WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.
Profesa
Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais, Tamisemi,
Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa shule
zilizoungua moto.
Alisema
ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya
mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.
“Bado
siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe wafanye
mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara inaangalia
ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa
hatua,” alisema.
Alisema
pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana
yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga
kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.
“Nilipokuwa
Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo kuwa mabaya
lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,” alisema.
Waziri
Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu
watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za
serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja
ajipange.
Aidha
alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na
hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika
mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za
serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya
Arusha.
“Mpaka
namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa ndio
mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano tuachie
sekta binafsi,” alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni