ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 20 Aprili 2015

AJIRA KWA WALIMU 2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA


2.0 AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2014/2015
Kwa kawaida upangaji wa walimu ajira mpya hufanywa na OWM
TAMISEMI baada ya kupokea arodha ya walimu kutoka katika vyuo na
vyuo vikuu kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya
kuhitimu na kufuzu kozi zao. Hata hivyo upangaji huo unatakiwa
kuzingatia dhamira ya serikali ya kuleta usawa kwa kupanga walimu
kwenye halmashauri mbalimbali kulingana na mahitaji.
Ili kuhakikisha kuwa kuna usawa, serika;li kupitia OWM TAMISEMI na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilifanya ufuatiliaji wa kina hadi
ngazi ya shule kubaini kwa uhakika zaidi mahitaji halisi ya walimu kwa
kila halmashauri na kila shule. Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa
halmashauri na shule hasa za mjini zenye walimu wa ziada na zingine hasa
za vijijini ambazo zina upungufu mkubwa wa walimu.
Napenda kuwaarifu kuwa taarifa hizo zimetusaidia kuwapanga walimu
wapya kwa usawa na haki ili kuondoa uwiano usio ridhisha kwenye
maeneo mengi ya vijijini. Hivi sasa tunakamilisha taratibu mahususi za
kupata kibali kwa ajili ya ajira za walimu na upatikana wa fedha za
kuwalipa stahili zao zinakamilishwa ili kuwezesha walimu wapya kuanza
ajira rasmi ifikapo tarehe 1 Mei, 2015.
Napenda kuweka bayana kuwa Maeneo mengi ya mijini kwa maana ya
Majiji, Manispaa na Miji hayajapangiwa walimu na baadhi yamepangiwa
walimu wachache kulingana na mahitaji. Kama nilivyoeleza hapo awali
kipaumbele kimetolewa katika maeneo ya vijijini na halmashauri ambazo
zina upungufu mkubwa wa walimu. Nawashauri na kuwasihi walimu
wapya waende kuripoti kama halmashauri na shule watakazopangiwa na
si vinginevyo. Ni imani yangu walimu wapya wote watakuwa tayari
kufanya kazi maeneo yenye mahitaji.
Orodha rasmi ya walimu na vituo watakavyokuwa wamepangiwa
itapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa –OWM TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 25/4/2015.
IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU OWM – TAMISEMI
TAREHE 13/04/2015

Hakuna maoni: