Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema kuwa
baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walioondolewa chuoni hivi
karibuni hawakuwa na sifa za kujiunga na masomo chuoni hapo.
Akizungumza
leo katika uzinduzi wa Maktaba mpya ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Rais Magufuli amewataka watanzania kuweka siasa kando
nakuzungumzia masuala ya msingi, huku akiwashangaa wanasiasa
waliojitokeza kuwatetea wanafunzi hao.
“Nimeshukuru
wale vijana wameondoka. Wanasiasa haohao, ‘eti ooh.. hao vijana
wamekosa pa kulala.. it’s nonsense’. Taifa letu tuliweke mbele kwanza.
Siasa zije nyuma,” alisema.
Alisema
kuwa baadhi ya wanafunzi ambao walibainika kuwa na elimu ya kidato cha
nne waliofeli masomo yao na kuruhusiwa kuendelea na masomo ya elimu ya
juu ni watoto wa viongozi.
“Ukimchukua
mtoto wa form four ukampeleka pale, hata kama atafanikiwa kupata
degree… itakuwa ya ajabu. Na baadhi ya watoto waliopelekwa pale ni
watoto wa viongozi. Watoto wa Maskini wenye qualification wamekosa
nafasi za kwenda Chuo Kikuu. Watoto wa watu fulani fulani wanapelekwa
wakati walifeli. It can’t be,” Dk. Magufuli alisisitiza.
Rais
Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake haitaruhusu fedha zinazopaswa
kutumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kupelekwa kwa ‘vilaza’ huku
waliofaulu wakikosa mikopo ya elimu ya juu.
Dk.
Magufuli ameahidi kuwa Serikali yake itahakikisha wanafunzi waliofaulu
kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili (division 1 &2)
wanajengewa mazingira mazuri ya kuendelea na masomo.
“Waliofeli watafute vyuo vyenye size yao,” alisisitiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni