kimaendeleo.
Vilevile amewataka viongozi na wanasiasa kutokushindana kupata ‘kiki’ kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Vilevile amewataka viongozi na wanasiasa kutokushindana kupata ‘kiki’ kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Jumamosi, 18 Machi 2017
Tundu Lissu Achaguliwa Kuwa Rais wa TLS Kwa Ushindi wa Asilimia 88
Wajumbe
wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa
kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama
chao.
Uchaguzi
huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama wa TLS wamekutana
kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji
kazi wa chama hicho.
Matokeo ni kama ifuatavyo:
Urais: Kura zilizopigwa 1682
- Tundu Lissu 1411 sawa na asilimia 88
- Francis Stolla 64
- Victoria Mandari 176
- Godwin Mwapongo 64
==>Kwa
upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi
aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.
Council Members
- Jeremiah Motebesya
- Gida Lambaji
- Hussein Mtembwa
- Aisha Sinda
- Steven Axweso
- David Shilatu
- Daniel Bushele
Ijumaa, 17 Machi 2017
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)