ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 4 Septemba 2018

Msukuma Asema Lowassa Anampango wa Kurudi CCM

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma (CCM), amesema viongozi wengi wa vyama vya upinzani wanataka kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Musukuma ameyasema hayo jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani Kata Machame Uroki wilayani Hai, uliofanyika katika Viwanja vya Kurasinde na ambapo pia amesema ifikapo Septemba 10 mwaka huu, nguzo za umeme italetwa katika kata hiyo ili wananchi waondokane na tatizo la umeme huku akiwataka kumchagua mgombea udiwani wa jimbo hilo kupitia CCM, Robson Kimaro.

“Viongozi wengi wanaitaka CCM, sasa nawasihi wananchi mliopo katika vyama vya upinzani kujitafakari kama mko sehemu salama,” amesema.

Aidha, akizungumzia kuhusu umeme katika wilaya hiyo amesema: “Sisi tutakwenda kumwagiza waziri mwenye dhamana na sasa tunapozungumza Meneja wa Tanesco (Shirika la Umeme nchini), Mkoa wa Kilimanjaro amesema nguzo zipo tayari kwa hiyo ndani ya siku 10 tatizo lenu la umeme litakuwa limekwisha katika  vijiji hivyo viwili vya Kurasinde na Bwera, ninachokizungumza nina uhakika nacho kwa sababu nipo ndani ya chama chenye serikali na kama nazungumza uongo nifukuzwe bungeni.”

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbinga, Sixtus Mapunda amesema, Robson alikuwa Diwani mzuri na mwenye nia ya kuwatumikia wananchi lakini tatizo alikuwa katika chama kisichojali maendeleo ya wananchi.

“Wananchi wa Machame Uroki mnahitaji maendeleo na si maneno, Robson baada ya kutambua hilo na kutambua dhamira yake ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo alitambua hawezi kutimiza lengo hilo ndani ya Chadema na kuamua kujiunga ndani ya CCM ili kuwaletea maendeleo hivyo naombeni mumuunge mkono kwa kumpa kura za kishindo,” amesema Mapunda.

Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kuwa, katika maneno ya mkoa huo ambayo wananchi wamewachagua viongozi wa vyama vya upinzani maendeleo yake yamekuwa yakirudi nyuma na kuwataka wananchi kutorudia makosa.

Kwa upande wake, Mgombea Udiwani Robson Kimaro amesema, kata hiyo ina changamoto ya uchakavu wa majengo ya Shule ya Msingi Mkwasaringe hali ambayo ni hatarishi kutokana na nyufa katika kuta hali ambayo imesababisha wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la nne kutumia darasa moja kusoma kwa kupokezana ambapo ameahidi kutaitatua changamoto hiyo


Ijumaa, 20 Julai 2018

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Ziara Ya Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Korea

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Lee Nak-yon atafanya ziara ya kikazi nchini kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kuanzia tarehe 21 hadi 23 Julai 2018. Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Jamhuri ya Korea tangu nchi zetu mbili zianzishe mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1992. 

Madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kufungua zaidi fursa za ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi katika ngazi na sekta mbalimbali. Mhe. Waziri Mkuu Lee atafuatana na ujumbe mzito wa maafisa wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa. Ujumbe wa wafanyabiashara utakaoongozana na Mhe. Lee unatarajiwa kukutana na wenzao wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wafanyabiashara uliopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 23 Julai 2018. Mkutano wa kwanza ambao ulikuwa na mafanikio makubwa ulifanyika Seoul mwezi Februari 2018.

Mhe. Lee Nak-yon atawasili nchini saa kumi na mbili na nusu jioni (12:30) ya tarehe 21 Julai 2018 na atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku inayofuata, Waziri Mkuu Lee na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), watafanya mazungumzo rasmi jijini Dar es Salaam na baadaye watashuhudia uwekaji saini wa mkataba wa kuondoa hitaji la visa kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and official/service passport). Aidha, Mhe. Lee atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya kusalimiana.

Jamhuri ya Korea ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania ambapo kupitia  Shirika la Kimataifa la Maendeleo (KOICA) na Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (EDCF) yamekuwa yakitoa misaada na mikopo mingi ya masharti nafuu kwa Tanzania ikiwemo misaada ya fedha katika bajeti, ujenzi wa miundombinu ya jamii, mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wataalamu mbalimbali wa kujitolea, vifaa na mashine kwa ajili ya sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

Baadhi ya miradi ambayo imegharamiwa na Serikali ya Korea ni pamoja na Mradi wa kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Chanika, Mradi wa Mfumo wa Usajili wa Meli na Mabaharia kwa Njia ya Mtandao Zanzibar, Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Taaluma na Tiba (MUHAS) kampasi ya Mloganzila na ujenzi wa daraja katika mto Malagarasi.

Vile vile, Korea ni mshirika mkubwa katika kusaidia maendeleo ya Bara la Afrika ambapo hivi karibuni katika mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Africa (KOAFEC VI) uliofanyika mwezi Mei 2018, Busan, Korea ambapo Serikali ya Korea ilitangaza msaada wa Dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya Bara la Afrika kwa kipindi cha mwaka 2018/2020. Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika na msaada huo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 20


==

Jumanne, 3 Aprili 2018

HISTORY: FORM FOUR PAST PAPERS (NECTA) AVAILABLE HERE

The collection of History past papers of Tanzania National assessment for form four (4), view or download in this site through he following link. Find more past papers for other subjects and Share to others

MBOWE ANENA

Mwenyekiti wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na viongozi wengine sita wa CHADEMA na kusema kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi karibuni.

Mbowe amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.

"Leo mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa

"Kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe

==>Msikilize hapo chini