ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 2 Aprili 2016

MAKALA YA LEO: JE MISAADA INAYOTOLEWA NA CAMFED INA TIJA?


kuna mashirika mbalimbali ambayo yameamua kwa namna moja kusaidia jitihada za elimu hasa kwa wafunzi wa kike katika shule za misingi lakini leo tunajiuliza je misaada inayotolewa ina tija kwa wanafunzi wenyewe?
au ndo inasaidia kuwafaidisha baadhi ya wadau waliopo katika mashirika hayo kama wakurugenzi wa mashirika, walimu na viongozi mbalimbali wa shule?
Kupitia maswali haya ndipo tulipoamua kutuma watafiti wetu katika shule mbalimbali hasa katika shule za sekondary za wilaya ya kilolo na kubaini uwepo wa madudu makubwa hasa kwa walimu wanaohusika na utoaji wa pesa mbalimbali kwa wanafunzi waliofadhiliwa na mradi huu wa CAMFED;
- Pesa nyingi zinazotolewa na wafadhili zimebainika kuishia kwa walimu walezi na kile kidogo kinachobaki ndicho wanafunzi hudanganywa kwa kununuliwa daftali au kupewa vifaa vya kujifunzia wafadhiliwa katika mradi huu kutoka shule fulani walisema" ni kwel CAMFED ina tufadhili kwa kutulipia ada na mahitaji mbalimbali ila hapa shuleni kwenu anaefaidi sana ni mwalimu wetu maana mara nyingine huwa wanatulazimisha tusaini hela elfu 80,000/= afu si tunapewa elfu thelathini (30,000/=) tukiuliza wanasema wanakata hela kwaajili ya matumizi ya shule".
mwandishi wetu hakuishia hapo alijaribu kuwadodosa baadhi ya walimu wanaohusika na mradi huo ambao walishindwa kabisa kujieleza na kutoa ushirikiano kwa kudai hayo ni mambo ya kitaasisi" haya ni mambo ya kitasisi sisi kama shule tuna utaratibu wetu wa kutoa pesa ambao humwekea akiba mwanafunzi" alisema mwalimu.

vile vile CAMFED hutoa misaada mbalimbali ya vitabu vya kujifunzia kwa wanafunzi ambavyo mara nyingi hufanya wakuu wa shule watumie vitabu hivyo kana kwamba wametumia bajeti ya shule

JE MISAADA HII INAMANUFAA KWA JAMII HUSIKA TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI :misaelkikoti.blogspot.com

Hiyo ni baadhi ya vitabu vilivotolewa na CAMFED kwa shule mbalimbali wilaya ya kilolo
 

 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akizungumza na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari zilizoko katika wilaya ya kilolo baada ya kukabidhi vitabu katika shule hizo. Kushoto kwake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ilula
Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akionyesha moja ya vitabu ambavyo amekibadhi kwa shule 22 za wilaya ya Kilolo halfa zilizofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ilula.  Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akimkabidhi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga moja ya mfano wa vitabu walivyokabidhi katika shule za sekondari wilaya ya Njombe.  Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilula.
Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi mwenye nguo ya njano akiwa na walimu wa shule za sekondari zilizopatiwa msaada wa vitabu kutoka shirika la CAMFED.(Picha zote na Denis Mlowe)
 Baadhi ya Maboksi ya Vitabu yaliyokabidhiwa kwa shule 22 zilizoko wilaya ya kilolo.

Na Denis Mlowe,Ilula
Katika kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinakua,shirika lisilo la Kiserikali la Campaign for Female Education (CAMFED)  chini  ya mpango wake kuwasomesha watoto wa kike kilitoa misaada ya vitabu 54,935 kwa shule 22 za sekondari zilizoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa vyenye thamani ya shilingi milioni 55.
Alipoongea  wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Ilula mwishoni mwa mwaka juzi mgeni rasmi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga alilishukuru shirika hilo kwa msaada huo kwa kuweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa vijijini.
 “Tumefurahi sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za hapa zina  changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya sayansi na kulifanya somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi sasa kutokana na msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu kutokana na uwingi wa vitabu wenyewe kwa shule zilizofaidika na msaada huo” alisema Kulanga
Aliwataka walimu na wanafunzi  wavitumie vitabu hivi vizuri kwa kuvitunza kwa lengo la kutumika kwa muda mrefu wakati wa masomo yao na kuamini kwamba vitabu vivyo vitaleta ufanisi  katika kukuza uelewa wa mwanafunzi katika matumizi sahihi ya lugha ya kiingereza.
Aidha alisema vitabu hivyo vitumike kwa wanafunzi wote kwa wa shule husika na kuwaasa wanafunzi wa shule zilizofaidika na msaada huo kuacha tabia mbaya ya kuuza vitabu na kuwataka walimu wa shule hizo kufatilia kwa makini wanafunzi wote watakaopatiwa vitabu hivyo.
Naye Mwalimu mkuu aliekuwa  wa sekondari ya Irole Laurence Maluka alipongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari 22 zilizofaidika na msaada huo wa vitabu alisema msaada huo wa vitabu utaweza kuwa saidia wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu hadi kwenda chuo kikuu,kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa katika shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi  5 lakini kwa sasa ni vitabu 5 kwa mwanafunzi mmoja.
“Ni jambo la kulishukuru sana shirika la CAMFED kwa msaada huu utapunguza zaidi, kwa kweli huu ni msaada mkubwa katika kuboresha taaluma na kuinua ufaulu hivyo tunaomba program hii ya shule zetu iendelee ili kuwafikiwa wanafunzi wengi zaidi katika wilaya ya Kilolo” alisema Maluka
Kwa upande wake Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi amewataka wanafunzi wa sekondari zote wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuongeza uwezo wa kujisomea ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada unatolewa na shirika hilo.
Alisema  vitabu hivi vitunzwe ili viweze kuwafaidisha wanafunzi wengi kwa kuwa  vitaleta faida kwa wanafunzi wengi zaidi katika kujisomea na kuwataka walimu wakuu wawapatie wanafunzi kila mmoja vitabu vitano na kwenda navyo nyumbani hadi amalizapo elimu ya sekodari na kuweza kuvirudisha. Alizitaja shule zilizofaidika na msaada huo ni shule ya sekondari Ilula, Nyalumbu, Mazombe, Irole,Lundamatwe, Selebu, Ngangwe, Uhambingeto, Lukosi, Mlafi Na Ndekwa.
Shule nyingine ni shule za za sekondari za Mtitu, Kilolo, Lulanzi,Ukwega, Udzungwa, Dabaga, Kitowo, Mawambala, Masisiwe, Madege na Makwema.

Hakuna maoni: