ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 28 Aprili 2016

Makatibu tawala wa mikoa 10 waapishwa


Imeandikwa na Anastazia Anyimike
RAIS John Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa wapya 10 walioteuliwa wiki hii tayari kuanza kazi. Makatibu hao wameapishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam sambamba na kula kiapo na kutia saini Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma walioufanya mbele ya Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Walioapishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Richard Kwitega (Arusha), Selestine Gesimba (Geita), Armatus Msole (Kagera), Aisha Amour (Kilimanjaro), Zuberi Samataba (Pwani), Albert Msovela (Shinyanga), Dk Angelina Lutambi (Singida), Jumanne Sagini (Simiyu), Dk Thea Ntara (Tabora) na Zena Saidi (Tanga).


Hata hivyo, Makatibu Tawala wa Mikoa 15 ambao jana hawakuapishwa ni wale ambao ni wa zamani, ambao baadhi yao wamehamishwa vituo vya kazi, ambao walishakula kiapo katika Awamu ya Nne ya Uongozi. Katibu Tawala wa Mkoa mpya wa Songwe atateuliwa baadaye.
Akizungumza mara baada ya kula kiapo hicho, Jaji mstaafu Kaganda alisema viongozi wengi wameshindwa kutekeleza wajibu wao kutokana na tatizo la mgongano wa maslahi. “Katibu Kiongozi (Balozi John Kijazi), ma-RAS hawa na wale wa zamani ni lazima wapewe semina hasa kwenye suala la mgongano wa maslahi ambalo ndilo linalowaponza.
Tulifanyie kazi hili ili tupunguze utumbuaji majipu,” alisema Kamishna huyo wa Maadili ya Viongozi wa Umma. Aidha, aliwataka kuhakikisha wanazingatia miiko ya uongozi na kuwawajibisha wengine kwa kuitumia miiko hiyo na kuwa endapo kiongozi atashindwa kufuata atashitakiwa kwenye Baraza la Maadili. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Kijazi aliwataka viongozi hao kuthamini heshima aliyowapa Rais ya kuwateua

Hakuna maoni: