Imeandikwa na Jeremiah Vitalis
Wabunge watatu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kuanzia Juni 30, 2016.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao 10 vya Bunge kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.
Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kile alichoelezwa kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake.
Hukumu hiyo imesomwa na Naibu Spika wa Bunge Dr Tulia Ackson baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo ilijiridhishwa kuwa kitendo hicho ni kosa.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na Mbunge wa Simanjoro, James Ole Millya, Simanjiro wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kila mmoja kwa makosa ya kusema uongo bungeni.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja lililojadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2016/17.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni