ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 25 Mei 2015

Nini tatizo la Migomo vyuo vikuu-

 Na mwandishi wetu  kazinde

 


Mara kadhaa matatizo haya ya wanafunzi kucheleweshewa fedha zao yamekuwa yakiibuka na imekuwa ni kawaida kwa Serikali kutumia vyombo vyake vya dola kuwatuliza, huku baadhi wakikamatwa na kufunguliwa kesi au kuachiwa kwa tuhuma za kukiuka sheria wakati wa kudai haki zao.
Hata hivyo, matatizo yanapoisha na jitihada za kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo yao huishia hapo hapo hadi tatizo jingine linapozuka. Kibaya zaidi ni pale Jeshi la Polisi linalolazimishwa kutumia nguvu za ziada katika kudhibiti wanafunzi na kusababisha baadhi kujeruhiwa, kupotezewa muda zaidi wa masomo na hata kujenga chuki dhidi ya Serikali yao.

Mwanachuo mmoja wa chuo kikuu MKWAWA alikuwa na majibu haya alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio EBON FM Iringa
mi nafikiri wanafunzi wengi wanagoma kwasababu madai yao yanashindwa kutatuliwa kwa wakati sitahili mfano wanafunzi wanapodai fedha za kujikimu lakini sababu zinazotolewa zinakuwa hazina msingi ndani yake  na hii mara nyingi inatokana na baadhi ya viongozi waliokabidhiwa dhamana katika idara husika kushindwa kufuatilia fedha kwa wakati na wengine kushindwa kuwajibika

NINI SULUHU YA TATIZO HILO
Kombe Godwin anasema, hatuna budi kubadili mfumo mzima wa watu wasio wajibika ambao wanafanya kazi kwa mazoea na njia pekee ni kuimarisha mifumo ya kiutendaji  kwa kuondoa mfomo uliopo sasa na suala la kutumia nguvu Kuzuia maandamano hakutatui matatizo ya wanafunzi na kutumia nguvu za ziada kudhibiti wanafunzi wanaogoma hakutatui matatizo yao. Kinachotakiwa ni Serikali kujipanga kuhakikisha matatizo hayo hayaibuki na kusababisha wanafunzi watumie haki yao ya kugoma au kuandamana.

JE JITIHADA ZINACHUKULIWA
Inashangaza kuona kwamba hadi leo aliyechelewesha fedha hizo ameachwa bila ya hata kutingishwa wakati waliogoma hadi kufanya fujo kutokana na kucheleweshwa kwa fedha hizo wamesimamishwa masomo, kupigwa na hata kufunguliwa mashtaka. Kwa utamaduni huu nchi itakwenda kweli

JE WANACHUO NAO WAFANYEJE KUDAI HAKI
Pamoja na hayo, wanafunzi pia wanatakiwa waanike matatizo yao kwa njia ambayo haitaharibu miundombinu ambayo wanaitumia kwenye masomo na ambayo itatumiwa na vizazi kadhaa vijavyo. Kufanya fujo na uharibifu ni kutowajibika pia kwa nchi yao na vizazi vinavyowafuata

Hakuna maoni: