CHADEMA
inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni
likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha
Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.
Tunaomba
umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na
waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni
UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.
Kupitia
taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na
mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki,
kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .
Msisitizo
unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia
utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi
yanaendelea nchi nzima.
Imetolewa na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni