Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko zito kikitaka
Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika mwezi ujao, vinginevyo
watatumia nguvu ya umma kuuzuia.
CCM
kimeitisha mkutano mkuu maalumu unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini
Dodoma, kwa lengo la Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete
kumkabidhi uongozi wa chama, Rais John Magufuli.
Kauli
ya kutaka Polisi kuzuia mkutano huo kama inavyofanya kwa vyama vingine
vya siasa, ilitolewa juzi mjini Moshi na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana
wa Chadema (Bavicha), Julius Mwita.
Msimamo
huo wa Chadema ambao uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho
Zanzibar, Salum Mwalim unafuatia Polisi kuzuia mahafali ya wahitimu wa
vyuo vikuu ambao ni wanachama wao.
Akizungumza
na wanahabari, Mwita alikwenda mbali na kudai kuwa, Chadema
watalifungulia Jeshi la Polisi kesi ya madai ya fidia kwa kuvuruga
mahafali ya Chaso mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Ukisoma
barua yao wamesema wamezuia mikutano ya hadhara sasa kama wanakuja hadi
kwenye vikao vya ndani, hatuwezi kuendelea kukubali jambo
hili.Tumetumia busara sana,” alisema Mwita na kuongeza:
“Msipouzuia Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma Julai 23 tunakuja kuuzuia sisi... yaani muwe tayari kusafiri kwenda Dodoma tukauzuie ule mkutano la sivyo, wauzuie kama walivyouzuia mikutano yetu.”
Mwita alimgeukia Mwalimu na kumweleza kuwa hiyo ni lugha ya ujana na inatekelezeka, akawahoji vijana wa Chaso waliokuwapo: “Wangapi mko tayari kuja Dodoma?” Wote wakaafiki.

“Intelijensia
ya polisi ni ya kiumbea, inayoweza kujua tu Chadema wanakwenda kwenye
mkutano, haiwezi kujua watu wamejificha wana bunduki na risasi 300
kwenye mawe kule Mwanza,” alidai.
Mwalimu alisema utaratibu wa Polisi na Serikali lazima ukome na kwamba wao ni viongozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni