Jumatatu, 9 Oktoba 2017
Jumapili, 8 Oktoba 2017
Jumamosi, 7 Oktoba 2017
Ijumaa, 6 Oktoba 2017
Alhamisi, 5 Oktoba 2017
Taarifa muhimu ya TCU kwa wanafunzi waliokosa vyuo
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa awamu ya kwanza
ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za
awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017.
Tume
inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji
wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa
2017/18.
Hata
hivyo kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kutokana na sababu
mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili
kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo
kuomba udahili:
• Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza;
• Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza;
• Waombaji wenye vigezo vya Stashahada walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN);
• Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na
• Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho toka vyuo vyao vya awali.
Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaritibu wa kutuma
maombi ni ule ule uliotumika katika awamu ya kwanza ya Udahili.
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
4 Oktoba 2017
Jumapili, 1 Oktoba 2017
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)