Juzi, jeshi hilo lilitoa onyo
kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare
zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama nchini na kwamba
atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Sheria ya
Kanuni za Makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002,
kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za
majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha kuwa ni kosa kisheria kwa mtu
yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa
mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali
kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kaimu Kamanda wa
Kanda hiyo, Hezron Gyimbi alisema wasanii hao walikamatwa juzi saa 10
jioni baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii wakiwa
wamevalia sare hizo kwenye sherehe ya harusi ya Emmanuel Mgaya maarufu
‘Masanja’.
Gyimbi aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Lucas Lazaro
(Joti), Alex John (McRegan) na Isaya Gidion (Wakuvanga) na Sekioni David
(Seki) ambaye ni meneja wao.
Alisema sare walizokutwa nazo watuhumiwa
hao ni za kazi za kawaida za jeshi la polisi hilo ikiwamo kofia,
filimbi, shati, suruali, cheo na mkanda.
“Tunaendelea kuwachunguza zaidi
kama wana vitu vingine vya jeshi la polisi na tunataka kujua kuwa sare
hizi wamepa- ta kibali kwa nani na uhalali wa kuwa nazo,” alisema
Gyimbi.
Alisema jeshi hilo linaendelea kumtafuta Masanja ili kujibu
tuhuma zinazomkabili. Kaimu kamanda huyo alisema watuhumiwa hao
walihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kuanzia juzi saa 10 jioni hadi
jana jioni huku na dhamana zao zilikuwa wazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni