KAMBI Rasmi ya Upinzani bungeni imekataa kusoma maoni yake kuhusu
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
baada ya kutakiwa kuondoa maneno yanayokiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.
Ilikataa kufanya hivyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu kuagiza Kamati ya Kanuni za Bunge pamoja na kiongozi wa kambi hiyo ya upinzani ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema, kukutana na kurekebisha maoni yao kabla ya kuyawasilisha bungeni.
Aliagiza hivyo jana kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara na Waziri Charles Kitwanga, baada ya kueleza kuwa alipopitia maoni ya kambi ya upinzani aligundua kuwa yalikiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni