Elimu Bora ni ile inayozingatia masuala yafuatayo;
Hali ya WanafunziJe, wako tayari na wanaweza kushiriki katika elimu yao? Je, wanapata ushirikiano kutoka kwenye familia na jamii zao?
Mazingira ya Kujifunzia
Je, ni salama kwa watoto wote bila kujali jinsia, imani na ulemavu? Je, vifaa kama vile madawati, vyoo na vitabu vinatosheleza mahitaji yote?
Mambo yanayofundishwa Darasani
Ni aina ipi ya ujuzi ambao Mitaala inatilia mkazo? Je, maudhui yake yanaendana na mahitaji ya jamii? Je, yanakuza uelewano, umoja, amani na haki za binadamu?
Walimu na Ufundishaji
Je, kuna walimu wa kutosha na wako tayari kufundisha? Je, ufundishaji unamjali mwanafunzi, na mahuasiano kati ya wanafunzi na mwalimu darasani yakoje?
Matokeo ya Elimu
Wahitimu wana aina gani ya maarifa, ujuzi na mtazamo? Na wanayatumiaje katika maisha yao ndani ya jamii?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni