ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 12 Mei 2016

Tanzia: Msanii wa Vichekesho Mohammed Abdallah (Kinyambe) Amefariki Dunia

 
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia Jumatano hii baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii baada ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku wakiandika RIP Kinyambe.

Mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.

“Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu Pia watu wake wa karibu akiwemo Mke wake wanadai imetokana na kujaa Kwa maji kwenye mapafu, ila jana ndo amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.

Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.

“Kusema kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikikamilika tutaweka wazi,” alisema Mkono.

Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho..

Mungu amlaze mahali  mahali pema peponi -Amina

Msanii Maalufu wa tasinia ya uigizaji wa comedy amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo .Sababu ya kifo chake ikiwa bado haijajulikana ila  kifo hicho kimetokea katika hospital ya mkoa wa mbeya  .mungu amlaze mahali pema peponi kinyambe.
Mwili umechukuliwa na mazishi yake yanatarajia kufanyika Uyole mbeya


Hakuna maoni: