ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 15 Juni 2017

RIPOTI YA TWAWEZA:Yamgusa Rais, wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa.

Asilimia 71 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani. Kiwango hiki kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi Juni 2016.  Viwango vya kukubalika kwa Rais vinatofautiana katika makundi mbalimbali:
  • Asilimia 68 wenye umri chini ya miaka 30 wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 82 wenye umri zaidi ya miaka 50
  • Asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari au zaidi
  • Asilimia 75 ya wananchi masikini wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 66 ya wananchi matajiri
Viwango vya kukubalika kwa viongozi wengine navyo pia vimeshuka katika kipindi hicho hicho.
  • Wabunge:  Kukubalika kwa utendaji wa wabunge kumeshuka kutoka asilimia 79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).
  • Madiwani: Kukubalika kwa utendaji wa madiwani kumeshuka kutoka asilimia 74 (Juni 2016) hadi asilimia 59 (Aprili 2017).
  • Wenyeviti wa vijiji/mitaa: Kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa kumeshuka kutoka asilimia 78 (Juni 2016) hadi asilimia 66 (Aprili 2017).
Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania. 
Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. 
Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa mwezi Aprili mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya).
 
Kukubalika kwa vyama vya siasa kunatoa taswira mchanganyiko. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kuimarika, ikiwa ni kati ya asilimia 54 na asilimia 65 kati ya mwaka 2012 na 2017, Baada ya kushuka mwaka 2013 na 2014 ambapo kiwango cha kukubalika kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya 2012. 
Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017. Kukubalika kwa Chadema kumeshuka hadi asilimia 17 mwaka 2017 kutoka asilimia 32 mwaka 2013.
 
CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee (asilimia 80), ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake (asilimia 68) wanaikubali CCM kuliko wanaume (asilimia 58), maeneo ya vijijini (asilimia 66) kuliko maeneo ya mijini (asilimia 57), na wananchi masikini (asilimia 69) kuliko matajiri (asilimia 53). Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.
 
Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla unafuata mtiririko tofauti: ni mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.
 
Ndani ya kipindi cha miaka miwili tu, vipaumbele vya wananchi vimebadilika sana. Mwaka 2015, asilimia 34 ya wananchi walitaja umasikini na uchumi duni kama moja ya vipaumbele vyao vikubwa ikilinganishwa na asilimia 60 waliotaja masuala hayo mwaka 2017. 
Mwaka 2015, ni asilimia 9 waliotaja upungufu wa chakula au njaa kama kipaumbele chao ikilinganishwa na asilimia 57 mwaka 2017.
 
Katika kipindi hicho hicho, wasiwasi wa wananchi juu ya huduma za umma na rushwa umepungua.

Asilimia ya wananchi wanaotaja masuala yafuatayo kuwa miongoni mwa changamoto kuu tatu zinazoikabili nchi:
  • Afya: asilimia 40 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 59 mwaka 2015.
  • Elimu: asilimia 22 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2015.
  • Miundombinu: asilimia 21 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 32 mwaka 2015.
  • Huduma ya maji: asilimia 19 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 46 mwaka 2015.
  • Rushwa: asilimia 10 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 28 mwaka 2015.

Jumatano, 14 Juni 2017

Acacia watii maamuzi ya serikali, wakubali kulipa fedha wanazodaiwa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHFlmVKFOA1wi1QeAbaNeMmb0fAmIGUbzK5vkHhWhVDdw5d059X1WEBCrn4Qqhkn-0zhgHtsfMCFmgSklJjxlRcB4hczsPlPBfSPcEE84vU0QDqnPTha0qCl587yJqoRSIyXZM-uxyjKL0/s1600/maguu.jpgRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017

Jumanne, 13 Juni 2017

Ripoti ya Pili ya Madini ya Mchanga

.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOBGN9eDI6B81SSr7VG_DwNXOhRTZfcT_eWAUjVpNP4jF3_I98SaLABNMZJ0QB5SuE-3VnK4adsuVDMltJbhUrRo5FTdHq_Yv4LBwJAq6UX2T1Ew7pTotnxEHxu0v5hGTtPEyOAyxZ1Ass/s1600/1.jpgKamati ya wanasheria na wachumi ya kuchunguza mchanga wa madini iliteuliwa Aprili 10 ikiongozwa na Prof. Nehemiah Osoro.
2.Miongoni mwa hadidu za rejea ambazo kamati ilipewa ni kujua idadi ya makotena yaliyosafirishwa nje ya nchi tangu 1998.
3.Kamati pia ilitakiwa kuchunguza kama Tanzania inauwezo wa kutengeneza 'smelter' nchini, gharama zake na muda utakaotumika. 
4.Kamati ilitakiwa kuchunguza tofauti ya mapato ambayo Tanzania ilipata na ambayo ilitakiwa kuyapata tangu mwaka 1998. 
5.ACACIA inayojinasibu kama mmiliki wa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi haijawahi kuwasilisha nyaraka za umiliki huo.
6. Kamati imebani kwa mujibu wa nyaraka kuwa kampuni ya ACACIA PLC haikusajiliwa nchini 
7.Kamati imebaini kuwa wamiliki wa makampuni ya madini nchini wametenda makosa mbalimbali ya jinai. 
8.Kamati imeridhia baadhi ya watumishi wa serikali, makampuni ya usafirishaji na TMAA wameliingiza Taifa hasara kwa makusud. 
9.Makampuni ya Pangea na Bulyahulu yamepatikana na hatia ya kuliingizia Taifa hasara kwa kutokutoa taarifa sahihi juu ya uzito wa makinikia:. 
9.Idadi na uzito wa makontena ya mchanga ulionekana kuwa mkubwa kwenye meli tofauti na kwenye nyaraka za bandarini. 
10.Baadhi ya makampuni ya wakala wa meli ziliwasilisha nyaraka za uongo za usafirishaji wa madini kati ya 1998 na 2017. 
11.Makontena 30 ya futi 20 yenye makinikia yalionekana kwenye nyaraka yamesafirishwa, lakini ukweli yalisafirishwa 33. 
12.Kupitia hati ya usafirishaji wa makontena melini, idadi kubwa ya makontena yalikuwa yakisafirishwa bila kuorodheshwa. 
13.Migodi ya Bulyanhulu na Pangea imekuwa ikipata faida lakini faida halisi haikuwa ikionyeshwa. 
14.Kamati imebaini makontena 44,277 kwa kiwango cha chini yalisafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 na 2017. 
15.Viwango vya dhahabu kwa kila kontena ni 28kg, kwa miaka yote ni tani 1,240 kwa kiwango cha chini, thamani yake Tsh 108tril 
16.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 ni trilioni 132.56 kwa kiwango cha chini.
17.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 ni trilioni 229.9 kwa kiwango cha juu.

18.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58
19.Kodi ya Mapato ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 ni trilioni 55 katika usafirishaji wa makinikia. 

20.Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 ni bilioni 94 katika usafirishaji wa makinikia.

21.Mh Rais jumla ya Kodi tulizopoteza ni Sawa na makadirio ya bajeti ya serikali kwa kiwango cha Mwaka 2017/18 kwa miaka 2.

22.Taarifa ambazo zimekuwa sikiwasilishwa TMAA kuhusu uchenjuaji wa makinikia hazina ukweli wowote. 

23.Mh Rais kamati imepata mikataba ya mauzo ya uuzwaji Wa makinikia nje ya nchi kuwa serikali haihusiki kabisa.

24.Mikataba hiyo Mh Rais haina Masharti kuwa Serikali inapaswa kupewa taarifa ya uuzwaji wa Makinikia kutoka ktk migodi.

25.Mh Rais katika uchunguzi wetu Serikali ina hisa asilimia 15 ikauza 5 na kila mwaka kamishna au Waziri wa Fedha hupokea dola laki 1. 

26.Pangea Gold mine ina mikataba miwili ilisainiwa na Mh Daniel Yona baadaye Mh Nazir Karamagi serikali haina hisa Yoyote.

27.Mh Rais Mkataba wa North Mara ulisainiwa na Waziri Daniel Yona Mwaka 1999 baadaye Nazir Karamagi Mwaka 2017 

28.Mh Rais katika Mkataba wa Geita Gold Mine ulisainiwa na Mh Abdallah Kigoda na serikali haina Hisa hata moja. 

29.Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji wa muda wa leseni na maeneo uchimbaji kinyume na sheria.

30.Mh Rais kamati imebaini kuwa Mh William Ngeleja na Sospeter Muhongo walitoa mikataba mipya bila kufuata sheria za nchi

31.Mh Rais Mkataba wa North Mara ulisainiwa na Waziri Daniel Yona Mwaka 1999 baadaye Nazir Karamagi Mwaka 2007 

32.Mh Rais mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na makamishina wa madini Mh Andrew Chenge na Dalali kafumu walihusika ktk mikataba ya madini. 

33.Makampuni ya uchimbaji yakilipwa fedha haziwekwi kwenye mabenki ya ndani badala yake huwekwa kwenye mabenki ya nje.

34.Uwekaji wa fedha kwenye mabenki ya nje badala ya mabenki ya ndani, umechochea utoroshaji mkubwa wa fedha.

35. Makapuni mengi yamekuwa hayaajiri wazawa, na mgodi mmoja ulitaka kuleta walinzi kutoka nje ya nchi.

36.Hakuna mfumo uliowekwa na serikali wa kuhakikisha kunakuwa na ufuatiliaji wa ajira zinazotolewa katika migodi nchini.

37.Sheria ya madini inatoa uhuru wa madaraka kwa Waziri wa Madini katika kuingia kwenye mikataba ya madini.

38.Mh Rais Kamati inatoa mapendekezo kuwa mikataba yote ya madini ipelekwe bungeni kujadiliwa na kisha kupitishwa kwa maslahi ya Taifa.

39.Kamati imeona hakuna haja ya kupelekwa migogoro nje ya nchi,badala yake migogoro isikilizwe hapa nchini.

40.Kamati imeona kuwa kuna uwezo wa kujenga 'smelter' hapa nchini kwa kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha kama mikopo..

 41.Licha ya kuwapo taasisi nyingi zenye dhamana ya kusimamia sekta ya madini, Tanzania imekuwa ikipata hasara kila mara.

42.Tanzania imekuwa ikipata hasara bandarini kutokana na kutokuwa na wakala wa meli. 

Mapendekezo:
1.Kamati inapendekeza serikali kupitia msajili wa makampuni iichukulie hatua kampuni ya Acacia kwa kufanyakazi kinyume na sheria. 

2. Serikali izuie usafirishaji wa makinikia nje ya nchi, hadi hapo wadaiwa watakapolipa madeni yao. 

3.Serikali iwachukulie hatua waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Manaibu na watumishi wote waliohusika. 

4. Serikali ijenge smelter hapa nchini ili kuokoa fedha zinazopotea kutokana na usafirishaji wa makinikia. 

5. Serikali ichunguze mwenendo wa watumishi wa Mabaraza ya Kodi kwa kuchukua muda mrefu kutoa maamuzi ya mashauri ya kodi. 

6. Sheria iongeze kiwango cha adhabu kilichoanishwa katika ukiukwaji wa sheria ya madini nchini.

7. Sheria iweke kiwango maalumu cha hisa ambacho zitamilikiwa na serikali na kuiwezesha serikali kununua hisa. 

8.Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali ya Watanzania na yamewekwe chini ya ofisi ya rais. 

9. Mikataba ya madini isiwe ya siri ni lazima iridhiwe na bunge

10. Sheria iondoe mamlaka aliyonayo Waziri wa Madini na Kamishna wa Madini katika sekta ya madini. 

11. Serikali ifute au kubadili sheria ya kodi ya madini ili kuondoa vifungu ambavyo havina manufaa kwa mataifa. 

12. Serikali itoe elimu kwa watumishi wake kuhusu sekta ya madini. 

==>Rais Magufuli anazungumza.
1.Muda mwingine ni vigumu sana huwa uzungumze nini mara baada ya ripoti hii yenye kutia uchungu sana. 
2.Nisije kusahau nawapongeza kamati mmefanya kazi kubwa kwa ajili ya Watanzania wapo waliotaka kukatisha maisha yenu.

3.Nisije kusahau nawapongeza kamati mmefanya kazi kubwa kwa ajili ya Watanzania wapo waliotaka kukatisha maisha yenu. 

4.Ndugu zangu watanzania Mungu alitupenda katuweka katika nchi ya Tanzania akatupatia Maliasili nyingi. 

5.Nina Uhakika huko alipo shetani anatucheka nina imani shetani huyohuyo anatumia viongozi kuifanya Tanzania kuwa maskini. 

6.Wakati mwingine tunapewa mikopo kwa Masharti ya ajabu ajabu huku mali tunazo sisi wenyewe jamani.  

7.Kampuni inafanya biashara ya Trilioni of money lakini hata haijasajiliwa nchini mara ngapi tunawaumiza wamamchinga wasio na leseni. 

8.Mali ni yangu mimi nakulinda wewe unanitisha kuwa tutashitakiwa kwa kisingizio cha ajira tuko hapa kulinda maslahi ya watanzania  

9.Hawa watu muda mwingine hawana hata huruma wamechukua madini na mchanga wote huo lakini hata kodi hawakulipa.  

10.Watanzania hapa Mawaziri na Wataalamu wote mioyo yao haiwaruhusu hata kwenda kukagua smelter nje ya nchi. 

11.Makampuni ya kujenga smelter ya dhahabu hayaruhusiwi lakini chuma, Cement na Tiles mnaweza hili ni soko la ajabu. 

12.Tulikuwa tunashare ya 15% lakini mtu akaona apunguze hii aweke asilimia 5 baadaye akaenda kuiondoa yote hiyo. 

13.Yupo mpiga Kelele mmoja ambaye anapiga Kelele kila siku tulipomchunguza huko nyuma anapiga simu kwa Mwanyika anaomba data.  

14.Sio kwamba mimi sina Damu ila Mungu alifawanyanyua mkaona mimi ndiyo ninafaa siwezi kuwasaliti hata kidogo. 

15.Mtu kama Dkt Kafumu alikwenda kufanya forgery yupo daktari mmoja pale Muhimbili naye tulimshika hata hausiki alileta ukabila 

16.Wahusika wote waliotajwa ndani ya Ripoti hii mimi nimeyakubali mapendekezo haya yote ntayasapoti kwa asilimia 100. 

17.Waziri Kabudi uwe na timu ya wanasheria waaminifu, rekebisheni hizi sheria tuzipeleke bungeni zifanyiwe mabadiliko

18.Wakikiri na kuomba msamaha tutakubali kuwasajili lakini kwa sasa hakuna kuwasajili na hakuna mchanga kutoka nje

19.Wizara zote zinazohusika wawaite Acacia wawadai fedha zetu zote na wakiri walituibia. Wakikubali tutaendelea


20.Tunahitaji wawekezaji, lakini katika uwekezaji ambao utatunufaisha wote, na si wawekezaji wezi.

21.Kama mtu ametajwa kwenye ripoti na yuko hai, muite umhoji kwanini alifanya aliyoyafanya

22.Mwl. Nyerere alisubiri hadi wakati utakapofika ndio tuchimbe. Nina uhakika huko aliko akituangalia machozi yanatoka
 

 

Magazeti ya Leo jumanne ya tarehe 13/06/2017