ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 16 Agosti 2017

Kupima UKIMWI sasa ni lazima ZAMBIA

Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba.

Rais Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya serikali ya kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.

Katika tangazo hilo, kiongozi huyo amesisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya wale walioathirika na wale ambao wako hatarini kuambukizwa virusi hivyo.

Amesema, licha ya sera hiyo kukiuka haki ya mtu kupima kwa hiari lakini akasisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kuweka rehani maisha ya binadamu mwenzake.

Sera hiyo inakiuka muongozo wa Shirika la Afya Duniani, WHO, na Shirika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS, unaohamasisha watu kupima Vvu na kupata ushauri nasaha kwa hiari.

Zambia ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo kusini mwa bara la Afrika ikiwa na asilimia 11.6 huku watu walio na umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.

Magazeti ya leo jumatano ya tarehe 16/08/2019


Jumanne, 15 Agosti 2017

Magazeti ya leo jumanne ya tarehe 15/08/2017

Rais Magufuli, Dangote, Obama kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Magufuli na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Kamati ya maandalizi ya sherehe hizo inayoongozwa na Katibu Kiongozi, Joseph Kinyua imebainisha kuwa imeandaa orodha ya majina ya viongozi wa kimataifa kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria la uapisho wa Kenyatta endapo ushindi wa Kenyatta hautopingwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, sherehe za uapisho hufanyika siku 14, baada ya mshindi wa uchaguzi kutangazwa ili kutoa fursa kwa chama chochote kinachotaka kupinga matokeo kufanya hivyo.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kualikwa katika sherehe hizo wakiwemo wakuu wa nchi ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.

Aidha, katika orodha hiyo pia yupo Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, mfanyabiashara tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote, Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia, Aga Khan, Waziri Mkuu mstaafu wa Italia, Matteo Renzi na Rais Xi Jinping wa China.

“Tupo kwenye maandalizi ya sherehe za uapisho wa Rais wakati tukisubiria hatua za kikatiba kukamilika. Orodha hii ni ya marafiki wa Kenyatta, viongozi wa Afrika na viongozi wengine wa kimataifa, tunaotarajia kuwaalika”, amesema mmoja wa wanakamati hiyo ya maandalizi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi Kenya, Wafula Chebukati mwishoni mwa wiki alimtangaza rasmi Rais Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kuwa washindi katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita nchini humo.