ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 15 Mei 2016

MAGAZETINI:#Watumishi 10,870 wa sekta ya afya kuajiriwa

OFISI ya Rais, Utumishi na Utawala Bora imesema katika mwaka ujao wa fedha 2016/17 inatarajia kuajiri watumishi wa sekta ya afya 10,870 kwa ajili ya kupunguza pengo la uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.
Hayo yalisemwa bungeni Dodoma juzi na Waziri wa wizara hiyo, Angella Kairuki, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2016/17.
“Nimesikia katika michango mingi wabunge wamezungumzia sana tatizo la uhaba wa watumishi wa sekta ya afya. Waheshimiwa wabunge katika mwaka ujao wa fedha sekta ya afya wataajiriwa watumishi 10,870,” alisema Kairuki.
Alisema muda wowote kuanzia sasa ndani ya mwezi huu, vibali vya ajira hizo vitatoka na wizara ya afya, itaendelea kuwapangia watumishi sehemu zao za kazi. Kairuki alisema katika mgawanyo huo wa watumishi 10,870, watumishi 3,147 ni wa kada mbalimbali 10 zinazohusu masuala ya mbalimbali ya utabibu, wauguzi 3,985 na kada nyingine za mama cheza, wataalamu wa viungo na famasia.
Alisema katika kuangalia namna serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika utoaji wa ajira kwenye sekta afya, ndani ya miaka mitano serikali ilitoa vibali vya ajira 52,947 na kati ya vibali hivyo walioweza kuajiriwa ni wataalamu 38,047.
Kairuki alisema kati ya waajiriwa hao, ambao hawakuripoti ni 14,860 ; na asilimia 71.93 ndio walioweza kuripoti. “Ukiangalia takwimu za mwaka jana 2014/15 pamoja kwamba ikama zimejazwa na halmashauri zetu, ziko kada zaidi ya 12 zenye wataalamu 335 hazikuweza kupata watu kabisa, ukiangalia kada hizo hata mafunzo yake hapa nchini hayatolewi, kwa mfano wataalamu kutoka kada ya biomedical engineers na wengine wengi,” alisema.
Aidha alisema katika mwaka 2014/15, Serikali ilitoa kibali cha watumishi 8,345, lakini katika soko la ajira kulikuwa na ukosefu wa wataalamu katika soko hilo 4,467. Alitoa mfano wahitimu wa mwaka 2015/16 ni wataalamu 10,000 wakati Serikali imetoa kibali cha ajira cha wataalamu 10,870.
Alisema katika mwaka wa fedha 2010/11, Serikali katika sekta ya afya ilianza na watumishi 7,300, lakini katika mwaka ujao wa fedha idadi hiyo itaongezeka na kufikia 10,870. Kairuki alisema serikali itaangalia namna ya kuwapanga watumishi hao kwa kuzingatia maeneo

Hakuna maoni: