Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika
video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana
''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa
mahakama ya juu''.
Video hiyo ilisambazwa kwa kasi
kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia
mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu
nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika
uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza
Besigye na Amama Mbabazi.
Kadhalika,
Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya
kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na
Amama Mbabazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni