ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 21 Mei 2016

Mama aua mwanawe kwa kumuibia 8,000/-

Imeandikwa na Ahmed Makongo, Bunda
MWANAMKE mmoja anashikiliwa na polisi wilayani Bunda, mkoani Mara kwa tuhuma ya kumuua mtoto wake kwa kipigo, baada ya kumtuhumu kumuibia Sh 8,000.
Kamanda wa polisi mkoani Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi Ramadhan Ngazi juzi alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo, lililotokea majira ya saa 11:30 jioni katika mtaa wa majengo eneo la Bunda Day mjini hapa.
Pili Omondo (28), mkazi wa mtaa huo alimpiga kwa fimbo kichwani mtoto wake ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Kabarimu na kumsababishia kifo.
Alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Wakuru Rungu (9) na kwamba baada ya kipigo hicho alimbeba na kumpeleka hospitalini, akidai kwamba amegongwa na pikipiki na ndipo muda mfupi akapoteza maisha. Kamanda Ngazi alisema kuwa mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na polisi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji ya mwanawe.
Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa mwanamke huyo alimpiga mtoto wake kwa kumgongesha kichwa ukutani akidai ni mwizi sugu na kwamba baadhi ya majirani walipomzuia alidai kwamba hata kama akimuua ni mwanawe.
Katika tukio lingine, mwanamke mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake amejifungua kichanga na kukitupa pembezoni mwa barabara kuu ya Mwanza-Musoma, katika eneo la mtaa wa Balili mjini hapa.

Hakuna maoni: