KAMPENI ZA UCHAGUZI KUWANIA UONGOZI KATIKA SERIKALI YA WANAFUNZI ZAENDELEA KWA MBWEMBWE
Serikali ya wanafunzi ya Chuo
Kikuu cha Mkwawa (DARUSO-MUCE) imemaliza muda wake na hivyo iko katika mchakato
wa kutafuta Rais mpya wa serikali hiyo pamoja na wabunge watakaongoza
serikali hiyo kwa kipindi cha 2015/16 Chuoni hapo.
Aidha kampeni za mgombea Urais
ndugu BAKARI, IBRAHIMU zimeonekana kuwawavutia wanafunzi wengi kwani
amekuwa akitembelea wapiga kura wake huku akiwa ameandamana na wafuasi
wake ambao wamekuwa wakimlinda kila anapokwenda. Aidha mgombea huyo Bw. BAKARI, IBRAHIMU ndie ambae anaonekana ni mwenye asilimia kubwa ya kuweza
kushinda katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki lijalo chuoni hapo. Wagembea wengine ni; MSUYA, FAROUK na Bw MABULA
WAGOMBEA URAIS DARUSO MUCE 2015/2016.....................
Na kwa upande wa makamu wa rais wagombea wawili wamejitokeza akiwamo dada ISSASSI SUZANI na KIBONA FAUSTA katika nafasi hii ushindani unaonekana kuwa ni mkubwa sana kwani wote wana watu weng wanaowapigania ili kupata nafasi hiyo
WAGOMBEA WA NAFASI YA MAKAMU WA RAIS DARUSO-MUCE 2015/2016
Mgombea wa nafasi ya Rais Bwana BAKARI, IBRAHIMU sera
zake kwa wapiga kura (hawapo pichani) ambapo alisema katika uongozi wake
ataanza kushughulikia mikopo kwa wanafunzi wa MUCE.
Pia amesema kama atapewa nafasi hiyo
atakuwa na utaratibu wa kuwakutanisha wanafunzi wa MUCE kuanzia mwaka wa
kwanza mpaka wa tatu na wataalumu waliopo katika fani zao, lengo likiwa
ni kuwaongezea uzoefu zaidi na kujua changamoto ya kazi za kitaaluma chuoni hapo.
Aidha aliongeza kuwa atahakikisha usiri wa matokeo utaboreshwa chuoni hapo, huku akimwaga ahadi ya hakuna tatizo ambalo hawezi kulishughurikia akiwa rais na hii ilikuja baada ya mheshimiwa kitako kumuuliza mgombea matatizo gani manne(4) hawezi kuwasaidia wanachuo akiwa madarakani.
Wanafunzi hao wameonekana wana ukomavu mkubwa wa kisiasa kwani wanasikiliza kwa makini sera za wagombea na kuuliza maswali mazuri.
Cha kufurahisha ni kelele za filimbi na mayowe ambayo yametwala kila kona huku wagombea wakishangiliwa na mashabiki wao.
Nafasi
zinazowaniwa katika Uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Rais, Makamu wa
Rais, pamoja na wawakilishi wa Vitivo (wabunge) na wawakilishi wa
Maeneo (wabunge wa makazi) ambao wote watapigiwa kura.
Wagombea
mbalimbali wamekuwa wakipita hapa na pale ikiwa ni pamoja na kubandika
picha zao katika kuta ikiwa ni sehemu ya kutafuta kura.
Kwa upande wa MSUYA naye amenadi sera sake moja ya mipango yake ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wanafunzi likiwemo tatizo la maji na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara, huku akiwasii wanafunzi kuangalia hali ya chou sasa kwamba kinahitaji mtu makini anayejua matatizo ya wanachuo wote na kuwatumikia.
KWA UPANDE WA MAKAMU WA RAIS SERA ZAO IMEONEKANA KWENDA SAMBAMBA NA MARAIS lengo kubwa ni kuboresha taaluma na mazingira y chuoni hapo.
Kwa upande wake Rais
anayemaliza muda wake Bwana AGUSTINO ALFA ameishukuru tume ya uchaguzi
kwa mchakato mzima na anafurahi kumaliza muda wake
na kuwataka watakaopata nafasi za kuongoza wazingatie sheria, demokrasia
na upendo ili kuleta mshikamano katika chuo, ili wanaoongozwa wajisikie
kuwa na amani kuwepo chuoni hapo badala ya kutatua migogoro isiyokuwa
na maana. Pia ameshauri wanachuo kusikiliza sera za wagombea kwa umakini mkubwa ili kuepuka KUUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA.
MSHAURI WA WANAFUNZI ALITUMIA FURSA HIYO KUWAASA WAGOMBEA KUTUNZA MAZINGIRA HASA KUTOBANDIKA MABANGO SEHEMU ZISIZO RASMI
NAYE MAKAMU WA CHUO AKASEMA;
Makamu mkuu wa chuo amewatakia wanafunzi kampeni njema zenye baraka na fanaka na zinazozingatia sheria na taratibu za chuo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni