ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 22 Aprili 2015

SIASA NI MCHEZO





  






Kwani kuna ambaye hajui kama bajeti ya nchi yetu inapitishwa na wanasiasa? Kuna asiyetambua kwamba kilimo kinachoitwa uti wa mgongo wa taifa hili nacho kinasimamiwa zaidi na wanasiasa? Hivi kweli kabisa huenda akatokea mtu aseme kuwa hajui kama elimu yetu ipo chini ya uangalizi na usimamizi wa wanasiasa?

Jamani!Hata ulinzi na usalama wetu nao hatujui kama upo chini ya himaya ya mwanasiasa? Hapana, huyu ni lazima nimtaje. Yeye ndiye amiri jeshi mkuu anayepigiwa saluti na wanausalama wote. Ndio mpaka afya zetu wanaopitisha bajeti yake ni wanasiasa tu na sio wengine. Hakuna kinachofanyika chini ya jua la nchi yetu lisiwe na mkono wa wanasiasa kwa sababu bajeti nzima inapitishwa na haohao.

Kifupi tunaweza kusema kwamba maisha yetu yote yapo chini ya mwamvuli wa siasa na kwa maana hiyo tusiifanyie mzaha. Ndio, tusicheze kabisa na siasa kwa sababu tutakuwa tunachezea maisha yetu wenyewe. Kwani si mnajua kama katiba ya nchi ambayo ndio sheria mama nayo miongoni mwa walioitunga na kuipitisha ni wanasiasa?

Hata katiba inayopendekezwa, wanasiasa walikwuwepo nahata jengo lililotumika ni lilelile linalotumiwa na wanasiasa kila uchao na uchwao. Si utani jamani siasa ndio yenye nguvu na nafasi kubwa kuliko chochote Tanzania na ndio maana hata wanataaluma bobezi nao hawashikiki kwenye siasa. Huko kuna ‘mshiko’ wa maana hata kama pakiwa kuna fujo na vurugu.

Lakini hata hivyo ukiachana na nafasi iliyokuwa nayo siasa hapa nchini, bado hatuwezi kuacha kusema kuwa ni mchezo mchafu. Mara ngapi mfano kule bungeni kumetokea vurugu? Nani hakuwahi kushuhudia washa zima maikrofoni inayofanywa na waheshimiwa wanasiasa (wabunge) ambao ndio tumewaamini wakatuwakilishe? Ni kweli tumewatuma wakaropoke au kupiga kelele zisizokuwa na natija kwetu? 
Tumewatuma wakatetee maslahi ya vyama vyao na matumbo yao?

Tukubali tu kwamba siasa ni mchezo mchafu unaowachafua wengi, wake kwa waume na vijana kwa wazee. Imechafua upande wa vyama vya upinzani na chama tawala. Inawachafua wasomi wetu na wanataaluma waliofurika huko.

Mtangazaji wa masuala ya siasa John Calvin Thomas (Cal Thomas) aliyezaliwa Disemba 2, 1942 katika jimbo la Washington D.C nchini Marekani,anasema kuwa sababu mojawapo ya watu kuichukia siasa ni kwamba ukweli ni mara chache kuwa lengo la mwanasiasa. Hii ina maana kuwa wanasiasa wengi kama sio wote hawaupi ukweli nafasi yake hasa kwenye malengo yao ya kisiasa mbele ya wananchi.

Hakuna maoni: