Msafara
wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama
kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba
unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea
mikoa hiyo.
Lowassa
ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake mkoani
Mbeya tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo
yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake mkoani Songwe wakati leo
asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.
Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.
Katibu
wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’,
Frank Mwaisumbe alisema kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa
1.00 jioni akiwa Tunduma wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa kwa njia ya simu
alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara
kwa sababu mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni