ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 5 Mei 2016

Walimu kunolewa wakiwa kazini

WALIMU wa shule za msingi na sekondari nchini watapatiwa mafunzo na Serikali wawapo kazini ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji.
Mafunzo hayo yatahusu matumizi ya stadi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), sayansi, hisabati na lugha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya alisema mafunzo hayo ni miongoni mwa mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha elimu inayotolewa nchini inakuwa na ubora wa hali ya juu.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) aliyetaka kufahamu mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuinua ubora wa elimu nchini.
Manyanya alitaja mikakati mingine kuwa ni kutoa mafunzo kwa walimu wa darasa la kwanza na la pili katika kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
“Ili kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya ubora wa elimu itolewayo, ofisi ya uthibiti ubora wa shule kanda na wilaya zinaendelea kuimarishwa kwa kuongeza idadi ya wathibiti ubora wa shule na vitendea kazi,” alisema.

Hakuna maoni: