TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu imepokea na
kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili ambayo ilipitia
adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za Maadili na kupewa
Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na
Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo
adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa
kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu
inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais
kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za
CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili
wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote
wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine
watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko
ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya
wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na
kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata
uteuzi wa nafasi wanayoiomba.
Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
22/05/2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni