ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 19 Mei 2016

MAGAZETINI:#Cannavaro aitwa Stars, Kabunda, Mgunda ndani

Imeandikwa na Rahel Pallangyo
KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 27, akiwemo nahodha wa zamani wa timu hiyo aliyetangaza kustaafu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Pia katika kikosi hicho ameita winga chipukizi Hassan Kabunda wa Mwadui FC ya Shinyanga, ambaye ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja’ (sasa marehemu).
Mkwasa pia amemjumuisha mshambuliaji Jeremiah Juma wa Prisons ambaye ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union, Juma Mgunda.
Kikosi hicho kinajiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017), ambapo kabla ya kuivaa Misri itacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkwasa amesema amemjumuisha Cannavaro kwani baada ya kupona ameonesha kiwango kikubwa na kusema hajawahi kupata barua yoyote kutoka kwake inayomtambulisha kuwa amestaafu kuichezea timu hiyo.
Cannavaro kwa nyakati tofauti alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa amestaafu kuchezea timu hiyo, baada ya Mkwasa kumtangaza Mbwana Samata kuwa nahodha wa Taifa Stars. Alisema amemuita Cannavaro na kumuacha beki wa Yanga, Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
Kikosi kamili na timu zao katika mabano ni Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Horoub, Mwinyi Haji na Juma Abdul (Yanga), Aggrey Morris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vincent Andrew (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KRC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Yanga) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Hakuna maoni: