KOCHA Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema anashukuru kumaliza ligi katika nafasi ya tatu na sasa anasubiri hatima yake.
Simba ilimaliza ligi juzi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kumaliza ya tatu ikiwa na pointi 47.
Kopunovic alianza kuiongoza Simba mwishoni mwa raundi ya kwanza akichukua mikoba ya Patrick Phiri aliyetupiwa virago baada ya timu kutopata matokeo mazuri.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kopunovic alisema ligi ilikuwa na changamoto nyingi na kumaliza nafasi ya tatu ni jambo la kushukuru.
“Halikuwa lengo letu, wote tulitaka kutwaa nafasi kubwa zaidi, lakini ligi ilikuwa na changamoto nyingi, nitakabidhi ripoti yangu kwa uongozi, hapo ndipo utajua hatima yangu,” alisema kocha huyo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba.
Akilizungumzia hilo, msemaji wa Simba Haji Manara alisema wanachokisubiri ni kuona ripoti ya kocha huyo kabla ya kufanya uamuzi mwingine.
“Watu wana papara ya kutaka kujua nini kitafuata, tumeshiriki ligi kama timu nyingine na yaliyotokea yametokea, kiutaratibu tunasubiri ripoti ya kocha ndipo mambo mengine yafuate kama kusajili ama la,” alisema.
“Tunataka tuwe na uhakika wa nini tunataka kufanya, kama mabadiliko ni yapi, yote hayo tunayafanya kwa muongozo wa ripoti ya kocha,” alisema Manara.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema, Simba imepania kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kumaliza kwenye nafasi zitakazowawezesha kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa mwaka wa nne sasa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni