ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 14 Mei 2016

MAGAZETINI:#Azam yapata makocha Wahispania

KLABU ya soka ya Azam FC ya Dar es Salaam imepata makocha wawili kutoka klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania. Makocha hao Zebensul Hernandez Rodriguez ambaye atakuwa Kocha Mkuu na Jonas Garcia Luis kocha wa viungo, waliwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana na kupokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saada Kawemba.
Kwa mujibu wa Kawemba watafanya mazungumzo na makocha hao na kama watakubaliana watawachukua ili wainoe timu yao. Kocha wa sasa wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu wa ligi.
“Wamekuja kwa ajili ya mazungumzo, tukikubaliana tutawachukua kwa ajili ya timu yetu,” alisema Kawemba. Kwa upande wake Rodriguez alisema amefurahi kuja nchini kwani anaamini kuna vipaji vya soka kwa jinsi walivyomuona mchezaji Farid Mussa wa Azam ambaye anafanya majaribio katika timu yao.
Farid Mussa ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefuzu majaribio katika klabu hiyo iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania na kilichobaki ni mazungumzo baina ya Azam na klabu hiyo kuhusu mauzo ya mchezaji huyo.

Hakuna maoni: