Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.
Upande
wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola
akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum
Mohammed.
Kongola
alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam
mshtakiwa alitamka maneno ya dhihaka kwa nia ya kushawishi na
kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Alinukuu maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka
ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila
mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila
sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani
ya giza nene"
Mshtakiwa
alikana mashtaka hayo.Upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na
uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande
wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo,
Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni
mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.
Hakimu
Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini
wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milioni 2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni