Na mwandishi wetu | , kilolo |
Picha:( kushoto) wanafunzi wakijisomea kulia: prof ndalichako akiapa kuwa W/ elimu.(maktaba yetu)
Utaratibu wa elimu bure unaofanywa na Serikali ambao umefanikiwa kulipa michango yote kwa wanafunzi wa shule za awali msingi na kidato cha kwanza mpaka cha sita, imeonekana kuanza kuvurugwa na walimu wa shule mbalimbali kwa kuanza kutumia mwanya huo kuwavuruga wanafunzi katika utoaji wa elimu bure.
Mwandishi wetu amefuatilia shule hizo zilizopo wilaya ya kilolo kubaini juu ya utekelezaji wa elimu bure amebaini mambo mbalimbali ambayo yameanza kufanywa na walimu na wakuu wa shule ambayo yanonesha kuwa yana mianya ya kuhujumu wanafunzi kupata elimu bure, haya yamejitokeza katika shule za sekondary zilizopo katika tarafa ya mazombe ambazo zimebuni mbinu mpya ya kurudisha watoto shuleni na kuwaacha bila kuwafundisha huku wakidai kwamba wanataka wanafunzi hawa wajisomee shuleni
Kwanini mwandishi wetu anahisi hili ni jipu?
Hili linaonekana ni jipu kwasababu wanafunzi wanarudishwa shuleni huku kukiwa hakuna mwalimu wakuweza kuwaangalia muda wote wanapokuwa shuleni hivo kuna uwezekano mkubwa kabisa kusababisha wanafunzi wengi kuanza kutumia mda huo kuanza kufanya mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa shule ikiwamo kufika shuleni na kucheza michezo ambayo haina tija, wanafunzi kutumia nafasi hiyo kujihusisha na mapenzi na hata wengine kuaanza kucheza kamali na hata kuharibu miundo mbinu ya shule
Vile hili limeonekana ni jibu kwasababu wanafunzi wanaporudishwa shuleni kwa kigezo cha kujisomea ilipaswa kuwa ni hiari na sio lazima lakini shule hizi zimefanya kurudi shuleni kuwa ni lazima hivo limeonesha nia ya dhati ya walimu kuwabana wototo hao ili wasipate mda wa ziada wa kujisomea nyumbani.
Pia suala la kurudisha wanafunzi shuleni limeonekana kukiuka waraka wa elimu uliotolewa na wizara ya elimu kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI ambayo imetambua mda wa kusoma kwa mwanafunzi wa kutwa na kuzuia walimu kutumia mianya yoyote ile kuhujumu elimu bure
pia inaonekana kabisa kuwepo na mvutano wa chini kwa chini baina ya utekelezaji wa elimu bure kwani kama shule hizi zinaona umuhimu wa wanafunzi kusoma hazikuwa na budi kujitolea kuwalinda watoto pale watakapokuwa wamerudi shuleni kujisomea na ikiwezekana walimu wakubali kupangiwa ratiba maalumu ya kujitolea kufundisha baada ya muda wa kazi
na pia kama ni nia njema kuhakikisha wanafunzi wanajisomea hakukuwa na budi kwa budi kwa utawala wa shule kulazimisha wanafunzi kurudia shuleni ila ingekuwa ni kwa hiari
Nini madhara ya hiki kinachofanywa na shule hizi za kilolo hasa tarafa ya mazombe na mji mdogo wa ilula?
Moja inasababisha wanafunzi kupoteza mda ambao wangeutumia vizuri wakiwa nyumbani kwao hasa tukizingatia wanafunzi wengi wanaishi mbali na makazi yao.
Mbili inawanyima wanafunzi uhuru wa kuchagua mazingira rafiki ya kujisomea.
Tatu, kuleta migogoro baina ya wazazi, walimu na wanafunzi hasa pale wanapo ondoka kwenda shule na kushindwa kusoma chochote kitu kinacholeta tafsiri mbaya ya uaminifu baina ya mwanafunzi, mzazi na walimu.
wanafunzi wanazungumziaje utaratibu huu ulioanzishwa na shule hizi?
Mwandishi wetu alipohojiana na baadhi ya wanafunzi kwa sharti la kutoandikwa majina yao walisema"hawa walimu si hatuwaelewi kwasababu wao wanasema turudie shuleni kwa lazima afu hawatufundisha sasa hapa ndo watasema tumekuja kusoma? maana hata nyumbani tunasehemu za kusomea na kila mwanafunzi hapa anautaratibu maalumu wa kujisomea mi nafikiri lengo lao ni kutukomesha tu na kutufanya tufeli ili wapate sababu ya kuongea"
Naye mwanafunzi mwingine alieonekana kukereka na utaratibu huu alisema" ivi we mwandishi ungekuwa mwalimu ungesema wanafunzi tufike shule kujisomea wakati unajua wanafunzi wenyewe ndo hawa tukifika shuleni kama hakuna mwalimu wengi wanaanza kucheza mpira na kutushawishi na sisi wengine tushindwe kusoma ebu hawa walimu waache mambo yao ya kushindana na serikali ya hapa kazi "
Na mwanafunzi mwingine alieonekana kufurahishwa na utaratibu wa kurudia lakini kukerwa na utaratibu uliowekwa alisema" kama huyo mkuu wa shule aliposema turudie lengo lake ni zuri lakini wanachokosea kuturudisha shule afu wao kubaki nyumbani huku wanajua sisi tunahitaji kusimamiwa ili kuepuka wanafunzi wengine kutuharibia tusisome kama hao unaowaona wanacheza nje ni vigumu mi kusoma ilihari wanafunzi wengine wanapiga kelele nje.
Na mwandishi wetu alipomtafutaWakuu wa shule hizi, ambao wameonekana kufanya utaratibu huu. wakuu wa shule hawa wameonekana kutoleta ushirikiano stahiki
Walimu nao walisemaje tulipohojiana na mwalimu mmoja alidai kuwa" mi mwenyewe nimesikia kuwa wanafunzi inabidi warudie kujisomea sasa sijui kuna nini ila si kama walimu mda wetu wa kazi mwisho ni saa tisa na nusu, ko kama tunarudia kutakuwa na extra time na itabidi tulipwe"
Wazazi wanasemaje? mwandishi wetu alipojaribu kuhojiana na baadhi ya wazazi walionesha kukerwa na kitendo cha wanafunzi wao kurudishwa shuleni ilihali hawasomi " mwandishi hawa walimu bwana hata si wenyewe tunashindwa kuwaelewa wanalazimisha watoto warudie shuleni eti kwa kigezo kwamba wakiwa nyumbani hawasomi ivi hii akili kweli maana wanafunzi wengine wanatoka sokoni wanaenda kusoma kiheka na wengine wanatoaka isele wanaenda kusoma nyalumbu au kiheka, sasa huoni kama wanawaumiza watoto wetu kwenda mara mbili kwa siku shuleni ilihali wakitembea umbali mrefu hawa wana lao jambo ngoja tusubiri ila utasikia wanasema sababu za kisiasa"
Mwandishi wetu anaendelea kuwatafuta wakuu wa shule husikaili waweze kutoa ufafanuzi wa suala hili lakini kama waandishi tumeona dhahili hili kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa mara moja.
Mkurugenzi, Maafisa wa elimu, pokeeni waandishi wetu tunaowatuma kwenu tumalizie kuaangazia "jicho la mwandishi wetu kutoka kilolo"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni