Waziri mkuu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia bunge la bajeti
Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi Mei 2016, Serikali inatarajia kutoa ajira za walimu wapatao 40,000 ikijumuisha wa cheti, Stashahada na Shahada ili kukabiliana na upungufu wa walimu uliopo katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Zaidi ya shilingi bilioni 17 zitahitajika kwa ajili ya kulipa posho pamoja na nauli za walimu wapya watakaoajiriwa na kupelekwa katika halmashauri zote nchini.
Elimu ya Sekondari
Mheshimiwa Spika, OR - TAMISEMI inaendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango
28
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya pili (MMES II) ili kuimarisha Elimu ya Sekondari. Lengo la mpango huu ni kuinua ubora wa elimu. Aidha, utekelezaji wa mpango huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya shule 264 za awamu ya kwanza ambao umekamilika kwa asilimia 64. Serikali inaendelea kukamilishaujenzi na uboreshaji wa shule 264 za awamu ya kwanza na kuendelea na uboreshaji wa miundombinu katika shule nyingine 528
MWENDELELEZO WA HOTUBA YA WAZIRI MKUU
HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, MHESHIMIWA GEORGE BONIFACE SIMBACHAWENE (Mb) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17
Utangulizi
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo tukiwa na afya njema. Kipekee kabisa napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniamini na kuniteua niongoze Ofisi yake kwa upande wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Vile vile, kwa namna ya pekee, namshukuru Mheshimiwa Jasson Constantine Rweikiza (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na maelekezo wanayotupatia katika kutekeleza majukumu yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue nafasi hii, kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim (Mb), Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson Mwansasu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na viongozi wote kwa nyadhifa mbalimbali walizozipata kutokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Aidha, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Zanzibar. Nawapongeza pia Wabunge wote wa Bunge la kumi na moja kwa kushinda uchaguzi na kuwawakilisha wananchi katika chombo hiki muhimu cha kutunga sheria za nchi na kuisimamia Serikali. Nawapongeza pia, wote waliopata nafasi za kuteuliwa kushika nyadhifa walizonazo katika Serikali ya Awamu ya tano.
Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa likae, lipokee, lijadili na kupitisha Mpango wa Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.
Majukumu ya OR-TAMISEMI, MIKOA na Mamlaka za Serikali Za Mitaa.
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatekeleza majukumu yafuatayo:-
i. Kuratibu utekelezaji wa dhana ya Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii. Kuratibu na kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri katika kutekeleza wajibu wake;
iii. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Vijijini na Mkakati wake;
iv. Kusimamia Wakala wa Usafiri wa Haraka katika Jiji la Dar es Salaam;
v. Kuratibu usimamizi na uendeshaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vi. Kuratibu na kusimamia uendeshaji wa Afya ya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vii. Kusimamia utekelezaji wa miradi na programu zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; na
viii. Kusimamia utendaji kazi wa Taasisi zilizo chini ya OR TAMISEMI ambazo ni, Chuo cha Serikali za Mitaa(Hombolo), Shirika la Elimu Kibaha, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mikoa majukumu yao ni pamoja na:-
i. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za maendeleo katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
ii. Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zitekeleze majukumu yake kwa ufanisi;
iii. Kuhakikisha kwamba kunakuwepo amani na utulivu katika Mikoa;
iv. Kufuatilia utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo yake;

vi. Kusimamia uendeshaji wa Afya ya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
vii. Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.
Mheshimiwa Spika, utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa unaongozwa na majukumu ya msingi yafuatayo:-
i. Kuhakikisha kuwa kunakuwepo na amani na utulivu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
ii. Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora;
iii. Kuhakikisha kuwa Serikali za Mitaa zinatoa huduma za kuridhisha, kuaminika, kwa wakati muafaka na zenye ubora kwa wananchi kulingana na Sera na Mikakati ya kisekta;
iv. Kuhakikisha kuwa zinasimamia vema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusimamia matumizi ya fedha zinazopelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kupata thamani ya fedha;
v. Kuwaunganisha wadau wote wa maendeleo walioko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutumia vema rasilimali watu na fedha kwa manufaa ya jamii iliyopo katika Mamlaka hizo; na
vi. Kuhakikisha kwamba makundi maalum na masuala mtambuka yanazingatiwa katika utoaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo utunzaji wa mazingira, kudhibiti magonjwa ya mlipuko, UKIMWI na kuzuia na kupambana na rushwa.
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Kipindi cha Mwaka wa Fedha 2015/16
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2015/16, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliidhinishiwa shilingi 5,417,149,119,969.00 kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya
fedha hizi, shilingi 395,588,786,000.00 ni kwa ajili ya OR –TAMISEMI, Mikoa Shilingi 254,859,800,969.00 na shilingi 4,766,700,533,000.00 ni kwa ajili ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Maduhuli na Mapato ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ilikadiria kukusanya Shilingi 13,503,000.00. Hadi mwezi Machi, 2015 Ofisi imekusanya shilingi 1,650,000.00 sawa na asilimia 12 ya makadirio. Maduhuli hayo yanatokana na uuzaji wa nyaraka za zabuni. Maduhuli hayo yamekuwa kidogo kutokana na kutopatikana kwa fedha za maendeleo, hivyo ni zabuni chache zimeuzwa. Kwa upande wa Taasisi zilizo chini ya OR – TAMISEMI, zilikadiriwa kukusanya mapato ya shilingi 7,583,319,100.00. Hadi mwezi Machi, 2016 shilingi 5,092,545,190.00 zimekusanywa sawa na asilimia 67 ya makadirio.
Maduhuli ya Mikoa
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Mikoa ilikadiria kukusanya
shilingi 225,793,743 kama maduhuli. Hadi mwezi Desemba 2015, kiasi cha shilingi 225,050,999 zilikusanywa sawa na asilimia 99.7. Maduhuli ya Mikoa yanatokana na mishahara isiyolipwa, tozo la pango kwenye nyumba za Serikali na mauzo ya nyaraka za zabuni.
Mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Mamlaka za Serikali za Mitaa zilikadiria kukusanya shilingi 521,879,000,000.00 kama mapato. Hadi mwezi Februari, 2016 jumla ya shilingi 231,651,527,779.00 zilikuwa zimekusanywa sawa na asilimia 44. Kwa upande wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, makusanyo yanatokana na kodi na ushuru mbalimbali unaotozwa na Mamlaka hizo kutokana na vyanzo vya mapato vilivyokubaliwa. Ofisi yangu imeendelea kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya mapato, kwa kuboresha usimamizi na mifumo ya ukusanyaji mapato kwa kutumia TEHAMA na kubuni vyanzo vingine vya mapato pamoja na kuziba mianya ya ufujaji na uvujaji wa mapato.
Utawala bora na uwajibikaji
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa unazingatia misingi ya utawala bora, tarehe 23 Desemba, 2015 nilitoa Waraka namba 13 ambao unawaelekeza Wakuu wa Mikoa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuboresha utoaji wa huduma bora kwa Umma. Aidha, Waraka huo umetoa maelekezo kuhusu kuhimiza kuendelea na zoezi la kufanya usafi katika maeneo yao, pamoja na usimamizi wa zoezi la kutoa elimumsingi bila malipo. Maelekezo yote niliyotoa yanaendelea kutekelezwa vizuri.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatua mbalimbali zimechukuliwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uwajibikaji thabiti. Hatua hizo ni pamoja na kuboresha misingi na mifumo ya uwajibikaji na kuchukua hatua stahiki na kwa wakati kwa watumishi wote waliobainika kukiuka Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia utekelezaji wa majukumu yao.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2014/15, watumishi 78 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kijinai. Kati ya Watumishi hao, Wakurugenzi wa Halmashauriwatano (5) wamevuliwa madaraka na kupangiwa kazi nyingine na Wakurugenzi watatu (3) wamefunguliwa kesi mahakamani na kesi zao bado zinaendelea. Watumishi wengine ni Wakuu wa Idara na watumishi wa kawaida wa Halmashauri ambao wapo waliofukuzwa kazi, kuachishwa kazi na wengine kushtakiwa Mahakamani. Katika mwaka wa fedha 2015/16, hadi kufikia mwezi Machi, 2016 watumishi 90 wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na wengine kufikishwa Mahakamani. Kati ya watumishi hao, Wakurugenzi watatu (3) wamevuliwa madaraka na kupangiwa kazi nyingine, wakurugenzi watano (5) wamefikishwa Mahakamani, Wakurugenzi kumi (10) wamesimamishwa kazi na kupewa mashtaka ya nidhamu. Aidha, watumishi wengine wamechukuliwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi au kushushwa vyeo. Lengo la hatua hizi ni kuleta tija na kuweka nidhamu kazini na matumizi bora ya rasilimali na madaraka katika utumishi wa Umma.
Mabadiliko ya Muundo wa OR - TAMISEMI.
Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Februari, 2015, muundo mpya wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ulipitishwa ili kukidhi mabadiliko mbalimbali ya majukumu hususan katika eneo la usimamizi wa rasilimali
fedha ambapo Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Fedha (Inspectorate and Finance Tracking Division) ilianzishwa. Lengo la kuanzisha Idara hii ni kuimarisha usimamizi katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kufanya ukaguzi katika mifumo, uendeshaji, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala ya fedha.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2016 kaguzi maalum zilifanyika katika Manispaa ya Ilemela, Kigoma, Ilala, Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Magu na Uyui. Vile vile, ukaguzi wa kawaida ulifanyika katika Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora, Halmashauri za Igunga na Uvinza. Kaguzi hizi zimebaini mapungufu katika kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha, manunuzi na kutozingatiwa kwa kanuni na miongozo ya kisekta. Wote waliohusika na mapungufu hayo wamechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka zao za nidhamu. Aidha, ushauri umetolewa katika Halmashauri hizo ili kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa kutokana na kaguzi hizo. Vile vile, ufuatiliaji umefanyika katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na kubaini kwamba, kuna idadi ndogo ya wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na usimamizi hafifu wa matumizi ya Mfuko huo. Ushauri wa jinsi ya kuboresha uendeshaji na usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
umetolewa kwa lengo la kuongeza idadi ya wanachama na matumizi bora ya fedha zinazokusanywa.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 Ibara ya 148 (d) na (f), OR-TAMISEMI itaendelea kufanya ukaguzi wa ufanisi, kawaida, maalumu na ufuatiliaji wa kina katika Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa ili kuboresha utendaji kazi na hivyo kupata thamani ya fedha (value for money).
Madeni ya Watumishi
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuhakiki na kulipa madeni ya watumishi wakiwemo walimu na wasiokuwa walimu kadri yanavyojitokeza. Hadi mwezi Oktoba, 2015 jumla ya shilingi 20,125,578,770.05 zimelipwa kwa watumishi wa Umma. Serikali itaendelea kulipa madeni ya watumishi baada ya kuyahakiki. Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa inaelekezwa kuwa waangalifu ili kuzuia kuzalisha madeni mapya.
Uanzishwaji wa Maeneo Mapya ya Utawala
Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka wa fedha 2014/15 hadi mwezi Machi 2016, maeneo
ya utawala mbalimbali yameanzishwa ikiwa ni pamoja na mkoa mmoja (1) wa Songwe na Wilaya sita (6) ambazo ni Songwe (Songwe), Kigamboni (Dar es Salaam), Ubungo (Dar es Salaam), Malinyi (Morogoro), Tanganyika (Katavi) na Kibiti (Pwani). Aidha, Halmashauri za Wilaya za Malinyi (Morogoro), Chalinze (Pwani) na Itigi (Singida) na Halmashauri za Miji ya Ifakara (Morogoro), Bunda (Mara), Mbulu (Manyara), Kondoa (Dodoma), Newala (Mtwara) na Mbinga (Ruvuma) pia zilianzishwa katika kipindi hicho.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 30 Machi 2016, Tanzania Bara ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 181, Tarafa 562, Kata 3,963, Mitaa 4,037, Vijiji 12,545 na Vitongoji 64,677. Lengo la kuanzisha maeneo haya ya utawala ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo.
Kuimarisha Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa halmashauri zinakuwa na uwezo wa kifedha ambao utaziwezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuboresha makusanyo ya mapato ya ndani. Hatua hizo ni pamoja na kufunga na kutumia mifumo ya kieletroniki ya
ukusanyaji na usimamizi wa mapato. Mifumo hiyo imeunganishwa na mifumo ya malipo kama vile mabenki, M-pesa, Tigo Pesa na ‘Airtel Money’ ili kurahisisha ulipaji wa kodi.
Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Machi 2016, Halmashauri 138 sawa na asilimia 74 zimekamilisha ufungaji na zimeanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato na Halmashauri nyingine 48 sawa na asilimia 26 zipo katika hatua mbalimbali za ufungaji wa mifumo hii. Matumizi ya mifumo hii imepunguza mianya ya ufujaji na uvujaji wa mapato kwa kuwezesha usajili na utunzaji wa taarifa za walipa kodi, aina za kodi, kiasi kilicholipwa na kinachodaiwa na kuwezesha malipo kulipwa moja kwa moja benki. Katika kuhakikisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki inafanya kazi ipasavyo, Ofisi yangu kupitia Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma Awamu ya IV (PFRMP 1V), imezijengea uwezo halmashauri kwa kuziwezesha kufunga na kutumia mifumo ya mapato ijulikanayo kama Local Government Revenue Collection Information Management System (LGRCIS) na I- tax.
Mheshimiwa Spika, matumizi ya mifumo ya kielektroniki imeonesha faida na mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri. Kwa mfano, mapato ya ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha
yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 5.0 mwaka wa fedha 2012/13 hadi bilioni 10.5 mwaka wa fedha 2015/16 na mapato ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani yaliongezeka kutoka shilingi milioni 600 mwaka wa fedha 2013/13 hadi shilingi bilioni 2.6 mwaka wa fedha 2015/16. Hii inaonyesha wazi kwamba mifumo hii ina uwezo mkubwa wa kuzuia uvujaji na ufujaji wa mapato ya halmashauri.
Mheshimiwa Spika, sanjari na matumizi ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri, Serikali pia imezifanyia marekebisho Sheria za Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 na Sheria ya Kodi ya Majengo (The Urban Authorities (Rating) Cap 289) ili kuongeza wigo wa mapato ya halmashauri kwa kurejesha ushuru wa nyumba za kulala wageni na kuzipa mamlaka halmashauri za wilaya kutoza na kukusanya kodi ya majengo haya. Kwa upande wa uthamini, sheria hiyo imeruhusu kuanzishwa kwa njia ya Uthamini wa Mkupuo (Mass Valuation). Lengo la utaratibu huu ni kurahisisha zoezi la uthamini na kupunguza gharama.
Mheshimiwa Spika, kutokana na mafanikio haya, napenda kuchukua nafasi hii kuagiza kuwa ifikapo tarehe 01 Julai, 2016, halmashauri zote nchini ziwe zimefunga na
kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato yake ya ndani. Aidha, naziagiza halmashauri kwamba, mara baada ya mikataba ya sasa kwisha, ukusanyaji wa mapato kwa njia ya mawakala usitishwe na badala yake makusanyo yafanywe na maafisa wa halmashauri kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
Usimamizi wa Maendeleo ya Miji
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais - TAMISEMI inasimamia maendeleo mijini na vijijini. Lengo ni kuhakikisha kuwa ardhi iliyoko mijini na vijijini inaandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kufuata Sheria na Miongozo iliyopo. Uzoefu unaonesha kwamba miji inatoa mchango mkubwa kwenye ukuaji wa pato la Taifa.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba chimbuko la miji ni vijiji, kwa kipindi kirefu, msisitizo wa ki-sera wa uendelezaji wa ardhi ulielekezwa zaidi mijini. Ongezeko la idadi ya watu mara tatu kati ya Sensa ya mwaka 1967 (watu milioni 12.3) na 2012 (watu milioni 44.9) limefanya vijiji viongezeke. Katika kipindi hicho idadi ya wakazi mijini imeongezeka mara tano kutoka asilimia 5.7 hadi kufikia 29.1. Kuna sababu mbalimbali zinazofanya watu wengi
kuhamia mijini zikiwemo za kijamii na kiuchumi. Hii imesababisha kuwepo kwa migogoro mingi inayohusiana na uendelezaji wa ardhi na utoaji wa huduma mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa vijiji, katika mwaka wa fedha 2014/15, vijiji 1,550 sawa na asilimia 12.4 ya vijiji 12,545 vilivyopo nchini vilikuwa vimeandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya matumizi ya ardhi. Katika mwaka wa fedha 2015/16, vijiji 53 viliandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna majiji matano (5), manispaa ishirini na moja (21), miji ishirini na mbili (22) na miji midogo themanini na saba (87) inayotambulika kisheria. Katika mwaka wa fedha 2015/16, OR - TAMISEMI imetambua miji mia sita (600) inayochipukia kwenye maeneo mbalimbali nchini ambayo inahitaji kutambuliwa, kupangwa na kuendeshwa ipasavyo.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sera ya Maendeleo Vijijini sanjari na uendelezaji wa miji, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Miji ambayo iko kwenye hatua za mwisho kupata idhini ya mamlaka husika ili iweze kuanza kutekelezwa. Sera hii
itakuwa kiunganishi katika kuleta maendeleo sawia vijijini na mijini.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2015/16, OR-TAMISEMI ilitoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuandaa na kutekeleza mipango ya jumla ya uendelezaji miji, kwa kupima na kumilikisha viwanja vya makazi, biashara, viwanda na maeneo ya umma, pamoja na kuandaa mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi ya Vijiji.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa miji inaendelezwa kwa mpangilio, miji ishirini na sita (26) ipo katika hatua mbalimbali za kuandaa mipango ya jumla ya uendelezaji (General Planning Schemes - GPS). Miji hiyo, ni manispaa kumi na tano (15) za Dodoma, Kigoma - Ujiji, Mtwara - Mikindani, Moshi, Morogoro, Iringa, Sumbawanga, Songea, Lindi, Singida, Tabora, Mpanda, Shinyanga, Musoma na Bukoba na halmashauri sita (6) za miji ya Kibaha, Korogwe, Njombe, Babati, Bariadi na Geita. Aidha, majiji matano (5) ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tanga nayo yanaandaa mipango hiyo.
Mheshimiwa Spika, ili kurahisisha kazi na kuwa na kumbukumbu sahihi za Mamlaka za Serikali za Mitaa, OR-TAMISEMI imeanza
kutumia mfumo wa taarifa za kijiografia (Geographical Information System - GIS) katika kuandaa mipango ya jumla ya uendelezaji wa miji, mipango shirikishi ya matumizi ya ardhi ya vijiji na uhakiki wa mipaka ya vijiji, wilaya na mikoa. Mfumo huu umerahisisha uandaaji shirikishi wa mipango endelevu ya matumizi bora ya ardhi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, uthamini wa majengo 38,000 umefanyika chini ya mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) unaotekelezwa kwenye miji minane (8) ya kimkakati na halmashauri nyingine zipo kwenye hatua mbambali za kufanya uthamini wa majengo ndani ya maeneo yao ya utawala.
Mheshimiwa Spika, OR-TAMISEMI imeunda Baraza la Uthamini (Rating Valuation Tribunal) ambalo jukumu lake ni kusikiliza malalamiko ya uthamini wa majengo ili kukamilisha taratibu za kuanza kutoza kodi ya majengo kwa viwango vya uthamini. Hadi sasa, malalamiko 107 yamepokelewa na kusikilizwa katika majengo 38,000 yaliyothaminiwa.
Mwogozo wa Anuani za Makazi
Mheshimiwa Spika, OR - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeandaa mwongozo wa anuani za makazi utakaotumika kwenye utekelezaji wa mpango wa anuani za makazi na postikodi kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa utakaoanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2016/17. Utekelezaji wa mpango huo utawezesha wananchi wote nchini kuwa na anuani halisi ya makazi, biashara, kumbukumbu za vizazi na vifo na ulipaji kodi. Aidha, anwani hizi zitarahisisha huduma za zimamoto, magari ya wagonjwa, usambazaji wa huduma muhimu (umeme na maji), ulipaji kodi na uzuiaji wa matendo ya uhalifu.
Mfuko wa Barabara
Mheshimiwa Spika, kazi zinazofanywa na mfuko huo ni kuratibu, kuandaa mipango, ufuatiliaji, kutoa miongozo, msaada wa kiufundi na kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara na madaraja. Mamlaka za Serikali za Mitaa zina mtandao wa barabara wenye urefu wa km. 108,946. Hali ya barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa, imeendelea kuwa bora. Kwa sasa barabara zilizo katika hali nzuri na ya kuridhisha ni km 61,798 sawa na asilimia 57, barabara za lami ni km 1,325 sawa na asilimia 1.2 na barabara za
changarawe ni km 22, 089 sawa na asilimia 20.3.
Mheshimiwa Spika, mikakati iliyopo ni kuziimarisha barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa ili barabara zilizo katika hali nzuri na ya kuridhisha zibaki kuwa katika hali nzuri. Vilevile kuendelea kuinua hadhi ya barabara za mijini kuwa za lami kupitia fedha za Mfuko wa Barabara, Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID), Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Serikali ilitenga shilingi bilioni 257.75 kwa ajili ya shughuli za matengenezo ya barabara. Hadi mwezi Machi 2016, jumla ya shilingi bilioni 137.643 zimepokelewa na kutumika kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kawaida (routine Mainatanance), matengenezo ya muda maalum (periodic maintenance) na matengenezo ya maeneo korofi (spot improvement) kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Spika, OR-TAMISEMI inatekeleza mradi wa kuboresha barabara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nne (4) za Iringa, Mufindi, Songea na Mbinga kwa fedha kutoka Jumuiya ya Ulaya. Barabara zenye urefu wa km. 88
zinafanyiwa matengenezo kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 85.696. Utekelezaji umekwishaanza na upo katika hatua mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza programu ya kuondoa vikwazo vya upitikaji wa barabara (roads bottleneck removal) katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID). Gharama za mradi kwa mpango huo ni shilingi bilioni 25.978. Utekelezaji wa mradi huu uko katika hatua mbalimbali na kiasi cha shilingi bilioni 22.139 kimeshalipwa hadi Machi 2016.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Serikali kwa kushirikiana na USAID imetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe ambapo km. 178.4 zimetengenezwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nne (4) za Kongwa, Morogoro, Kiteto na Kilombero. Hadi Machi 2016, Mamlaka za Serikali za Mitaa zilipokea kiasi cha shilingi bilioni 8.74. Lengo la mradi ni kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani kupelekwa kwenye masoko.
Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, OR - TAMISEMI imeendelea kuratibu
na kutoa utaalam wa kiufundi kwenye miundombinu na mifumo ya TEHAMA ngazi ya OR – TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri kwa kuwajengea uwezo watumishi wa ki-TEHAMA; kufunga vifaa vya mawasiliano kwa njia ya luninga na uimarishwaji wa kituo cha TEHAMA (data center); kusimamia mifumo ya udhibiti na matumizi ya fedha (Epicor), kufunga Mfumo wa Makusanyo wa Kodi na Tozo, (Local Government Revenue Collection Information System – ”LGRCIS”), na kuwezesha ngazi mbalimbali kutumia takwimu katika kufanya maamuzi.
Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2016, Mamlaka za Serikali za Mitaa 133 zimekuwa zikiendelea kutumia mfumo wa Epicor Toleo la 9.05 bila matatizo. Malipo yote kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa yanafanyika kwa utaratibu wa akaunti 9 kama ilivyoelekezwa. Kwa kutumia mifumo hiyo, halmashauri zimeweza kutekeleza bajeti kwa kufuata taratibu na miongozo iliyotelewa na Wizara ya Fedha. Aidha, taarifa za mapato na matumizi za kila mwezi zinapatika kutoka kwenye mfumo.
Usimamizi wa Elimu
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inasimamia na
kuratibu uandikishaji wa wanafunzi katika elimumsingi na kidato cha tano, kuajiri walimu, kutoa elimu kwa watu wazima na vijana nje ya mfumo rasmi wa shule, kuongeza miundombinu ya shule na kutoa mafunzo kwa watendaji katika ngazi mbalimbali.
Elimu ya Awali na Msingi
Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na mafanikio makubwa kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi Awamu ya I (MMEM I) na ya II ambao kwa sasa utekelezaji wake uko katika Awamu ya III. Ili kuhakikisha kuwa elimu ya awali inatiliwa mkazo, jumla ya shule 14,946 zina madarasa ya Elimu ya Awali kati ya shule 16,014 za msingi sawa na asilimia 93.33 ya shule shule zote za msingi zilizopo. Hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali imeongezeka kufikia wanafunzi 971,717 (Wavulana 480,053 na Wasichana 491,663) mwaka 2016 kutoka wanafunzi 877,489 (Wavulana 436, 778 na Wasichana 440, 711) mwaka 2015.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Elimu ya Msingi, OR-TAMISEMI imeendelea na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi Awamu ya Tatu (MMEM III) kwa lengo la kuimarisha elimu ya

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni