ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 11 Juni 2016

Juma Abdul, Telela kuwakosa Waalgeria

Imeandikwa na Vicky Kimaro.
WACHEZAJI mahiri wa Yanga, Juma Abdul na Salum Telela, hawatakuwepo katika kikosi cha Yanga kitakachoondoka nchini kesho kwenda Uturuki kwa kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) dhidi ya MO Bejaia ya Algeria mwishoni mwa wiki ijayo.
Hata hivyo wachezaji wapya wa timu hiyo, mabeki Hassan Kessy kutoka Simba, Vicent Andrew ‘Dante’ kutoka Mtibwa na Juma Mahadhi kutoka Coastal Union ni miongoni mwa nyota watakaokuwemo katika msafara huo.
Meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh alisema jana kuwa wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali. “Juma Abdul ni majeruhi, hivyo hatoweza kwenda, Telela yeye mkataba wake umeisha na mpaka sasa uongozi bado haujamuongezea,” alisema Meneja huyo.
Hata hivyo,Telela inadaiwa tayari amefanya mazungumzo na timu za Simba na Azam kwa nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Kwa mujibu wa Saleh, wachezaji Mahadhi, Dante na Kessy watakuwepo kwenye msafara huo na kwamba wanaamini timu yao itaenda kufanya vizuri ugenini.
Alisema mara baada ya mchezo na MO Bejaia watarejea Uturuki kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na watarejea nchini siku mbili kabla ya mchezo huo.
Yanga imepangwa Kundi A katika michuano hiyo na TP Mazembe ya DRC, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana na itaanza ugenini nchini Algeria wiki ijayo. Kwa upande wa Kundi B zipo timu za Kawkab Athletic, Fath Union Sports zote za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli ya Libya.

Hakuna maoni: