ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 26 Aprili 2016

Vyama vyakacha kuwasilisha hesabu NI CUF tu waliowasilisha

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 iliyotolewa jana mjini hapa inaonesha kuwa kati ya vyama 22 vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja pekee ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa ajili ya ukaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Profesa Mussa Asaad alitaja Chama cha Wananchi (CUF) , ndicho kimewasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari mwaka 2015 hadi Juni mwaka huo.
Alisema vyama vingine 21 vimeshindwa kufanya hivyo hali ambayo amemshauri Msajili wa vyama hivyo kufuatilia jambo hilo. “Ripoti hii inabainisha kwamba vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni 22, lakini hadi Juni mwaka 2015, vyama vilivyowasilisha hesabu zao kwa ukaguzi ni chama kimoja tu cha CUF, sasa hivi vingine vimekiuka sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992”, alisema Profesa Asaad.
Akizungumzia udhaifu mwingine ambao umebainika katika ripoti hiyo Profesa Asaad aliweka hadharani Balozi mbalimbali za Tanzania nje, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Hakuna maoni: