Na mwandishi wetu;Kijangai y
Wengi wangekuja na orodha isiyokuwa na mwisho ambayo inaeleza tofauti tofauti kuhusu tabia nzuri za mwanamke.
Hapa tumekuja na orodha ya sifa nzuri na muhimu zaidi ambazo zinafaa kutumiwa kama kuwa kigezo cha kupima tabia nzuri za mwanamke.
Kwa kuwa wanawake huwa na tabia tofauti tofauti, hatuwezi kusema lazima mwanamke awe na tabia zote hizi ili asomeke kama mwanamke mwenye tabia nzuri. La. hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mwanamke anaweza kuwa nazo, na nyingine kutokuwa nazo na bado akaorodheshwa kuwa na tabia nzuri. Zama nami.
Hapa tumekuja na orodha ya sifa nzuri na muhimu zaidi ambazo zinafaa kutumiwa kama kuwa kigezo cha kupima tabia nzuri za mwanamke.
Kwa kuwa wanawake huwa na tabia tofauti tofauti, hatuwezi kusema lazima mwanamke awe na tabia zote hizi ili asomeke kama mwanamke mwenye tabia nzuri. La. hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mwanamke anaweza kuwa nazo, na nyingine kutokuwa nazo na bado akaorodheshwa kuwa na tabia nzuri. Zama nami.
Baadhi ya sifa nzuri kutoka kwa mwanamke
1. Kusamehe
Ni vigumu kuwa katika uhusiano halafu uwe hauna moyo wa kumsamehe mpenzi
 wako. Kawaida katika mahusiano, huwa kuna changamoto kadhaa ambazo 
hujitokeza hivyo lazima uwe na tabia ya kuweza kusamehe. Hii inaweza 
kuanzia kukosana kwa mambo ya kinyumbani, ama mambo mengine 
yanayofanana.
Mwanamke mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kumsamehe mpenzi wake bila 
kuweka kinyongo. Iwapo mpenzi wako umemshika katika fumanizi nk na bado 
unampenda, basi jambo zuri la kufanya ni kumsamehe na kuendelea na 
maisha.
2. Msikilizaji mzuri
Mara nyingi migogoro ambayo inatokea majumbani kati ya wapenzi wawili 
husababishwa na kutosikilizana. Huyu akiambiwa hivi huyu anajibu hivi. 
Well, iwapo mwanamke anataka mahusiano yake yake marefu na ya kufaana, 
basi anapaswa kuwa msikilizaji mzuri.
Mwanamke ambaye huwa anatulia na kumsikiliza mpenzi wake, mahusiano yake
 na mpenzi wake huwa ya furaha zaidi ukilinganisha na ya yule ambaye 
hatilii maanani maoni ya mwenzake. 
3. Mwaminifu
Hii ni kuanzia kuongea ukweli bila kudanganya hadi maswala ya chumbani. 
Iwapo mwanamke ana mchepuko mahali fulani ama anamwendea kinyume mpenzi 
wake, basi aina hii ya tabia haifai kabisa.
Sifa ya mwanamke mzuri ni ile ambayo ni ya uaminifu. Mwanamke mwaminifu 
kwa mpenzi wake haitofika wakati fulani ambapo atakosana na mpenziwe.
4. Msaidifu
Katika mahusiano, kuna wakati fulani hufika ambapo lazima wapenzi wawili
 wasaidiane kufanya jambo ama kutimiza kitu fulani. Hivyo mwanamke mzuri
 ni yule ambaye anatoa msaada wa kumsaidia mpenzi wake na jambo fulani. 
Mathalan inaweza kuwa kumsaidia kimawazo, kifedha ama jambo tofauti. 
Mwanamke mwenye tabia hii humpendeza sana mpenzi wake kwa kuwa 
inaonyesha ya kuwa mwanamke kama huyu ana uwezo wa kumtumikia mpenzi 
wake wakati ambapo anaweza kupatwa na majanga. 
5. Mwenye imani
Kuna tabia za wanawake ambazo huwachosha wanaume, nazo ni kukosa imani. 
Iwapo wewe una tabia za kutokuwa na imani basi tabia kama hio unafaa 
kuiacha mara moja. Tabia za kutokuwa na imani ni kama vile kuharakisha 
jambo, kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani nk.
Hali kadhalika, mwanamke mwenye imani ni yule ambayo ana subira. Iwapo 
ameambiwa na mpenzi wake kuhusu jambo fulani, basi yeye hutulia hadi 
kungojea matokeo yake.
6. Kuhamasisha
Wanaume humpenda mwanamke ambaye anatoa motisha ili kumsaidia kutimiza 
lengo lake. Vile vile kwa kawaida kuna wanaume ambao wanahitaji kiinua 
mgongo ili kutimiza mambo fulani. Hivyo wewe kama mwanamke, mara moja au
 nyingine unafaa kuonyesha umotisha wako kwa kumuelekeza mpenzi wako 
mara moja au nyingine. 
7. Mcha Mungu
Mwanamke mcha Mungu bila shaka maisha yake huwa ya kufanikiwa. Mtu 
yeyote yule lazima awe mcha Mungu ili awe na sifa nzuri ya maisha katika
 jamii.
8. Heshima
Heshima haimaanishi ni kwa mpenzi wako pekee bali kwa jamii nzima. 
Mwanamke ambaye anapenda kugombana na majirani kila kukicha halafu 
ikifika jioni anamheshimu mpenzi wake hafai. 
Tabia za mwanamke mzuri ni yule ambaye anaheshimu na kuishi na majirani zake vizuri bila kuwa na mivurutano yeyote ile.
9. Anajiamini
Mwanamke mzuri ni yule anajiamini na anaamini mahusiano yake. Mwanamke 
mzuri ni yule ambaye hatasikia maneno ya watu halafu akampakizia mpenzi 
wake. Iwapo kuna swala tata ambalo linafanyika, basi mwanamke aina hii 
atamwekea kikao mpenzi wake na kujaribu kumuuliza maswali na kutaka 
kufafanua chochote ambacho kitakuwa kinamkwaza. Mwanamke aina hii 
hupendwa na wanaume kwa sababu anajua ya kuwa akifanya jambo fulani basi
 mpenzi wake atataka kuelezewa bila kuwa na hisia zozote mbaya.
10. Anajua mapenzi
Ikija katika swala la mapenzi, mwanamke mzuri ni yule ambaye anaujua 
mwili wake vizuri, hivyo si mwoga wa kuonyesha sehemu yake ya ndani ya 
mapenzi. Mwanamke huyu haoni aibu ya kujaribu mitindo tofauti tofauti ya
 kufanya mapenzi nk.
Wanawake ambao wanajua mapenzi ni moja wapo wa sifa nzuri ambayo wanaume wanapenda.
Hizi ni baadhi tu ya sifa za mwanamke mzuri. Iwapo unataka kuongezea ama kuchangia, angusha comment yako hapo chini.


                                    

