Alhamisi, 5 Aprili 2018
Jumanne, 3 Aprili 2018
HISTORY: FORM FOUR PAST PAPERS (NECTA) AVAILABLE HERE
The collection of History past papers
of Tanzania National assessment for form four (4), view or download in
this site through he following link. Find more past papers for other
subjects and Share to others
MBOWE ANENA
Mwenyekiti
wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya
kuachiwa huru yeye pamoja na viongozi wengine sita wa CHADEMA na kusema
kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi
karibuni.
Mbowe
amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya
kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na
wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.
"Leo
mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo
kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani
Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama
mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili
ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa
"Kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe
"Kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe
==>Msikilize hapo chini
Jumapili, 1 Aprili 2018
WARAKA WATIKISA
Askofu
Mkuu wa Makanisa ya Babtisti Tanzania, Mchungaji Arnold Manase
amewataka viongozi wa dini kushauri kwa namna njema bila kutabiria nchi
mambo mabaya kwani ubaya huenea haraka kuliko wema.
Aidha, amesema kila dhehebu nchini likisimama na kutoa waraka wake taifa halitakalika.
Askofu
Manase ameyasema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, jijini Arusha wakati
akitoa salam kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Jerusalem Babtisti
lilipo Ngarenaro mjini Arusha.
Kupitia
Ibada hiyo, Askofu Manase amewaomba wadau wa amani nchini, ikiwamo
Serikali kukaa na wadau ili kujadili mustabali wa taifa.
“Tunahitaji kuomba amani ya Mungu itawale, kama ambavyo Yesu Kristo alivyotuachia amani yake.
“Tukiwa
kama viongozi wa dini kama kuna mambo tunaweza kushauri basi tuyashauri
kwa namna njema tusitabirie nchi mambo mabaya Kwani ubaya unaenea
haraka kuliko wema, nawasihi tuhubiri amani,” amesema Askofu Manase.
Wanaopotosha Ukweli Waraka Wa Maaskofu KKKT Ni Wajinga
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo,
amesema wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa
kuupaka matope ni wajinga.
Askofu
Shoo ametoa kauli hiyo leo katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya
kaskazini, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka katika
ibada maalumu ya kusherekea sikukuu hiyo.
Amesema
kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia
nguvu nyingi kupotosha waraka wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope
kwa malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni
wajinga.
“Wapo
wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha ujumbe wa waraka wa maaskofu
na wamekuwa wakilipaka kanisa matope ili waweze kurejea katika waraka
ule, watu hawa naweza kuwaita ni wajinga lakini pamoja na hilo nataka
wakayatafakari na kama wanaona kuna hatua za kuchukua wachukue.
“Kanisa
limekuwa linapata kejeli za aina mbalimbali kutoka kwa watu hao na
kuwatuhumu kuwa maskofu walifikia maamuzi ya kuandika waraka huo
kutokana na sababu za kimaslahi kwa maana ya sadaka makanisani kupungua
jambo ambalo si la kweli.
“Kanisa
linasitikika sana, tunaposema jambo la kweli na jambo linalohusu maisha
ya Watanzania wote, halafu kunatokea watu chache ambao naweza kuwaita
wajinga wanakebehi na kusema eti kwa sababu sadaka zimepungua kanisani
sisi sadaka hazijapungua kwani wakristo wanajitoa sana na
hatujapungukiwa na kitu ila tunasema yale tunayoyaamini,” amesema.
Askofu
Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo
watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za
kujaribu kuuzima ukweli ulipo katika wataka huo na wao hawajali kuhusu
hilo bali watasimamia ukweli zaidi.
“Najua
tutaitwa majina mengi maaskofu na hizo ni jitihada za upotoshaji wa ule
ukweli ulipo katika waraka na tukumbuke hili si jambo la hivi hivi tu….
kwani kwa wakati mmoja mabaraza ya maaskofu wa makinsa makubwa mawili
nchini kukaa na kutoa waraka ambao una ujumbe ulioshabihiana si kitu cha
kawaida mimi nasema kuna kitu Mungu anataka kutuambia kupitia ujumbe
ule tutafakari hili kama taifa,” amesema.
Halima Mdee kufikishwa mahakamani Jumanne
Mbunge
wa Kawe, Halima Mdee, anatarajia kufikishwa mahakamani Jumanne Aprili
3, kuungana viongozi wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), akiwamo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, wanaoshtakiwa kwa
makosa manane yakiwamo uchochezi, kuhamasisha maandamano na uasi.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo
leo na kuongeza kuwa mbunge huyo amekiuka masharti yaliyomtaka kuripoti
kituo cha polisi pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho kabla
ya kufikishwa mahakamani.
Halima
alikamatwa leo Jumapili Aprili Mosi, saa tisa alfajiri katika Uwanja wa
Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), alipokuwa akirejea nchini
akitokea Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
Aidha,
alipoulizwa ni kwanini Halima amekamatwa wakati mawakili wake walikuwa
wakitoa taarifa zake, Mambosasa amesema: “hayo ni maneno tu, anafahamu
taratibu zikoje, anafahamau sheria zinasemaje kwa sababu wanatunga
wenyewe huko bungeni hilo si suala la kujadili na mimi, asubiri atajibu
hayo mahakamani.
Mambosasa
amesema hayo muda mchache baada ya Chadema kulitaka Jeshi la Polisi
kumpatia dhamana Mbunge ili aweze kuendelea na matibabu.
Mkurugenzi
wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje ya chama hicho, John Mrema
amesema licha ya kwamba Mbunge huyo kuwa mgonjwa ambaye hivi punde
ametoka hospitali, lakini pia dhamana ni haki yake na lawama zote
zitakuwa juu yao endapo afya ya mbunge huyo itatetereka.
“Hadi
mchana wa leo Aprili Mosi, Jeshi la Polisi limeendelea kumshikilia
Katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na hajapatiwa dhamana pamoja
na daktari wake kuwathibitishia polisi kuwa Mheshimiwa Halima ni
mgonjwa.
“Tunasikitishwa
na kulaani kitendo hiki cha polisi kuendelea, kumshikilia mgonjwa
ambaye alikuwa amelazwa hospitalini, , tumetuma mawakili daktari wake
lakini hawajafanikiwa mwisho, Jeshi la Polisi litawajibika kwa
Watanzania endapo afya ya Halima Mdee ikitetereka au ikidhoofu zaidi na
lawama zote zitakuwa juu yao,” amesema Mrema
Bavicha kula Pasaka mahabusu na kina Mbowe
Viongozi
wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) kesho watasherehekea Sikukuu ya
Pasaka kwa kuwatembelea viongozi wa chama hicho waliopo magerezani.
Mwenyekiti
wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi ataongoza msafara wa viongozi wa baraza
hilo watakaokwenda Segerea kumtembelea Mwenyekiti wa Chadema Taifa,
Freeman Mbowe na wenzake.
Amesema wamefikia uamuzi huo kwa lengo la kwenda kuwatia moyo na kuwa nao pamoja.
Amesema
viongozi wengine watakwenda Mbeya kwa ajili ya Mbunge wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.
"Tunataka kusherehekea nao Pasaka na kuwafahamisha kuwa chama kinaendelea, hatuwezi kurudishwa nyuma wala kutetereshwa,"amesema.
Ole Sosopi pia amewataka vijana wa baraza hilo kuwa tayari kupambana kwa ajili ya chama.
Amesema;
"Kuna mambo mengi yanaendelea na tunafahamu wazi kuna ajenda ya kutaka
kukifuta Chadema, sasa nawaambia hakuna namna chama hiki kitafutwa, tupo
imara na tunazidi kuimarika,'
“Vijana kazi yetu ni kulinda chama na kazi hiyo tutaifanya kwa nguvu zote bila woga, hatutaogopa kufa," amesema.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)