ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 23 Juni 2016

TCU yaita wenye kero

Imeandikwa na Lucy Ngowi
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa fursa kwa wananchi wenye kero, maoni na changamoto kuhusu masuala ya elimu ya juu hususani udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu, wayawasilishe kwao.
Ofisa Habari Mwandamizi wa tume, Edward Mkaku alisema jana mkakati huo umefanyika kutekeleza agizo kutoka Ofisi ya Rais –Menejimenti na Utumishi wa Umma, lililotaka taasisi hiyo iadhimishe wiki ya utumishi wa umma kwa kusikiliza kero, maoni na changamoto.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkaku alisema tangu jana saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana, walipokea wananchi 44 waliowasilisha maoni yao.
Wengi wao ni waliokuwa wakiulizia mwongozo wa kudahiliwa vyuo vikuu ambao kwa mwaka huu haujatoka.
Pia waliulizia mfumo wa kuhama kutoka chuo kimoja kwenda kingine, mfumo wa udahili unavyofanya kazi na utambuzi wa vyeti.
Hata hivyo, alisema wamebaini wananchi wengi wamekuwa wakichanganya kazi za tume na za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Hakuna maoni: